Rais Samia hapaswi kuitwa Daktari

Rais Samia hapaswi kuitwa Daktari

Kuna gia ya angani ilipigwa hapa katikati, shwaaaaaa tukashtukia mtu anaitwa Daktari.

Kutoka form four mpaka kuwa Daktari ni gia kubwa. Hii ni gia ya SCANIA, unapiga mpaka msuli wa kiwiko unavimba.

Utaratibu wa Doctorates ni kwamba, mtu anayetakiwa kuitwa Daktari ni yule tu ambaye aliusomea huo Udaktari darasani (PhD), mfano Dr. Magufuli au Dr. Tulia.

Mtu aliyetunukiwa Udaktari wa heshima hapaswi kabisa kuitwa au kujiita Daktari. Udaktari wake unabaki kuwa wa heshima na sio Udaktari wa Title. Hizi ni kanuni za utoaji wa Doctorates.

Samia hapaswi kuitwa Dr. SAMIA kwa sababu hakusomea Udaktari (PhD). Alitunukiwa tu.

Hili swala lazima litangazwe watu waelewe ili kuepusha matapeli.

Tutakuja kupigishwa gia za mwendokasi mpaka tuombe poo. Dr. Manyaunyau, Dr. Masantula.

Elimu izingatiwe!
Wivu ni kitu kibaya sana! hivi mtu ambaye tayari ana'occupy the highest office on land unadhani udaktari wa heshima unamuongezea chochote katika katika na mambo yake?
 
Wivu ni kitu kibaya sana! hivi mtu ambaye tayari ana'occupy the highest office on land unadhani udaktari wa heshima unamuongezea chochote katika katika na mambo yake?
Udaktari unamuongezea sana maujiko ndo mana kila siku anatunukiwa udaktari wa maigizo.
 
True, naunga mkono hoja, PhD za Honoria Causa, sio official title ya kuitwa Dr, ila kwenye social gatherings na kwenye events ni sawa kumu address as Dr. na ndio maana kwenye press release za ikulu, huwezi kuona Rais Samia akiandikwa Dr.

Hili niliwahi kushauri Kuongezeka Ph.D za Heshima: Kuna haja TCU watoe ufafanuzi wa matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima na Ph.D za ukweli?
P
Baada ya kusoma andiko lako imenibidi nipitie taarifa nyingi za Mawasiliano Ikulu na kugundua uko sahihi. Wamekuwa wakikwepa kumuadress kwa maandishi kama Dr. Samia bali kama mhe Samia Suluhu Rais ....
Matatizo yako kwa CCM na viongozi wake, huko kila wakimuaddress lazima waandike Dr tena kwa fahari kubwa sana na ni kama hawataki wengine (wanaostahili) waitwe hivyo bali wamilikishe title hiyo kwa mwenyekiti wao tuu.
Ndani ya CCM kuna kaushamba kameota mizizi na imejikita haswa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Magufuli we ulisoma naye PhD? We bwege kweli, unajua kilichomwua Ben Saanane? Bora Samia anatunukiwa na vyuo vinavyotambulika, tena hadharani bila kificho. Tuambie huyo mfu wako alitunukiwa lini, we ulihudhuria akitunukiwa? Samia ana masters kutoka mojawapo ya chuo kikuu bora duniani "Manchester University" umesikia we bwege? Anayetoa degree yoyote ni chuo baada ya kuona umekamilisha vigezo. Hiyo chuki na wivu havitakuacha salama
Mkuu Punguza Stress..
Magufuli alikuwa na Ph.D. in Chemistry kutoka University of Dar es Salaam na wala hakupata Honorary PhD
na alimaliza doctoral studies mwaka 2009.
 
Hili ni tatizo la upinzani kukosa agenda. Kushika dola labda iwe mwaka 2300 kama hizi ndo agenda mlizo nazo. Wananchi hawawezi kuwa na imani na upinzani unaopoteza muda kuongelea elimu na hadhi ya Rais badala ya kuongelea mambo yanayowagusa kila siku.
 
