Rais Samia: Hakuna kuingia Mikataba pasipo kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili leo tarehe 29 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Prof. Ibrahim Juma - Jaji Mkuu
Haitoshi kuwa na sheria nzuri ambayo haitimizi malengo ya kutungwa kwake. Zipo sheria ambazo ni vikwazo kwa maendeleo mfano ni ile ya manunuzi.

Sheria zingine za zamani, zina maudhui ya karne ya 19 au 20. Tunahitaji kuziangalia upya.

Hata kwenye ku draft sheria bado tunatumia makaratasi wakati wenzetu wanatumia computer.

Baadhi ya maeneo yataleta changamoto kwenye sheria zetu kwa kuwa hatukufundishwa, mfano eneo huru la Biashara Afrika. Kuna haja ya kutazama mambo haya ili sheria zetu zitusaidie.

Samia Suhuhu Hassan - Rais
Natumaini maboresho yanayofanywa kwenye sekta ya Sheria yataleta tija kubwa kwa taifa hili.

Nawasihi mawakili wote wa Serikali wajisajili, pia napongeza kwa kuanzishwa kwa chama hiki cha Mawakili. Mmepata mlezi mzuri (Mwanasheria mkuu), atawanoa na kuwalea vizuri.

Nawapongeza kwa kuanzisha mfumo (mtandao) wa mawasiliano unaolenga kuboresha kazi zenu. Umetengenezwa na vijana wazalendo, nawapongeza.

Wananchi wetu wengi wana shida nyingi na hawana watu wa kuwasilikiza, mnayo dhamana kubwa ya kuwasikiliza na kuwapa suluhisho. Nendeni mkawasaidie.

Mawakili waitwe mara kwa mara kukumbushwa wajibu wao, wengine wakienda huko wilayani wanajisahau. Pia wafuatiliwe kutathimini utekelezaji wa kazi zao.

Serikali itaendelea kutenga bajeti ya maendeleo kwa sekta ya sheria nchini ili kusogeza huduma bora kwa wananchi.

Tumefungua nchi kwa kiasi kikubwa, wawekezaji wanaingia nchini kwa kasi kubwa. Migogoro inaweza kuanza kutokea, ili tuendelee na uwekezaji mzuri lazima mawakili wa serikali muwe makini kuharakisha kusikiliza migogoro hii kabla haijafika mahakamani.

Lindeni uchumi wetu kwa hali na weledi, nendeni mfanye kazi.

Kuanzia sasa hakuna kuingia mikataba pasipo kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hii itasaidia kupungua changamoto na migogoro na wawekezaji kwa kuwa mikataba mingine husainiwa kienyeji.

Simamieni haki, Mungu anapokuteua usimamie sekta hii anataka uwe muadilifu. Kasimamieni haki.

Tatizo la kusweka watu mahabusu litapungua ikiwa kesi zitasikilizwa mapema kabla hazijaenda mahakamani. Kuweni waadilifu na wenye uaminifu.

Changamoto hizi zifanyiwe kazi haraka. Nitaitisha kikao tuje tujadili, mtoe presentation, tugawane majukumu na kila mtu apewe jukumu la kwenda kufanya.

=====

MHE. RAIS SAMIA AZINDUA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu, OWMS, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Mawakili wote wa Serikali ambao hawajasajiliwa kwenye rejista ya Mfumo wa Taarifa wa Mawakili wa Serikali kujisajili kabla ya muda kupita ili watambulike na Mfumo wa Kieletroniki wa Taarifa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ujulikanao kwa jina la OAG-MIS.

Mhe Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali (Public Bar Association) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma wenye Kauli mbiu isemayo, “Utekelezaji wa Majukumu Unaozingatia Sheria ni Nyenzo Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa”.

“Amri inapotoka Wanasheria wajisajili na muda umetolewa kama mtu hajajisali awe na dharura ya maana sana, ama alikuwa mgonjwa hospitalini hawezi au alipokuwa hakuna mtandao hakupata taarifa kwa wakati lakini kama muda utapita na usajili hajafanya basi Mwanasheria Mkuu nakutaka kusimamia hilo”, amesema Mhe. Rais Samia

Amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwahimiza wale ambao bado hawajajisajili wajisajili kwenye mfumo wa OAG-MIS vinginevyo baada ya muda kupita hawatatambulika kama Mawakili wa Serikali na itabidi watafute sekta za nje wajisajili au kupewa msamaha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mhe. Rais Samia amepongeza uanzishwaji wa Chama cha Mawakili wa Serikali cha kitaaluma na kusema uwepo wake utasaidia zoezi la kuratibu utendaji kazi wa Mawakili wote wa Serikali walio katika utumishi wa umma nchini na mmepata mlezi mzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayeweza kuwasemea katika masuala yenu ya kitaaluma, kikazi, kinidhamu na kimaslahi.

