Mtondoli
Member
- Nov 9, 2021
- 70
- 174
Ndugu zangu rais huyu ukimtazama vizuri kuanzia speech zake na action anazozichukua utagundua kuwa Hana nongwa na mtu, Ila Kuna watu wananongwa na rais.alianza vizuri Sana na hajabadilika ni Yule Yule na Nia yake ni ileile.ya kuwaunganisha watanzania.kutibu majeraha yaliyotokana na mbinyo wa demokrasia na kujaribu kutaka kuifungua Tena demokrasia yetu.hulka ile ile ya viongozi wetu wa kisiasa hawakutaka kumpa muda hata wa miezi miwili ayaweke sawa mafaili yake ajue pakuanzia .ameingia tu hata msiba haujaisha wakaanza vurugu za kudai katiba ,na kuanza kukimbizana huku na kule kuandaa sijui makongamano ya katiba kuandaa mikutano ya hadhara wakati huo bado hata arobaini ya magufuli haijafika ,nchi bado inatafakari na ipo kwenye majonzi wao na mbowe wao wakaanzisha harakati na kelele huku na kule,hata Kama Nia ya rais ilikuwa njema nyinyi mmechangia kuiharibu .tunawaambia Kila siku Kuna vitu havihitaji nguvu nyingi kuvipata ni akili kidogo tu.nina hakika kupitia Samia suluhu hassan katiba mpya itapatikana na tume huru ya uchaguzi itapatikana .lakini mkiendekeza mipasho ,vijembe ,matusi,na ghiliba za kufanya makosa na kuyatumia makosa hayo kwamba ni udhaifu wa rais haikubaliki.sisi tutulie tukiwa na letu tulizungumze kwa kutumia meza ya mazungumzo huku tukiheshimu mamlaka ,narudia Tena Samia suluhu hassan ndiye haswaa taifa lilikuwa linamhitaji ,ni mtu wa aina yake