Rais Samia hapa ulikosea kidogo na sijui ni nani alikujaza Upepo na ukalisema hili

Daah kazi ipo haya mambo ukiyasikia yanaumiza wacha tukae kimya tuendelee kupata maumivu na shilingi inavyoporomoka itafika mbali sana kuipata Usd moja..
Tunatangaza utalii kwa gharama kubwa na tunategemea wageni watoke huko harafu tunatoa kauli ambazo ni Tata kwao kazi tunayo aisee..
 
Nadhani Kiongozi anasalimisha matakwa yake ndani ya Matakwa ya umma ndio Katiba. Mambo mengi binafsi anaweza kuamini lakini yakashindwa na nguvu ya Matakwa ya umma.
 
Ukimsoma vizuri huyu mama Urais anaupenda sana.

Haya yote ni slogan ya Samia must go.

Watanzania bila katiba ya wananchi ni kazi bure kabisa.

Halafu cha kusikitisha ni Watanganyika ndio madalali wa huyu Mkojani ambaye sasa hivi anatukomesha, zikitoka ajira ni pasu kwa pasu, ila zikitoka Zanzibar sifa lazima uwe Mzanzibar.

Tembelea TRA sasa hivi utaamini maneno yangu wamejazwa vijana Kizanzibar.

Issue ilivyo ni zaidi ya siasa za ccm na Chadema, ni revenge ya Wazanzibar kupitia kwa Samia lazima Zanzibar kwa miaka michache ijayo, kaka anampigia dada simu, dada anarekebisha, Mitanganyika inachonganishwa yenyewe iuwane.

Mitanganyika haijiulizi mbona Wazanzibar sasa hivi wanaishi pamoja peaceful?
 
Hata filamu ya kuhamasisha watalii kuja kuitembelea nchi hii alienda kuigiza huko huko kwa hawa watu anaowasema vibaya. Watanzania wenzangu tuzinduke, nchi unakwenda mrama, hawa Watu sisi tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyotuhitaji sisi.
Ukweli mchungu ni kwamba, Tanzania kamwe haiwezi kusonga mbele kimaendeleo bila ya misaada kutoka kwa mabeberu,
 
Hivi watu wote sisi 71 tulio like hii post ya GENTAMYCINE tutatekwa tuuwawe?
 
Inajitegemea kwa utajiri upi..?
 
Nadhani Kiongozi anasalimisha matakwa yake ndani ya Matakwa ya umma ndio Katiba. Mambo mengi binafsi anaweza kuamini lakini yakashindwa na nguvu ya Matakwa ya umma.
uko sahihi sana Mkuu,

Lakini nadhani moja ya jambo alilolisema na ambalo limekuwa mada kwenye uzi huu ni yeye kusema vile alivyosema kuhusu maagizo ya baadhi ya mabalozi. Kimsingi katiba yetu imesema sisi ni nchi huru, Rais amekuwa mkali kwelikweli juu ya baadhi ya mabalozi kufikiri wanaweza kutuelekeza cha kufanya kama nchi. Imani hii akiisema kwa wananchi wengi wa chini inampa 'edge'. Watu walitamani wasikie Rais anayejiamini against mabeberu na it came at a right time. Ieleweke Rais hakatai wao kulaani "bali kuelekeza nini cha kufanya" na pengine wamefanya in public na in private pia (hili hatujui wamesema nini).

Sasa swali langu kwa baadhi ya wakosoaji wake, kama kauli tu hii ya Rais tena kuhusu mabeberu wao wanapata 'hofu' na uoga unadhani itakuwa ni rahisi wao kuingia barabarani?
 
Kila nikikumbuka ile kauli kuwa mgombea wa CCM 2025 ni Samia labda hapa katikati mambo yaharibike sana naona kabisa mambo yameshaharibika sana na yataharibika sana, na pia ile kauli yake mwenyewe kuwa aliwahi kuonywa kuwa adui yako siyo wapinzani bali ni wa shati la kijani mwenzako ni dhahiri ajali ya kisiasa imeshaandaliwa.
 
Kauli yako kuwa Balozi za Kigeni ambazo zilikemea na kutaka Uchunguzi wa Kifo cha Mzee Kibao (ukiilenga hasa Marekani) kuwa zilifanya hivyo bila ya Baraka za Marais wao umeikosea mno Kuisema.
mama anataka watu kukaa kimya wakati watu wanazidi kupotea na kuuawa hadharani?
Kwanini yeye hakuwahi kukemea haya mapema na badala yake anakemea wanaokemea?
Au anafikiri watawala wanayo mamlaka ya kupoteza na kuumiza watu watakavyo?
Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo yupo usiku na mchana
 
Amina / Amen Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…