“Lakini nimefurahishwa kusikia kwamba Chama hiki sasa kilichoundwa kitafanya kazi kwa karibu na Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS), lakini pia nimefurahishwa na kusikia uhusiano wa karibu wa kazi baina yenu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar”, amesema Mhe. Rais Samia

Aidha, amesema itakuwa ni rahisi kuwasiliana kupitia mfumo huo wa Mawakili wa Serikali ambao ameuzindua na kusema ni dhahiri maboresho hayo yataongeza ari na tija kwa Mawakili wa Serikali wanapotekeleza majukumu yao katika maeneo mbali mbali nchini.

Akimkaribisha Mhe. Rais Samia, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mkutano huo ulitanguliwa na kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara, Taasisi, Idara na Halmashaurizote nchi nzima na kuelezwa kuhusu mpango wa kuanzisha Chama cha Mawakili wa Serikali.

Dkt. Ndumbaro amesema chama hiki kitakuwa kikisimamia masuala ya kitaaluma na masuala ya kimaadili ya Wanasheria na ni fursa nzuri ya kutoa changamoto za kimaadili ambazo zimekuwa zikiwakabili na itawezekana tu kama Mhe. Rais Samia atakubali ombi la kuzindua chama hicho.

“Mhe Rais Samia kupitia Chama cha Mawakili wa Serikali tunatarajia kwamba chama hiki kitaleta umoja wenye nguvu na jukwaa mahususi kabisa la kuishauri Serikali katika mambo mbalimbali ya kisheria na tunatarajia kwamba itakuwa ni sehemu ya majidiliano ya kisheria kwa wanasheria wa Serikali ambalo lilikosekana huko nyuma.

Amewakumbusha Mawakili wa Serikali kwamba kuwa Wakili wa Serikali ni heshima kubwa na heshima ya kuwa Wakili inaendana na wajibu hivyo wanapaswa kuitumikia Serikali ipasavyo, kutumia sheria kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza ndani ya Serikali.

Awali Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewataka watendaji kuhakikisha wanawatumia vizuri wanasheria waliopo kwenye rejesta ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata ushauri kabla hajaingia kwenye mikataba au kabla ya kuvunja mikataba ili wazingatie kanuni na taratibu.

Mhe. Jaji Dkt. Feleshi amesema chama kitakuwa ni jukwaa la Mawakili kujadili masuala mbalimbali ya kisheria yakiwepo ya kimafunzo yanayohusiana na utoaji wa huduma za kisheria na kutatua malalamiko ya kisheria kutoka kwa wadu mbalimbali.

Naye Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Msalama Mkama ameishukuru Serikali kwa kuwa na maono ya mbali na kuanzisha Chama cha Mawakili wa Serikali ambacho kitakuwa kama jukwaa kwa Mawakili hao kujadili masuala yao ya msingi kwenye Sekta ya Sheria.

Bw. Mkama amesema kuwa chama hicho kitaiwezesha Serikali kuwaunganisha Mawakili na kujadili changamoto zao kwa pamoja na kuiwezesha Serikali kufahamu idadi na utendaji kazi wa Mawakili katika Wizara, Taasisi, Sekretariati za Mikoa na Halmashauri zote nchini.

“Chama kitawawezesha Mawakili kushirikishana katika ujuzi walio nao na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika kusimamia mashauri ya Serikali kutoka kwenye taasisi zao na pia kutatua changamoto walizonazo kwa kutumia uzoefu walio nao.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende, Mkurugenzi wa Mashtaka, Slyvester Mwakitalu, Viongozi waandamizi wastaafu wa Sekta ya Sheria nchini akiwemo Mtemi Andrew Chenge.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
IMG-20220929-WA0012.jpg

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, Dodoma kwa ajili ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali.
IMG-20220929-WA0014.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kuangalia namna Mfumo wa kuratibu taarifa za Mawakili wa Serikali unavyofanya kazi. Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
IMG-20220929-WA0015.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali na mfumo wa kuratibu taarifa za Mawakili wa Serikali uliopo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dodoma. Wa kwanza kulia mstari wa nyuma kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende
IMG-20220929-WA0017.jpg

