Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Katika uchaguzi wa hapo Mwakani ni vyema tukaendelea kukumbushana na kuelezana ukweli tu kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan jasiri muongoza njia, simba wa nyika,nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge hana Mbadala wake na hakuna mwenye uwezo wa kuvaa viatu vyake.
Ni Mwaka wa uchaguzi lakini ni uchaguzi wa Mgombea Mmoja tu Mwenye sifa na uwezo wa kuliongoza Taifa letu Mheshimiwa Daktari Mama Samia.Ni uchaguzi wa kuliweka Taifa letu katika mikono ya mtu mwenye kuleta matumaini kwa mamilioni ya watanzania,kuwahakikishia watanzania nafasi ya kutimiza ndoto zao,kuwawezesha watanzania kufikia malengo yao na kuwainua watanzania kiuchumi.
Ni uchaguzi wa kumpitisha Rais Samia kuendeleza kazi nzuri aliyoianza ya kujenga uchumi shirikishi na wenye kugusa maisha ya watu wengi.ni uchaguzi wa kwenda kumchagua kiongozi ambaye tayari ameshaonyesha uwezo na nguvu ya kuliongoza Taifa letu katika nyakati ngumu zenye kuhitaji uimara,utulivu,maono,akili kubwa na uhodari wa kiuongozi kama alivyofanya Rais wetu Mama Samia kutuvusha katika kipindi kigumu cha Corona,mfumuko wa bei hasa mafuta ya petroli,dizeli na mbolea kuliko tokana na vita vya ukrein.
Ni uchaguzi wa kumchagua mtu ambaye haendi kujifunza kazi,au kujifunza mpangilio wa vyumba vya ikulu au ofisi zilizo chini ya ofisi ya Rais au kuanza kuunda taasisi mpya.tunakwenda kumpigia kura Rais Samia kwa kuwa tayari tumeona umahiri wake katika kuendesha ofisi ya Rais kwa manufaa na ustawi wa Taifa letu na watanzania wote kwa ujumla wake.
Ndio sababu ninasema ya kuwa RAIS Samia hana Mbadala wake wa kuweza kuvaa viatu vyake.Bali ni fursa ya viongozi wengine kuendelea kujifunza mambo mengi ya kiuongozi kutoka kwa Mama huyu ambaye ni kama maktaba ya uongozi. Ni fursa na nafasi ya wengine kukua na kukomaa kiuongozi kupitia mikono yake..
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.