Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Hivi inamaana hata sasa bado tu Chief hajashtuka tu kwamba mvinyo umeiva tayari ama ndo sikio ....?
Siku zote wanasema ukija kuiona kansa kwa macho yako ya nyama basi tambua kwenye adubini wadusu wanalingana na ukubwa wa nzi. So far pengine umesahau tu na kumkumbusha kwamba si tu akina Polepole na kundi lake bali pia na watanzania kiujumla wameshachoka kupita kiasi. Enzi zimekwisha na kila mchuma janga ula na wa kwao
 
2025-2030 unaweza kuwa wakati mgumu sana Kwa Rais Samia, Kwasababu Hawa Kina Gwajima na mpina anaoshindwa kujizuia na kuwajibu Kwa anger baada ya Uchaguzi wataibuka wengi sana sana
Watakuwa hawana Cha kupoteza
 
Nilifikiri utasema unaomba akubali kufanya reforms kwenye Katiba 😳 !
Kumbe wewe Mkuu unataka Mheshimiwa aachie ngazi ???!! 🤣🤣

Hiyo ni ndoto Bandugu !
Wanaachiaga kama Afya imezorota sana kama Biden Afya ya Akili ilitetereka ikawa hakuna namna nyingine !!
reform hataki, iliyibaki niu kuachia ngazi kwa hiari bila shuruti
 
Migogoro inayoesemwa ipo ni ya kufikirika
Ni watu wachache tu wanaodhani wao tu ndio wana hati miliki ya chama na serikali ns utawala
Mama Samia yuko vizuri

Na nishukuru kamati za Usalama ndani ya CCM waliofanya maamuzi ya jina la mgombea uraisi kufanyika mapema hapo hapo kikaoni

Kumwiepushia nchi mengi.Sasa hivi wameanza kutoka kwenye mashimo.na kuonyesha rangi zao halisi
 
Wakati tunaendelea kujielimisha nk .. Mleta mada naomba kuuliza kitu. Wakati wafuatao wanatafuta kugombea nafasi au awamu yao ya pili walishindanishwa na akina nani?
Hayati ALI HASSAN MWINYI
Hayati Ben Mkapa
Hayati John Magufuli
Mwisho tunajua nini shida ya haya yote.. Dini yake na kua ni mtanzania asili ya Zanzibar na hamna zaidi ya ilo.
Maswali yako yanafikrisha sana- sina majibu yake- msema kweli mpenzi wa Mungu...
 
Mawazo ya kijinga.

Suluhisho ni nguvu ya kura na agenda ya wananchi.

Siyo kubadilisha genge la wanasiasa kila siku.
hizo kura tayari zimeisha dokolewa hata kabla hazijapigwa... sasa kama ndio hivyo, wanao sema NRNR na october tunatiki, wapi wako sahihi?
 
Rais Samia: Fikiria Hatua Sahihi kwa Maslahi ya Taifa na Familia Yako Pia.

Katika siku za hivi karibuni, inavyoonekana katika jicho la pembeni kwamba kumekuwa na mjadala mkali kuhusu mustakabali wa uongozi ndani ya Chama chako cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, hasa kutokana na mienendo ya baadhi ya viongozi waliobaki kama urithi kutoka awamu ya tano ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Hoja zifuatazo hapa chini zinaashiria umuhimu wako kama wewe Raisi wetu- Samia Suluhu Hassan kufanya maamuzi magumu lakini ya busara kwa wakati huu.

kwanini ni busara kama wewe Rais Samia kuangalia uwezekano wa kuachia ngazi kwa amani, ili kulinda heshima yako, ustawi wa familia yako na mustakabali wa taifa kwa ujumla wako:

1. Viongozi wengi wa awamu ya Magufuli wana ajenda zao hata kama wako kimya – wanapima upepo:
  • Wengi wa viongozi waliolelewa na kupewa nafasi kubwa wakati wa awamu ya Magufuli wanaonekana bado kushikilia misimamo na mikakati yao ya zamani.
  • Kuna ishara kwamba wanajaribu kurejesha baadhi ya sera na mitazamo iliyotamalaki wakati huo, jambo ambalo linaweza kuleta msuguano na dira mpya unayoijenga Rais Samia.
  • Mwisho wa siku, Rais Samia unaweza kuishia kupambana na kundi lako mwenyewe ndani ya chama, hali itakayochochea migawanyiko mikubwa.
2. Hali hii inaweza kukutesa sana katika miaka mitano ijayo
  • Kama hali hii haitadhibitiwa mapema, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko ya ndani ya chama kuibuka hadharani.
  • Kelele za kisiasa zitakua kubwa, zitaathiri utulivu wako wa akili na kufanya kuongoza taifa kuwa jambo gumu mno.
  • Badala ya kutumia muda wako katika kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia, Rais Samia utaishia kuzima moto wa migawanyiko isiyoisha.
3. Kwa nini usiruhusu mchakato huru wa kumpata mgombea mpya wa urais ndani ya CCM?
  • Hii itakuwa njia ya kuonesha ukomavu wa kidemokrasia ndani ya chama na pia kutoa nafasi kwa damu mpya yenye kukubalika kwa pande zote.
  • Ni bora kuondoka kwa heshima na maridhiano kuliko kushikilia madaraka hadi hali iwe tete na kuishia kubeba aibu isiyo ya lazima.
4. Fuata mfano wa Joe Biden nchini Marekani:
  • Rais Biden mara nyingi alitoa ishara kwamba yupo tayari kuweka mbele maslahi ya taifa na familia yake, kuliko kushikilia madaraka kwa nguvu.
  • Rais Samia unaweza kufanya vivyo hivyo, kwa kuzingatia afya yako ya kiakili na faraja ya familia yako- Mume, watoto na wajukuu zako ambao wanakutegemea, watafarijika wakikuona ukiwa na amani.
5. Pension na mafao yako yako salama hadi kiama
  • Kama rais mstaafu, utaendelea kulipwa pensheni yako, kuheshimiwa na kulindwa na taasisi za nchi.
  • Kwa hiyo huna haja ya kuendelea kuvumilia presha ya kisiasa inayoweza kukuchosha kimawazo na kukupunguzia furaha ya maisha.
6. Ni heri kuachia ngazi ukiwa bado unaheshimiwa.
  • Ukichukua hatua sasa, utaondoka madarakani ukiwa bado una hadhi kubwa na unapendwa na sehemu kubwa ya wananchi.
  • Hii ni bora kuliko kusubiri hadi hali iwe mbaya, uonekane kulazimika kuondolewa kwa aibu au shinikizo.
7. Mwachie Polepole na kundi lake waendelee.
  • Ukiwa kweli kuna mkakati unaopikwa na baadhi ya makundi ndani ya chama au serikali yakO, ni bora Uwaachie waendelee na Ujitoe kwa heshima.
  • Utabaki kuwa rais Uliyependa maridhiano na ustawi wa taifa kuliko maslahi binafsi.
Mwisho:
Rais Samia bado una nafasi kubwa ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu. Uamue kwa busara, kwa ajili ya amani yako binafsi, familia yako na taifa kwa ujumla, hutakuwa wa kwanza wala wa mwisho kufanya hivyo.
Sio kuchelewa na waka hauta chelewa. Ukiamua sasa, Utaacha urithi wa kipekee wa kiongozi wa kwanza mwanamke aliyesimamia mpito wa kisiasa kwa utulivu na hekima.