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakiwa kwenye banda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Chama cha Mawakili wa Serikali jijini Dodoma. Anayemsikiliza kwa makini ni Mercy Kyamba, Mkurugenzi Msaidizi Udhibiti Bora wa Ofisi hiyo
IMG-20220929-WA0016(1).jpg

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo akimsilikiliza kwa makini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi Mkutano na uzinduzi wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika jijini Dodoma.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili leo tarehe 29 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Prof. Ibrahim Juma - Jaji Mkuu
Haitoshi kuwa na sheria nzuri ambayo haitimizi malengo ya kutungwa kwake. Zipo sheria ambazo ni vikwazo kwa maendeleo mfano ni ile ya manunuzi.

Sheria zingine za zamani, zina maudhui ya karne ya 19 au 20. Tunahitaji kuziangalia upya.

Hata kwenye ku draft sheria bado tunatumia makaratasi wakati wenzetu wanatumia computer.

Baadhi ya maeneo yataleta changamoto kwenye sheria zetu kwa kuwa hatukufundishwa, mfano eneo huru la Biashara Afrika. Kuna haja ya kutazama mambo haya ili sheria zetu zitusaidie.

Hivi yule wakili wa serikali alikuwa anaitwa MUTALEMWA KISHENYI, alikamatwaga na rushwa kule manyara,kesi yake sijaisikia Tena sijui iliishia wapi
 
Mimi nikafikiri ingalau amekwenda Serengeti - Mara kushughulikia mauji yaliyofanywa na polisi wake na kuliambia taifa hatua alizochukua...

Masikini huyu mama pengine hata hajui. Yeye anaponda raha tu kwa sherehe za pilau na nyama huku damu za watu wasio na hatia zikimlilia Mungu Baba toka ardhini zikidai HAKI na KISASI..

Rais Samia obviously anadhani uongozi na u - Rais ni kuponda raha na kuswampa huku na kule. She is absolutely wrong..!

Hajui kuwa U - Rais wake it's about people's lives.

By the time atakapong'amua ukweli huu, it would be too late kurekebisha mambo bali itakuwa ni wakati wa HUKUMU YAKE physically & spiritually yeye na wenzake... NIMESEMA MIMI...!!

Acha waponde raha...
 
Samia Suhuhu Hassan - Rais

Kuanzia sasa hakuna kuingia mikataba pasipo kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hii itasaidia kupungua changamoto na migogoro na wawekezaji kwa kuwa mikataba mingine husainiwa kienyeji.
Hilo litakuwa na maana ikiwa tu kuanzia sasa nyie maraisi mtakuwa mnateua Mwanasheria Mkuu ambae anajitambua na anafanya kazi kwa maslahi ya Tanzania badala ya kumfurahisha aliemteua. Sio kuteua watu yeboyebo kwa sababu tu za kisiasa na ubinafsi
 
Mimi nikafikiri ingalau amekwenda Serengeti - Mara kushughulikia mauji yaliyofanywa na polisi wake na kuliambia taifa hatua alizochukua...

Masikini huyu mama pengine hata hajui. Yeye anaponda raha tu kwa sherehe za pilau na nyama huku damu za watu wasio na hatia zikimlilia Mungu Baba toka ardhini zikidai HAKI na KISASI..

Rais Samia obviously anadhani uongozi na u - Rais ni kuponda raha na kuswampa huku na kule. She is absolutely wrong..!

Hajui kuwa U - Rais wake it's about people's lives.

By the time atakapong'amua ukweli huu, it would be too late kurekebisha mambo bali itakuwa ni wakati wa HUKUMU YAKE physically & spiritually yeye na wenzake... NIMESEMA MIMI...!!

Acha waponde raha...
Mojawapo ya vitu vilivyochangia JPM aage dunia kwa ugonjwa wa moyo ni kujitwisha mizigo yote ya serikali ili aonekane mzalendo na mwema kwa wananchi wake.

Rais anapoteua watu huwapa madarakani kamili kama wasaidizi wake. Hivyo uimara wa kitaasisi humsaidia kazi rais.

Rais ni bosi wa serikali lakini hana uwezo wa kufanya kila kazi. Waziri wa mambo ya ndani, IGP na jeshi lake la polisi ndio wawajibikaji wa kwanza kabisa katika suala la serengeti.
 
