Rais Samia, fukuza walioukuletea jina la mtu asiye na sifa ili umteue

Rais Samia, fukuza walioukuletea jina la mtu asiye na sifa ili umteue

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mheshimiwa Raisi, kama hilo jina halikuwa pendekezo lako bali uliletewa na wasaidizi wako ili umteue kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, nakushauri uwafukuze mara moja waliohusika kupendekeza kwako jina hilo

Pili, ikiwezekana sitisha kufanya teuzi kipindi hiki na jipe muda wa kutosha kupitia na kuchambua majina kabla ya kuyaleta kwa umma.

Usipotusikiliza, Mheshiimiwa una hatari ya kuharibikiwa mapema sana na inawezekana baadhi ya watu walioteuliwa na mtangulizi wako hawafai kuendelea kufanya kazi na wewe hivyo ni bora uteua watu wako.

Japo mi si mwana-CCM ,ila inawezekana kuna wenzako wanataka uonekane hutoshi kwenye hiyo nafasi ikiwa ni maandalizi ya 2025- nadhani umenielewa.

Mwisho, niseme tunakushukuru kwa kuwa msikivu na huo ndio uongozi.Ubarikiwe sana.
 
images (23).jpeg
 
Hadi amefanya utenguzi alishamalizana nao

Tuendelee kuchapa kazi

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote

Rest well our hero President John Pombe Joseph Magufuli
 
We SI mwana ccm-A Ila ni mwana ccm-B.

Wapinzani kula na kulala yote CCM,Ila kucheza mwaenda kucheza viwanja vya watu.

So Kama mwanafamilia wa CCM una haki ya kutoa ushauri so mbaya
 
Usipotusikiliza, utaharibikiwa mapema sana na ikiwezekana baadhi ya watu walioteuliwa na mtangulizi wako hawafai kuendelea kufanya kazi na wewe hivyo ni bora uteua watu wako.
Mmm ya chadema kwenu yamewashinda ya akina Halima Mdee toka lini wewe ukageuka mshauri wa CCM?
 
Back
Top Bottom