Ni ujinga kupigana na majina yake sababu hata akifutiwa huo udr bado ni samia yule yule anayetuongoza. Yaaani shubiri kwa walamba shubiri na asali kwa walamba asali haibadilishwi kwa kumfutia au kumpachika udr.

Sio ujinga, tutofautishe Doctor of Letters na Doctor of Phylosopht PhD.
 
Hili ni tatizo la upinzani kukosa agenda. Kushika dola labda iwe mwaka 2300 kama hizi ndo agenda mlizo nazo. Wananchi hawawezi kuwa na imani na upinzani unaopoteza muda kuongelea elimu na hadhi ya Rais badala ya kuongelea mambo yanayowagusa kila siku.

Ni mpinzani gani ameongelea PhD ya kupewa ya Rais?. Tatizo Jambo lolote ambalo lipo kinyume na CCM mnaita ni wapinzani.
 
Kuna hatari kubwa sana kwako ya kukumbwa na yaliyomkumba Ben Saanane.
Kumbuka; aliyekufa ni Mwendazake peke yake, wale watu wote aliokuwa akiwatumia kwenye missions zake za kuteka watu, kuwekea watu sumu, kutesa watu au hata kuwaua kikatili na kisha kutupa maiti zao zikiwa kwenye viroba, wote bado wapo hai. Na mbaya zaidi sasa hivi wamejitungia Sheria yao ili wasiweze kushitakiwa Mahakani kuhusiana na makosa yao yote ya jinai ambayo watatenda. Be Very Careful my dear, "Noah Nyeusi" hazitakauka nyumbani kwako na kazini kwako.
Noted
 
Yeye mwenyewe kakiri PhD ilimshinda halafu Leo wanampa cheo Cha udokta.
 
Kuna gia ya angani ilipigwa hapa katikati, shwaaaaaa tukashtukia mtu anaitwa Daktari.

Kutoka form four mpaka kuwa Daktari ni gia kubwa. Hii ni gia ya SCANIA, unapiga mpaka msuli wa kiwiko unavimba.

Utaratibu wa Doctorates ni kwamba, mtu anayetakiwa kuitwa Daktari ni yule tu ambaye aliusomea huo Udaktari darasani (PhD), mfano Dr. Magufuli au Dr. Tulia.

Mtu aliyetunukiwa Udaktari wa heshima hapaswi kabisa kuitwa au kujiita Daktari. Udaktari wake unabaki kuwa wa heshima na sio Udaktari wa Title. Hizi ni kanuni za utoaji wa Doctorates.

Samia hapaswi kuitwa Dr. SAMIA kwa sababu hakusomea Udaktari (PhD). Alitunukiwa tu.

Hili swala lazima litangazwe watu waelewe ili kuepusha matapeli.

Tutakuja kupigishwa gia za mwendokasi mpaka tuombe poo. Dr. Manyaunyau, Dr. Masantula.

Elimu izingatiwe!

Nani alikwambia mama Samia anaitwa Daktari?
 
Wivu ni kitu kibaya sana! hivi mtu ambaye tayari ana'occupy the highest office on land unadhani udaktari wa heshima unamuongezea chochote katika katika na mambo yake?

Wewe ndio una wivu. Abood na utajiri wake amehangaika mpaka kununua udokta, msukuma naye kanunua udokta nk. Kuna Raha yake kuitwa Dr acha tu. Usichukulie kawaida.
 
Watotowangu wakwanza nimemwita jina Dokta Ramazani, wapili Profesa Ramazani,watatu Injinia Ramazani wanne nataka nimwite Wakilimsomi Ramazani hamna wa kunizuia
 
Daktari mwenye vyeti vya kuunga unga daktari hata ishu ndogo ya mafuta na umeme vimemshinda labda dokta wa kienyeji.....By the way ndo mama yenu huyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nchi hii bhana! Mwanasiasa mwenye vyeti vingi, vizuri na vya moja kwa moja ni Profesa Sospeter Muhongo, mwenyewe aliwahi kusema kama atatakiwa kuviwasilisha itabidi atafute pick up lakini bado mlimzingua!
 
Back
Top Bottom