Hao waliouawa ni majambazi...
 
Sawa, I agree...

Lakini inapolazimika kuwajibika yeye, basi sharti afanye vile especially aliowapa jukumu hilo wanaposhindwa kutenda wajibu wao au wanapotenda kinyume kwa makusudi au kwa kutojua...

Serengeti situation vidole vinamwelekea yeye haijalishi ana aliowateua kufanya jukumu lake ama la...
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili leo tarehe 29 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Prof. Ibrahim Juma - Jaji Mkuu
Haitoshi kuwa na sheria nzuri ambayo haitimizi malengo ya kutungwa kwake. Zipo sheria ambazo ni vikwazo kwa maendeleo mfano ni ile ya manunuzi.

Sheria zingine za zamani, zina maudhui ya karne ya 19 au 20. Tunahitaji kuziangalia upya.

Hata kwenye ku draft sheria bado tunatumia makaratasi wakati wenzetu wanatumia computer.

Baadhi ya maeneo yataleta changamoto kwenye sheria zetu kwa kuwa hatukufundishwa, mfano eneo huru la Biashara Afrika. Kuna haja ya kutazama mambo haya ili sheria zetu zitusaidie.

Samia Suhuhu Hassan - Rais
Natumaini maboresho yanayofanywa kwenye sekta ya Sheria yataleta tija kubwa kwa taifa hili.

Nawasihi mawakili wote wa Serikali wajisajili, pia napongeza kwa kuanzishwa kwa chama hiki cha Mawakili. Mmepata mlezi mzuri (Mwanasheria mkuu), atawanoa na kuwalea vizuri.

Nawapongeza kwa kuanzisha mfumo (mtandao) wa mawasiliano unaolenga kuboresha kazi zenu. Umetengenezwa na vijana wazalendo, nawapongeza.

Wananchi wetu wengi wana shida nyingi na hawana watu wa kuwasilikiza, mnayo dhamana kubwa ya kuwasikiliza na kuwapa suluhisho. Nendeni mkawasaidie.

Mawakili waitwe mara kwa mara kukumbushwa wajibu wao, wengine wakienda huko wilayani wanajisahau. Pia wafuatiliwe kutathimini utekelezaji wa kazi zao.

Serikali itaendelea kutenga bajeti ya maendeleo kwa sekta ya sheria nchini ili kusogeza huduma bora kwa wananchi.

Tumefungua nchi kwa kiasi kikubwa, wawekezaji wanaingia nchini kwa kasi kubwa. Migogoro inaweza kuanza kutokea, ili tuendelee na uwekezaji mzuri lazima mawakili wa serikali muwe makini kuharakisha kusikiliza migogoro hii kabla haijafika mahakamani.

Lindeni uchumi wetu kwa hali na weledi, nendeni mfanye kazi.

Kuanzia sasa hakuna kuingia mikataba pasipo kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hii itasaidia kupungua changamoto na migogoro na wawekezaji kwa kuwa mikataba mingine husainiwa kienyeji.

Simamieni haki, Mungu anapokuteua usimamie sekta hii anataka uwe muadilifu. Kasimamieni haki.

Tatizo la kusweka watu mahabusu litapungua ikiwa kesi zitasikilizwa mapema kabla hazijaenda mahakamani. Kuweni waadilifu na wenye uaminifu.

Changamoto hizi zifanyiwe kazi haraka. Nitaitisha kikao tuje tujadili, mtoe presentation, tugawane majukumu na kila mtu apewe jukumu la kwenda kufanya.

nadhani hapa mama anampigia mbuzi ngoma ambayo hajui kuicheza.kama mfumo wa mahakama zetu wote uko corrupt je hao mawakili wamesalimika?tunahitaji transformation kubwa ktk mfumo wetu wa mahakama na watendaji wake wote pamoja na hao mawakili.kuna kesi za miaka hadi ishirini hata hazitolewa maamuzi mpaka leo tatizo rushwa leo hii hao watendaji ambao wamepatikana kwa mfumo huo watakuwa na weledi?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili leo tarehe 29 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Prof. Ibrahim Juma - Jaji Mkuu
Haitoshi kuwa na sheria nzuri ambayo haitimizi malengo ya kutungwa kwake. Zipo sheria ambazo ni vikwazo kwa maendeleo mfano ni ile ya manunuzi.

Sheria zingine za zamani, zina maudhui ya karne ya 19 au 20. Tunahitaji kuziangalia upya.