Povu ruksa. Mjumbe hauwawi- message sent and delivered
Ni ushauri, anahiari ama kuufuaya au kuuacha, ila kuna mambo nayakubali kwenye ushsuri na mingine hapana. Nakubali pale uliposem
Ni bora kuondoka kwa heshima na maridhiano kuliko kushikilia madaraka hadi hali iwe tete na kuishia kubeba aibu isiyo ya lazima.
Hii ni sawa
  • Wengi wa viongozi waliolelewa na kupewa nafasi kubwa wakati wa awamu ya Magufuli wanaonekana bado kushikilia misimamo na mikakati yao ya zamani.
  • Kuna ishara kwamba wanajaribu kurejesha baadhi ya sera na mitazamo iliyotamalaki wakati huo, jambo ambalo linaweza kuleta msuguano na dira mpya unayoijenga Rais Samia.
Haya ni kweli.
  • Kama hali hii haitadhibitiwa mapema, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko ya ndani ya chama kuibuka hadharani.
  • Kelele za kisiasa zitakua kubwa, zitaathiri utulivu wako wa akili na kufanya kuongoza taifa kuwa jambo gumu mno.
  • Badala ya kutumia muda wako katika kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia, Rais Samia utaishia kuzima moto wa migawanyiko isiyoisha.
Haya hayana tatizo kwake kama kiongozi kwani huu utakuwa muhula wake wa mwisho. Hana cha kukusa.
Kwa nini usiruhusu mchakato huru wa kumpata mgombea mpya wa urais ndani ya CCM?
  • Hii itakuwa njia ya kuonesha ukomavu wa kidemokrasia ndani ya chama na pia kutoa nafasi kwa damu mpya yenye kukubalika kwa pande zote.
Hii si sawa kwa sasa kwasababu lile kundi ulilolitaja hapa ndo watatekeleza kufikia malengo yao.
Ni bora kuondoka kwa heshima na maridhiano kuliko kushikilia madaraka hadi hali iwe tete na kuishia kubeba aibu isiyo ya lazima.
Hili ni sawa lakini atangaze kutokugombea urais. Vingine ni kujitengenezea historia mbaya ya kuondolewa kwa kutokupitishwa. Kumbuka lile kundi bado lipo.
Fuata mfano wa Joe Biden nchini Marekani:
Hili si sawa. Tanzania haifanani kwa vyovyote na Marekani.
Ni heri kuachia ngazi ukiwa bado unaheshimiwa.
  • Ukichukua hatua sasa, utaondoka madarakani ukiwa bado una hadhi kubwa na unapendwa na sehemu kubwa ya wananchi.
  • Hii ni bora kuliko kusubiri hadi hali iwe mbaya, uonekane kulazimika kuondolewa kwa aibu au shinikizo.
Hii ni sawa.

Ningekuwa mimi ndo yeye, ningesikiliza ushauru baadae nikafuata yale ninayojua ni salama zaidi kwangu sio kila ushauri huwa unafuatwa.
 
Mungu anailinda nchi hii, baada ya kufariki JPM malaika Mabeyo akamuongoza Samia kwa kumshika mkono na kuiweka nchi mahali salama.

JK na kundi lake limefaidika na uwepo wa Mabeyo kama malaika mlinzi mkuu imekuwa ni faida njema kwa Taifa.

Hatufahamu hao wengine iwapo wangeichukua ikulu kwa kumuweka pembeni SSH leo hii tungekuwa katika hali gani.

Tatizo la uongozi ni kwamba hakuna anayeweza kuwaridhisha watanzania wote milioni 65, hata huyo hayati JPM aliumiza wafanya biashara wengi sana kwa kiburi tu cha kipuuzi.

Hakuna afadhali ya wote inakuwepo kwa wachache tu ndio maana hakuna rais mwema tangu awamu ya Julius Nyerere.
Tanzania ya sasa lzm uwakere watu ili nchi isonge ila kuwakera huko sio kuwateka , kuwafunga bila makosa
 
Kuna point hapa nimeiona..

Hv Samia angeamua amanilizie hiki kipindi cha Magufuli then a-step down, haya mambo ya uchaguzi 2025 awaachie wengine ambao wako interested... sidhani kama angepungukiwa chochote...

All in all nimengundua binadamu huwa tunajipa presha isiyokuwa na maana.
 
Naamini bado hajachelewa
 
Back
Top Bottom