Rais Samia, hata siku moja mwekezaji habembelezwi kuja kuwekeza nchini, tafadhali zingatia yafuatayo watakuja wenyewe

English iwe medium of instruction kuanzia chekechea nchi izungumze lugha ya dunia na staff waelewe lugha ya kuendeshea mitambo!

Reli ziunganishe mikoa yote ili bidhaa za wawekezaji zisafiri kwa wingi kwa bei chee na kwa haraka

Umeme usikatike kama enzi za Magu kwasasa uozo mtupu huko wizara ya mashati aka nishati !

Bandari ipunguze ushuru kwa wawekezaji wakubwa!
 
Nyie watu bana!!
 
umenena vyema
 
Kwa jambo hilo Watz tumelaanika.!!--- tumefanya wizi, udokozi, rushwa, ufisadi, nk katika ngazi zote ni jambo la fahari.
Kweli Mkuu. Kama mtu atakuambia kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu kazini ndio msingi wa maendeleo, basi mwambie wazi Tanzania hatutakaa tuendelee kamwe!

Unakuta unafungua biashara au kiwanda, unawapa watu ajira, wanakuibia hadi unafilisika, unafunga biashara, wanaanza kulalamika kukosa ajira!
 
Wizara ya fedha Ina wachumi wengi tu,tic Kuna wachumi na wataalam wa biashara wengi tu,mtoa mada kadhihirisha tu ujuha na ujuvi wake
Unachomanisha ni kwamba wizara ya fedha ina watu waliosomea uchumi. Sasa kusomea uchumi chuoni sio kwamba ukipewa kazi za uchumi basi wewe ndio utaweza kufanya mambo yaende vizuri, la sivyo kusingekuwa na taifa masikini duniani maana kila taifa duniani lina maprofessor wa uchumi.

Mwigulu Nchemba kasomea mambo ya uchumi lakini bado anashindwa kusimamia uchumi wa nchi tukaendelea anakimbilia kwenye tozo, anasema hakuna Mtanzania atagongewa mlango kulipia deni la Taifa. Hiyo ni lugha ya kuongea msomi wa uchumi?

Mtu akisema hakuna mtu atagongewa mlango kuombwa hela za mishahara na posho za wabunge ana akili huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…