Rais Samia, hata siku moja mwekezaji habembelezwi kuja kuwekeza nchini, tafadhali zingatia yafuatayo watakuja wenyewe

Mama sijui alisomea nini na sijui ni kipi anakielewa zaidi ili aweze kukifanyia jazi mwenyewe.

Ila iwapo anatumia. Vichwa vya wengine kufanyia kazi bila yeye kuvijua au kufanya utafiti , timu yake ya 2030 inawadanganya CCM na wananchi kwa ujumla.
 
Aache uendawazimu,nani wa kuwekeza kwenye nchi ya majenereta

Au waje watengeneze viwanda vya majenereta
Hilo nalo jambo, kiwanda cha majenerator.

Tanzania ni nchi ambayo ukijenga kiwanda cha kutengeneza majenerator, bei yake itabidi iwe juu kuliko yale yanayoingizwa nchini na ukiuza kwa bei ya chini itabidi ufunge kiwanda. Kuna vitu vya ajabu sana kwenye nchi hii
 
Viongozi wa serikali wanafikiri wawekezaji wanatoa hisani, wale ni wafanyabiashara wanaangalia fursa. Pia Wana taarifa nyingi za nchi yetu kuliko zile tunazowapa.
Kwa sababu wanawekeza pesa zao lazima waangalie na mazingira yetu, ni kichekesho Kwa nchi yenye vyanzo vingi vya nishati kuangaika na mgao wa umeme au maji . Siasa inapoingiliana na utaalamu ni tatizo au pale mkuu wa wilaya, mkoa au polisi anapoingilia kazi ya tra.
Kama serikali ikitengeneza mazingira mazuri wawekezaji watakuja wenyewe hawatasubiri kuitwa.
 
Unahitaji ulinzi wewe..
Very productive thread kwa wenye mamlaka
 
Pull and Push factors
 
Ujasusi wa kidola na kiuchumi. Kwenda kuwapigia ngoma huku wakijua kila kitu nyumbani kwako ni bure.

Sana sana utaambulia kuona maghorofa mazuri ughaibun
 
Ubarikiwe Mkuu.


Nashangaa Kuna lijamaa limoja la CCM humu, Kila siku linaandika machapisho ya kumsifia Samia.


Badala ya Kuandika vitu kama hivi
Linaitwa li - Lucas mwashambwa...

Yaani ili mradi yenyewe yamekula na kushiba ndiii matumbo yao, basi they never care and think about others...!

All in all, umemwaga madini ya dhahabu safi yenye thamani ya juu sana. Wenye akili huko serikalini wakikusoma, wataelewa na watajirekebisha ktk utendaji wao..
 
Umemaliza kila kitu Cha msingi tunaita investment enablers for any particular state, FDI sio Siri indicators on investment and easness in doing business, local capital investments, ukwasi wa mabenki nk, Sheria zetu na Mahakama za ndani. Umetisha sana
 
Kwenye knowledge pyramid you have synthesized ur analysis 🙏
 
Sasa mtu katoka kwenye jamii watu wapo 1.8M. Ally Kessy alisema ukipiga filimbi wote wanatoka.
 

Ulisahau matatizo ya Uvamizi uliopewa jina la muungano, namna gani unakwamisha kuja wawekezaji na watalii nchini
 
Ni HAKIKA na KWELI tupu..

Ni jambo la kushangaza kuwa, Rais wa nchi anatembea huko duniani kutafuta wawekezaji wakati serikali yake huyu Rais imeshindwa hata kuwa na assurance ya huduma bora na ya uhakika ya MAJI na UMEME...!

Yaani Rais anaalika foreign investors huku akiwa hajui kuwa nchi yake iko gizani (haina umeme wa uhakika) na ina kiu cha maji (haina huduma ya maji) achilia mbali hayo mengine ya utulivu wa kisiasa, nafuu ya urasimu wa utoaji huduma nk nk..

Bila shaka huyu kiongozi (Rais) afanyaye hayo kabla kwanza hajaweka mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji wa ndani na wa nje, obviously atakuwa ni mwendawazimu na hajitambui...

Hatumtukani Rais wetu. Lakini kama anafanya matendo yafanywayo na mwendawazimu bila shaka na yeye atakuwa ni mwendawazimu tu bila kujali status yake...!
 
Ndioo Hilo Lilukas , ni lipuuuzi kwelikweli
 
JF bado kuna vichwa hasa kongole mleta uzi umepita kwenye nyanja zote muhimu mbaya zaidi ni kuwa viongozi wetu hujifanya kujua kila kitu mwisho ujinga wao huwa wazi kabisa sio open minded

Binafsi huwa naona safari za Dr Samia sijui kwenda ughaibuni kutafuta wawekezaji huwa naona kama ni kupoteza muda na matumizi yasiyo ya lazima ya Kodi zetu kwa mazingira ya Tanzania hakuna mwekezaji mwenye akili timamu atakuja kuwekeza Tanzania hizi ni day dream.

"Mganga wa kienyeji huwa aendi sokoni"
 
Uwekezaji ni fursa kubwa na bahati kupatikana na hivyo ni kweli tupu mwekezaji hapaswi kubembelezwa, ukiona anabembelezwa huwa inamaanisha anapokwenda kuwekeza kuna changamoto nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…