Rais Samia, hata siku moja mwekezaji habembelezwi kuja kuwekeza nchini, tafadhali zingatia yafuatayo watakuja wenyewe

Wakati wawekezaji wanapokuja hapa, unashindwa kujadiliana nao na kuelewana jinsi utakavyonufaika na uwekezaji wao, unawaachia mianya ya kukugonga katika mikataba, halafu wewe unachekelea umepata uwekezaji!
Ikiwa una wawekezaji wale wa kubembeleza waje nchini, ndio unajiwekea mazingira ya kugongwa kwenye mikataba, maana kila kipengele wanakuambia sisi hicho hatutaki, na ukikiweka tunaondoka, na wewe unajichekesha na kusema sawa basi nitakiondoa
 
Hoja makini..ila shida ni huu upuuzi wa kijani..hao wahuni wanachoangalia ni maslahi yao tu.

#MaendeleoHayanaChama
Ndio maana tunasema upinzani wa siasa nchini ulio makini una faida kwa nchi. Siku CCM wakielewa hilo labda itasaidia

Katika upinzani makini huwezi kusema mikataba ya uwekezaji ni siri.
 
Mkuu, nadhani sasa nimeelewa ni wapi tunaposhindwa kuelewana.
Mimi sizungumzii Dangote wa kiTanzania awepo leo hii.
Hii ni process ya muda mrefu ya kwajenga Angote wetu.

Sikumbuki, au sijasikia tu, toka Samia aingie akitamka neno SIDO, wewe umewahi kumsikia?
Umewahi kumsikia akizungumzia sera za serikali yake zinazolenga juhudi hizo?
Ila kila siku nasikia habari za "matrilioni ya wawekezaji' yanayosemekana kayapata kila anapokwenda kwenye ziara zake huko nje.

Acha nisiwe ninaandika mengi humu kwenye mada muhimu kama hii.
 
Ikiwa una wawekezaji wale wa kubembeleza waje nchini, ndio unajiwekea mazingira ya kugongwa kwenye mikataba, maana kila kipengele wanakuambia sisi hicho hatutaki, na ukikiweka tunaondoka, na wewe unajichekesha na kusema sawa basi nitakiondoa
hapa tumeelewana barabara. Ahsante sana.
 
Sawa kabisa, kumbe tuko wote. Acha Dangote wa nche atutengenezee Dangote wa ndani, na kwa sasa tumtengenezee mazingira mazuri Dangote wa nje ili tuje tuwe na Dangote wa ndani.
 
Nakumbk hata aliyekuw MP wa Arusha mjini mhe Lema aliwah sema ushabiki ktk mambo ya msingi ndio kikwazo cha maendeleo nchini,. Yaani tunashindana kama timu za mpira
Unajua huwa naangalia timu za mpira, yaani utakuta mchezaji wa timu moja kama aliokota mprira uliotoka akidhani wao ndio wanarusha, akaambiwa na refa ni timu pinzani wanatakiwa kurusha, unajua huwa hamkabidhi mchezaji wa timu pinzani mpira, anautupia pembeni ili akauokote mwenyewe!
 
Yote hayo yameboreshwa na ndio maana unaona wawekezaji wanapishana kila siku Tanzania uongozi wa Rais Samia Suluhu umezalimilia kukuza uwekezaji pia kupitia uwekezaji vijana wapate fursa
 
Sawa kabisa, kumbe tuko wote. Acha Dangote wa nche atutengenezee Dangote wa ndani, na kwa sasa tumtengenezee mazingira mazuri Dangote wa nje ili tuje tuwe na Dangote wa ndani.
Hapana.
Dangote hata siku moja hana nia wala sababu ya kututengenezea mshindani wake. Hili ni jukumu letu, na kuhakikisha kwamba mazingira mazuri kabisa yapo kwa Dangote wetu kupatikana.

Haya "mazingira mazuri" huoni kwamba ni ya faida kwetu wenyewe hasa, zaidi ya hao wanaotoka nje? Ndiyo yawekwe mazingira mazuri ya uwekezaji, hili linamanufaa zaidi kwetu hata zaidi ya hao wa kutoka nje. Sote tunataka umeme mzuri na chee, maji, barabara, reli, n'k..
 
Mkuu 'Synthesizer', ahsante sana kwa mada makini sana hii, nitarudi hapo baadae nikipata nafasi nikusome vizuri zaidi kama nilivyoahidi huko mwanzo.
Ninajua tunakubaliana katika mengi ndani ya mada hii.
 
