GE2025 Rais Samia: Hakutakuwa Na Vurugu Siku Ya Uchaguzi, Mimi Ndiyo Amiri Jeshi Mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Siyo wote tunatumia VPN.
Lakini Jamii Forums imefungiwa na TCRA, wewe unafanya nini huku? Kama unaipenda sana hii serikali kwa nini usifuate amri zao? Usitumie Jamii Forums, mama yako ndio anataka hivyo
 
Ni sahihi yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Wananchi ni nje ya majeshi. Maaskari wanapoteka, kutesa na kuua wana baraka zake pia.

Wananchi ni zaidi ya majeshi na Amiri wao
 
Nami lazima nitoke tarehe 29 lazima kama kufa nife sio kwa maisha haya. Kwani kupigwa wamepigwa wangapi wewe mwenyewe unapigwa ila hujui 29 natoka kama kupigwa nipigwe tu
Jaribu uone moto wake.
 
Nilijiandikisha Dar ila kwa Sasa nipo Bukoba hivi nitaweza kupiga kura zote au ya urais tu? Au hata ya urais Kuna vipengele lazima vifanyike?
 
Nilijiandikisha Dar ila kwa Sasa nipo Bukoba hivi nitaweza kupiga kura zote au ya urais tu? Au hata ya urais Kuna vipengele lazima vifanyike?
Usijali utapiga kura yako . Kuna utaratibu utawekwa wa kukupatia haki ya kupiga kura hata kama upo Sehemu nyingine nje ya ile ambayo kujiandikisha
 
Ni sahihi yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Wananchi ni nje ya majeshi. Maaskari wanapoteka, kutesa na kuua wana baraka zake pia.

Wananchi ni zaidi ya majeshi na Amiri wao
Mbona wewe hujatekwa wala kuuwawa
 
Anajisahau sana au hafahamu katiba au katiba hii ni mbovu. Yeye anakuaje amiri jeshi wakati ni mgombea na wala sio rais.
 
Anajisahau sana au hafahamu katiba au katiba hii ni mbovu. Yeye anakuaje amiri jeshi wakati ni mgombea na wala sio rais.
Kwa hiyo unafikiria kwamba kwa sasa anayeongoza serikali ni nani? Au unafikiri kuwa serikali haipo?
 
Acheni kunifurahisha. Yaani mnafungia mitandao na bado mnataka tukawape tena nafasi nyingine ya kutukandamiza? Kweli hamjielewi nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…