ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Naunga mkono hoja.
Mambo ya kulazimisha watu kwenye vikundi ni upuuzi,Wala myhamimishe mtu mmja mmja na wazamini wake Ili pesa imwagike watu wapige kazi.
============
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wasimamizi wa mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 kurahisisha masharti ya mikopo hiyo ili kuwasaidia zaidi wenye mahitaji ikiwamo kuwasaidia kujaza fomu kwa usahihi ili mikopo ipatikane kwa urahisi.
“Naomba sana msimamie urejeshwaji wa mikopo hii ili vijana hawa waweze kupata mikopo, lakini hata wakati wa utoaji wa mikopo yenyewe legezeni masharti, kuna watu wanahitaji mikopo hii, yale mafomu mliyowawekea wanashindwa kuyajaza vilivyo na mnapofanya tathmini mnasema hawa hawakujaza vizuri wasipewe lakini kumbe ndiyo wenye haja ya hizo pesa,” amesema Samia.
Rais Samia ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu leo Jumatano Juni 18, 2025, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.