Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Tunasemaga Locuta causa finita !
Hata Polepole analijua hilo !
Wabishi wakae kwa kutulia tu!
Hakuna mahali Katiba imevunjwa !
Kwa maana Katiba hiyo hiyo ndio iliyompa Mkuu Madaraka yote hayo makubwa na hao wabishi wanaolalama kwa sasa hawakuwahi kulalamika kuhusu hiyo Katiba !

WHY NOW ! ? Big question mark ⁉️
 
Mwaka 1985 Mwinyi alipita kwenye mchakato kwa kumshinda Salim..hivyo hivyo Mkapa,Kikwete,Magufuli wate walishindanishwa ndani ya Chama huyu Samia ni Rais kujiteua bila kupita kwenye mchakato..
Unajua kusoma kweli? Nauliza tena, hao wote kwenye awamu yao ya pili walishindanishwa na nani?
 
Bila shaka utakua kamanda mwenzetu wa CHADEMA.. maana bila kutukana kamwe utaweza kuendelea kuitwa kamanda.
Huyo Mama yako hapendwi ila analazimisha kupendwa, mngempambania na matusi waliyomporoshea Wakenya !
 
Ni mawazo yangu maana nimepima upepo kitambo sana humu tangu mwaka 2008, sijui wewe ulijiunga lini ndugu yangu? umepima upepo? tunakoelea Panya road watatamalaki...
Mkuu nimekuelewa sana. Kumbe haya ni mawazo yako na wala wewe si Mjumbe aliyetumwa kutuletea ujumbe husika. Kama ulivyosema awali, Mjumbe hauwawi. Hivyo kwa uhai wako katika Jukwaa hili utakuwa umejiandaa vizuri sana kwa vipigo kutoka pande zote. Kila la kheri.
 
....Wakati wafuatao wanatafuta kugombea nafasi au awamu yao ya pili walishindanishwa na akina nani?
Aiseeee!
Unajua kusoma kweli? Nauliza tena ,awamu zao za pili walishindanishwa na nani?
Sasa na mimi na kuuliza unajua kuandika na kusoma kweli? Ama hilo neno 'au' ulikosea kuandika 'ua' . Ukiujua huu wengine wanaujua ule. JF hapa, nyata taratibu.
 
Inashangaza sana, Samia anavunja katiba ya CCM kwa kujiteua mwenyewe na Nchimbi wake huku wanaCCM wanaangalia kama kwamba hakuna wanaume wenye uwezo wa kuongoza nchi .... 😲
shithole countries. wezi na mafisadi wanataka waendelee na yao
 
Mkuu nimekuelewa sana. Kumbe haya ni mawazo yako na wala wewe si Mjumbe aliyetumwa kutuletea ujumbe husika. Kama ulivyosema awali, Mjumbe hauwawi. Hivyo kwa uhai wako katika Jukwaa hili utakuwa umejiandaa vizuri sana kwa vipigo kutoka pande zote. Kila la kheri.
Wavilete tu... kelele zimezidi sana humu nchini, kila sehemu moto, moto, moto, mara Polepole na sukuma gang, mara Mpango kajiuzuru, mara Kasim Majaliwa.. kuna tatizo mahali fulani. ktk timu ya mpira, mara nyingi ni kocha anatakiwa kujiudhuru na si vinginevyo , hata kama amefanya usajili wa akina Messi, Ronadinho , na wengineo. Wasipo funga , lawama zote ni kwake na lazima ateme bungo.. Ndio maana ya bandiko langu.
 
Naunga mkono hoja.
Mzalendo wa kweli hawezi kuona mambo yanaharibika kwa kuangalia maslahi ya tumbo lake na familia yake tu.
Hivyo kama na yeye pia ana punje ya uzalendo, kwa hapa tulipofikia, busara kwake ni kuachia ngazi.

Sisi Watanzania wa kawaida hatutaki tena kuongozwa na wale ambao wanatuongoza bila ridhaa yetu maana wengi wao huwa wanaongoza kwa nyodo sana na hawajali maslahi ya watu wa hali ya chini.

Nakumbuka zile kauli zake kwa wajane za kusema " hebu mwondosheni huyo maana anashughulisha watu hapa!"

Sidhani kama itakuwa busara kuendelea kuongozwa na yule ambaye anatanguliza maslahi ya wenye nacho na kuwaacha wengi wapambane na hali zao.

Busara na hekima ni kuachia ngazi kama alivyofanya Joe Biden.
 
Huu ujumbe umfikie SAMIA SULUHU HASSAN kupitia watu wake wa karibu. Chawa hakikisheni ujumbe huu anausoma mama yenu, asipoelewa basi atakua na "kishimbe".
 
Mheshimiwa sana,

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako- Achia ngazi kama Biden alivyo fanya- hupungukiwi na kitu... waachie pia wafungwa wa kisiasa wakiwemo pia wale ulio watembelea Nairobi- Mungu wa Mbinguni atakubariki sana.​

 
Polepole atalindaje mkataba wa kinyonyaji wa DP WORLD, na waarabu walionunua hifadhi ya ngoro ngoro na kuwafukuza wamasai?
Fanya utafiti kidogo kuhusu Ngorongoro..ni dude kubwa kuliko unavyodhani ..
 
