Rais Samia: Hatutatoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa

Rais Samia: Hatutatoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba Wizara ya Mambo ya nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za haraka kwa wanaotumia mitandao na teknolojia vibaya, akikemea pia wingi wa wanaharakati kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani.

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumatatu Mei 19, 2025, jijini Dar es Salaam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, akitaka kutotoa nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nje ya nchi kuja kujaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama uliopo nchini Tanzania.

"Nimeona Clip kadhaa za kunisema, mara nina ubaguzi na nini! Ninalofanya ni kulinda nchi yangu na ndiyo wajibu wangu niliopewa. Kwa hiyo hatutotoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvuruga hapa awe ndani ama anayetoka nje," amesema.

Katika maelezo yake, Rais Samia ameitaka Wizara na Maafisa wanaohusika kutoa ufafanuzi kuhusu yale yanayosemwa na wanaharakati na watu mbalimbali, kukanusha ama kuchukua hatua za haraka ikiwa yanayosemwa yana ukweli kuhusiana na sekta zao mbalimbali.

 
Kweli wageni wanaweza kukuvuruga lakini kwenye hili amejivuruga mwenyewe. Kama yasingefanyika ya hovyo kama haya wageni wangekuja kufanya nini. Tena kwa hii speech ndio amejivuruga zaidi.

Angalia karusha mpira kwa watu wa chini yake kujibu na kutoa ufafanuzi. Kwa nini asifanye nini kama mkuu wa nchi? Mambo mengi yametokea watu kutekwa-kuachiwa. Hakuna aliyetoa maelezo, ambapo kwa akili ya kawaida ulitegemea yeye ndio atoe uelekeo, lakini waaaapi! Sasa hapo si ndio atasemwa zaidi?!
 
Back
Top Bottom