Hahaha! Kweli. Usichukulie literally. Mkuu, angalia nimesema acha Dangote wa nje atutengenezee Dangote wa ndani, na kwa sasa tumtengenezee mazingira mazuri Dangote wa nje ili tuje tuwe na Dangote wa ndani.

Kwa hiyo jukumu la kutengeneza Dangote wa ndani ni letu, Dangote wa nje ana facilitate mazingira, sio kwamba yeye ndio anatungenezea. Anatusaidia pia katika technology transfer kuja nchini. Anao mainjinia na wataalamu alioajiri wazawa, ambao sasa wanaelewa nini kinahusika kutengeneza cement na wanaweza kuwezeshwa kuanzisha viwanda, hata kwa ubia
 
Yote hayo yameboreshwa na ndio maana unaona wawekezaji wanapishana kila siku Tanzania uongozi wa Rais Samia Suluhu umezalimilia kukuza uwekezaji pia kupitia uwekezaji vijana wapate fursa
Hilo ni jibu la kisiasa, tunaloita generic response, ambayo Watanzania ni hodari sana kuyatoa(Wakenya wanaita Kiswahili mingi). Unajibu bila kujibu.

Niambie kipi kimeboreshwa kuhusu visa na residency permits kwanza. Tuanzie hapo, specificities.

Unawaambiaje Wamarekani njooni kuwekeza Tanzania ina amani wakati wanajua Lissu yuko Ubelgiji mkimbizi wa siasa hadi leo, Lema yuko Canada, hutaki mjadala wa Katiba mpya wapinzani wanaopendekeza? Utawadanganya Wamarekani?

Wakikuambia katiba mpya ni positive thing kwa nchi yeyote hata sisi USA tumefanya amendments za katiba mara nyingi, unawajibu hiyo sio priority yangu au sio jambo lilikuwa kwenye ilani ya chama changu kwenye uchaguzi. You must be joking. Watakuona unawapotezea muda.
 
Very deep, bila shaka watakuelewa..

unataka mwekezaji aje huku watu wako maofisi kila kitu rushwa na mambo mengi konakona.

Unataka wawekezaji waje huku work force yako kwa kiasi kikubwa ni unskilled, wavivu, watu wako sio waaminifu wadokozi, wezi wanawaza maisha rahisi

Unataka wawekezaji waje wafokewe na makada wasiojua lolote wala chochote, zaidi ya uchawa, uchawi, na ngono ndio vimewafikisha hapo.

Unataka wawekezaji waje halafu makada wa chama chetu wawalazimishe wawape kazi ndugu zao unskilled, wezi nk, makada walazimishe vikampuni vyao vipate contracts za kazi.

Weka sawa mifumo, tengeneza jamii inayoishi kwa misingi, chama cha makada kikubali dunia imebadirika nacho kibadili mfumo wake wa ujinga ujinga kulea na kukuza vijana wa hovyo...nk nk
 
Sema wewe kiazi, sisi mihogo tutaambiwa tuna mizizi. Ukweli mtupu umeandika. Hakuna mtu anayebembelezwa kufanya biashara sehemu fulani. Mwekezaji ni mfanya biashara na si mzee wa kanisa. Anachoangalia ni sehemu yenye maslahi kwa uwezekaji wake. Mengine ni kujidanganya tu.
 
Ukiwa huna hayo lazima umbembeleze,sio rahisi kwa hayo Mambo kufanyika kirahisi maana mengi take yanahitaji pesa
 
Hii Ni Africa hayo Mambo hayaondoki overnight
 
Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)


Kwa jambo hilo Watz tumelaanika.!!--- tumefanya wizi, udokozi, rushwa, ufisadi, nk katika ngazi zote ni jambo la fahari.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Fikiria unakuta li waziri lina hojiwa kwenye TV, linaanza kuchokonoa pua na vidole.....
Hapo mwekezaji anachoka kabisa....
 
Viongozi wetu wanaotunga sera na kusimamia sijui huwa wanasomea nini vyuoni kama mambo basic tu kama haya hawayaelewei! Inafikirisha sana.
 
Viongozi wetu wanaotunga sera na kusimamia sijui huwa wanasomea nini vyuoni kama mambo basic tu kama haya hawayaelewei! Inafikirisha sana.
Wako bize kuibia umma tu na kuhakikisha ccm ina dumu madarakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…