Hata kwenye ku draft sheria bado tunatumia makaratasi wakati wenzetu wanatumia computer.

Baadhi ya maeneo yataleta changamoto kwenye sheria zetu kwa kuwa hatukufundishwa, mfano eneo huru la Biashara Afrika. Kuna haja ya kutazama mambo haya ili sheria zetu zitusaidie.

Samia Suhuhu Hassan - Rais
Natumaini maboresho yanayofanywa kwenye sekta ya Sheria yataleta tija kubwa kwa taifa hili.

Nawasihi mawakili wote wa Serikali wajisajili, pia napongeza kwa kuanzishwa kwa chama hiki cha Mawakili. Mmepata mlezi mzuri (Mwanasheria mkuu), atawanoa na kuwalea vizuri.

Nawapongeza kwa kuanzisha mfumo (mtandao) wa mawasiliano unaolenga kuboresha kazi zenu. Umetengenezwa na vijana wazalendo, nawapongeza.

Wananchi wetu wengi wana shida nyingi na hawana watu wa kuwasilikiza, mnayo dhamana kubwa ya kuwasikiliza na kuwapa suluhisho. Nendeni mkawasaidie.

Mawakili waitwe mara kwa mara kukumbushwa wajibu wao, wengine wakienda huko wilayani wanajisahau. Pia wafuatiliwe kutathimini utekelezaji wa kazi zao.

Serikali itaendelea kutenga bajeti ya maendeleo kwa sekta ya sheria nchini ili kusogeza huduma bora kwa wananchi.

Tumefungua nchi kwa kiasi kikubwa, wawekezaji wanaingia nchini kwa kasi kubwa. Migogoro inaweza kuanza kutokea, ili tuendelee na uwekezaji mzuri lazima mawakili wa serikali muwe makini kuharakisha kusikiliza migogoro hii kabla haijafika mahakamani.

Lindeni uchumi wetu kwa hali na weledi, nendeni mfanye kazi.

Kuanzia sasa hakuna kuingia mikataba pasipo kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hii itasaidia kupungua changamoto na migogoro na wawekezaji kwa kuwa mikataba mingine husainiwa kienyeji.

Simamieni haki, Mungu anapokuteua usimamie sekta hii anataka uwe muadilifu. Kasimamieni haki.

Tatizo la kusweka watu mahabusu litapungua ikiwa kesi zitasikilizwa mapema kabla hazijaenda mahakamani. Kuweni waadilifu na wenye uaminifu.

Changamoto hizi zifanyiwe kazi haraka. Nitaitisha kikao tuje tujadili, mtoe presentation, tugawane majukumu na kila mtu apewe jukumu la kwenda kufanya.

Hii habari ina mkanganyiko. Hiki kitakuwa Chama cha Mawakili wa Serikali maana tayari TLS ipo. Hilo lilitakiwa liwekwe wazi. Au nia ni kuizika TLS ili watu wapeleke kesi za nyani kwa ngedere kwa kutegemea mawakili wa hiki chama wawatetee hata pale mshitakiwa ni Serikali?
 
Mimi nikafikiri ingalau amekwenda Serengeti - Mara kushughulikia mauji yaliyofanywa na polisi wake na kuliambia taifa hatua alizochukua...

Masikini huyu mama pengine hata hajui. Yeye anaponda raha tu kwa sherehe za pilau na nyama huku damu za watu wasio na hatia zikimlilia Mungu Baba toka ardhini zikidai HAKI na KISASI..

Rais Samia obviously anadhani uongozi na u - Rais ni kuponda raha na kuswampa huku na kule. She is absolutely wrong..!

Hajui kuwa U - Rais wake it's about people's lives.

By the time atakapong'amua ukweli huu, it would be too late kurekebisha mambo bali itakuwa ni wakati wa HUKUMU YAKE physically & spiritually yeye na wenzake... NIMESEMA MIMI...!!

Acha waponde raha...
aliponda raha wapi?
tuache nongwa
 
Huyo mwanasheria wa serikali anaweza kuachwa afanye kazi zake kwa uhuru? au bado ataendelea kuwa mikononi mwa viongozi wa CCM?

Nina wasiwasi kama huovile ushauri utakuwa na manufaa kwa taifa kwasababu huyo mwanasheria nae amezungukwa na watu walewale wenye mawazo ya kulinyonya taifa.
 
Back
Top Bottom