Rais Samia: Hata Washington umeme unakatika ingekuwa Tanzania, Makamba angetukanwa

Rais Samia: Hata Washington umeme unakatika ingekuwa Tanzania, Makamba angetukanwa

Rais Samia Suluhu Hassan akiwahutubia watanzania walioko Marekani amesema alishangazwa na umeme kukatika nchini humo ambapo amesema ingekuwa Tanzania, January Makamba angetukanwa
View attachment 2203746
Rais anashangilia umeme kukatika badala ya kujipanga amalize tatizo.

Yani hajui umeme kukatika nchi ya ughaibuni linaweza kuwa tatizo kubwa la kiusalama kwake.

Jambo la hatari, anachekelea.
 
hapo mwisho unasikia minong'ono ya watu ikipinga kuwa so kweli umeme haukukatika itakua ni shida ya kiufundi ktk jengo... US umeme ukatike kirahis hvyo
 
Rais anashangilia umeme kukatika badala ya kujipanga amalize tatizo.

Yani hajui umeme kukatika nchi ya ughaibuni linaweza kuwa tatizo kubwa la kiusalama kwake.

Jambo la hatari, anachekelea.
Huyo video tu mwishoni hao wanaomung'unya maneno inaonyesha kuwa umeme haukukatika bali ni hitilafu kwenye hilo jengo
 
Huyo video tu mwishoni hao wanaomung'unya maneno inaonyesha kuwa umeme haukukatika bali ni hitilafu kwenye hilo jengo
Kuna siku moja nilikuwa namsikiliza mama wa miaka zaidi ya 60 wa New York City.

Anajitapa kwamba kala chumvi sana.

Anasema kaishi sana, maisha yake kapata kuona umeme ukikatika mara tatu jijini New York.

Nikasema bahati yako hujafika Vingunguti.
 
Yaani kapata bahati umeme kukatika akiwa amerika basi imekuwa sababu kuifananisha Amerika na Tanganyika!.
 
Ni kawaida yake kuyashadadia matatizo, refer: vitu vitapanda bei.
 
Huyu mama anapenda sana kufanya justification akiona jambo haliwezi. Ni dhahiri suala la umeme limemshinda. Hata alipoona watu wanalalama juu ya bidhaa kupanda akasema sababu ni vita ya ukrain, matokeo yake bei ikapanda zaidi.

Kwa maneno haya tutegemee umeme kuzidi kukatika na tanesco kuipuuza hiyo kero ya kukatika umeme maana wameambiwa hata washington unakatika. Yawezekana walikuwa bize kuhakikisha umeme haukatiki ili wasimkere maza ila kwa kauli hii watarelax.
 
Sidhani kama Mama amefikiria marambili kabla ya kutoa hicho kionjo. Yawezekana umeme ulikatika kwenye lile jengo tu, Au ulikatika kwenye ule mtaa tu (transformer), au ulikatika kutoka kituo cha usambazaji umeme (sub-station). Issue ya umeme kwenye nchi ni very sensitive na wananchi wana hasira kwa sasa. Kwahiyo lolote atakalosema kwenye eneo hilo la umeme, anatakiwa awe makini zaidi. Hata kama ni kionjo, huwezi kuleta kionjo cha kaliba hiyo katikati ya msiba, tena kwa mfiwa.
 
Back
Top Bottom