Rais Samia: Fikiria Hatua Sahihi kwa Maslahi ya Taifa na Familia Yako Pia.

Katika siku za hivi karibuni, inavyoonekana katika jicho la pembeni kwamba kumekuwa na mjadala mkali kuhusu mustakabali wa uongozi ndani ya Chama chako cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, hasa kutokana na mienendo ya baadhi ya viongozi waliobaki kama urithi kutoka awamu ya tano ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Hoja zifuatazo hapa chini zinaashiria umuhimu wako kama wewe Raisi wetu- Samia Suluhu Hassan kufanya maamuzi magumu lakini ya busara kwa wakati huu.

kwanini ni busara kama wewe Rais Samia kuangalia uwezekano wa kuachia ngazi kwa amani, ili kulinda heshima yako, ustawi wa familia yako na mustakabali wa taifa kwa ujumla wako:

1. Viongozi wengi wa awamu ya Magufuli wana ajenda zao hata kama wako kimya – wanapima upepo:
  • Wengi wa viongozi waliolelewa na kupewa nafasi kubwa wakati wa awamu ya Magufuli wanaonekana bado kushikilia misimamo na mikakati yao ya zamani.
  • Kuna ishara kwamba wanajaribu kurejesha baadhi ya sera na mitazamo iliyotamalaki wakati huo, jambo ambalo linaweza kuleta msuguano na dira mpya unayoijenga Rais Samia.
  • Mwisho wa siku, Rais Samia unaweza kuishia kupambana na kundi lako mwenyewe ndani ya chama, hali itakayochochea migawanyiko mikubwa.
2. Hali hii inaweza kukutesa sana katika miaka mitano ijayo
  • Kama hali hii haitadhibitiwa mapema, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko ya ndani ya chama kuibuka hadharani.
  • Kelele za kisiasa zitakua kubwa, zitaathiri utulivu wako wa akili na kufanya kuongoza taifa kuwa jambo gumu mno.
  • Badala ya kutumia muda wako katika kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia, Rais Samia utaishia kuzima moto wa migawanyiko isiyoisha.
3. Kwa nini usiruhusu mchakato huru wa kumpata mgombea mpya wa urais ndani ya CCM?
  • Hii itakuwa njia ya kuonesha ukomavu wa kidemokrasia ndani ya chama na pia kutoa nafasi kwa damu mpya yenye kukubalika kwa pande zote.
  • Ni bora kuondoka kwa heshima na maridhiano kuliko kushikilia madaraka hadi hali iwe tete na kuishia kubeba aibu isiyo ya lazima.
4. Fuata mfano wa Joe Biden nchini Marekani:
  • Rais Biden mara nyingi alitoa ishara kwamba yupo tayari kuweka mbele maslahi ya taifa na familia yake, kuliko kushikilia madaraka kwa nguvu.
  • Rais Samia unaweza kufanya vivyo hivyo, kwa kuzingatia afya yako ya kiakili na faraja ya familia yako- Mume, watoto na wajukuu zako ambao wanakutegemea, watafarijika wakikuona ukiwa na amani.
5. Pension na mafao yako yako salama hadi kiama
  • Kama rais mstaafu, utaendelea kulipwa pensheni yako, kuheshimiwa na kulindwa na taasisi za nchi.
  • Kwa hiyo huna haja ya kuendelea kuvumilia presha ya kisiasa inayoweza kukuchosha kimawazo na kukupunguzia furaha ya maisha.
6. Ni heri kuachia ngazi ukiwa bado unaheshimiwa.
  • Ukichukua hatua sasa, utaondoka madarakani ukiwa bado una hadhi kubwa na unapendwa na sehemu kubwa ya wananchi.
  • Hii ni bora kuliko kusubiri hadi hali iwe mbaya, uonekane kulazimika kuondolewa kwa aibu au shinikizo.
7. Mwachie Polepole na kundi lake waendelee.
  • Ukiwa kweli kuna mkakati unaopikwa na baadhi ya makundi ndani ya chama au serikali yakO, ni bora Uwaachie waendelee na Ujitoe kwa heshima.
  • Utabaki kuwa rais Uliyependa maridhiano na ustawi wa taifa kuliko maslahi binafsi.
Mwisho:
Rais Samia bado una nafasi kubwa ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu. Uamue kwa busara, kwa ajili ya amani yako binafsi, familia yako na taifa kwa ujumla, hutakuwa wa kwanza wala wa mwisho kufanya hivyo.
Sio kuchelewa na waka hauta chelewa. Ukiamua sasa, Utaacha urithi wa kipekee wa kiongozi wa kwanza mwanamke aliyesimamia mpito wa kisiasa kwa utulivu na hekima.

Povu ruksa. Mjumbe hauwawi- message sent and delivered
Bandiko hili Bado lina dumu kwa Muheshimiwa sana mama Rais wetu - Samia Suluhu Hassan...
 
Mheshimiwa sana,

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako- Achia ngazi kama Biden alivyo fanya- hupungukiwi na kitu... waachie pia wafungwa wa kisiasa wakiwemo pia wale ulio watembelea Nairobi- Mungu wa Mbinguni atakubariki sana.​

 
Back
Top Bottom