Rais Samia, hata siku moja mwekezaji habembelezwi kuja kuwekeza nchini, tafadhali zingatia yafuatayo watakuja wenyewe

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o! Uwe unajiuliza, nini kitamfanya mwekezaji aje Tanzania badala ya kwenda nchi nyingine? Namna gani tunaifanya Tanzania kuwa na comparative advantage katika kuvutia wawekezaji? Kumbuka chema chajiuza, kibaya chajitembeza!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza (local na Tanzania as an exporter to regional markets)
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (policy transparency) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations for repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits hapa Tanania? Kwa nini hili halijaangaliwa? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency permit kwa wawekezaji hata wale wakubwa na waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permits.

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na kukutana na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usiseme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na balance dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
 
Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (transparent) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations of repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency kwa wawekezaji hata wale wakubwa hata waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permit

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usieme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na control dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
Ushauri mfupi na wa bure lakini una thamani kubwa mno. Hizi ndiyo juhudi ambazo Tanzania ilianza kufanya tulipoamua kuachana na ujamaa lakini hivi sasa hizo juhudi zimepoteza dira. Hongera sana mwandishi.
 
Tuna matatizo mengi sana yaliyo wazi ambayo ni rahisi sana mwekezaji kuya ng'amua jambo ambalo umuwia ugumu sana yeye kuja hapa nchini.
 
Unampangia? Mama kanyaga twende tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 7.
 
Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o! Kumbuka chema chajiuza, kibaya chajitembeza!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (transparent) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations of repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency kwa wawekezaji hata wale wakubwa hata waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permit

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usieme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na control dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
Nakumbuka mwaka 2015 baada ya songombingo za uchaguzi zanzibar tukakosa grant kusubiri utulivu... Baadae wakaamua kuelekeza hizo grant sehem ingine... Kilichobakia ni historia adi leo

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom