Rais Samia, Hotuba ya Nape na Makamba ni ya kutupumbaza watanzania. Wana jambo lao

Rais Samia, Hotuba ya Nape na Makamba ni ya kutupumbaza watanzania. Wana jambo lao

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Mh. Rais Samia.

Nimesikiliza hotuba za hawa watu wawili, Makamba Jr (Jana) na Nape(Leo). Hawa watu wanajua kucheza na siasa ili mambo yao yakubirike kwa jamii. Ukiteleza kidogo tu wana wewe.

Ukiwaangalia kwa nje ni kama kondoo lakini kwa ndani wanalo jambo lao. Ni vile mimi nimeanza kukuelewa kwa uongozi wako na kwa vile nawajua hawa watu wawili nakushauri kuwa nao makini. Imebidi niandike hapa kwa kifupi baada ya kufutatilia nyendo zao kwa makini.

Kwanza wana watu wengi Nyuma yao na wanakubarika kwa hao watu.

Pili wana hasira sana na mambo yanavyoenda kwa maana wao kukosa nafasi katika uongozi wa nchi hii.

Tatu wanataka wapate fadhira kwa kuwa wazazi wao wamekuwa ndani ya chama kwa mda mrefu.

Nne, Kifo cha Magufuli kimewakatisha ndoto yao ya kuukwa urais 2025 kwa kuwa sasa ni wewe unagombea.

Nia yao hasa ni hiyo Nne. Bado haijafa kabisa.

Fuata Hotuba ya Joseph Gwajiba ya leo nawe utafanikiwa.

Nakushauri kuwa nao makini.
 
CCM ni janga la Taifa wao kwa wao wanaanja kuparuana yetu macho
 
Wazazi wao ndio walioasisi Tanu na hatimaye CCM?!!
Kuna mambo yanaendelea sio mazuri sana ndugu yangu.

Kuna watu wanaumia sana kuendelea kuwa nje ya chama na wanaona wana CCM wengine hawanahaki kwa sasabu hizo.
 
Nne, Kifo cha Magufuli kimewakatisha ndoto yao ya kuukwa urais 2025 kwa kuwa sasa ni wewe unagombea.

Mi nikafikiri kuwa, kifo cha JPM kimekuwa nafuu kwao, kwani ile... TUTAMLAZIMISHA AGOMBEE TENA,..... mara… MITANO TENA... haipo tena!!?
 
Kama Gwajima amekuwa mtu wa kusikilizwa ndani ya chama chenu basi mmefika mwisho wa kufikiri
 
Huyo mama hata asigombee 2025 akapumzike tu alee wajukuu.
 
Utetez wako ni weak sana, makamba alikua open kbs na alicho shauri. Je kwa wale walioshauriwa na makamba wao unawazungumziaje?
 
Mtoa hoja ninaamini sio mganga wa kienyeji,wewe umejuaje hisia na malengo ya hao uliowataja?je wewe ni spokesperson wao?kwani katiba ya ccm inawazuia kugombea urais au nafasi yeyote ile?watanzania tu watu wa ajabu mno na tunakokwenda tutakua Taifa la walalamikaji na mbaya zaidi kulalamika bila FACTS.
 
Afuate ushauri wa Josephat Gwajima huyu huyu aliyemwaminisha Magufuli kwamba kutovaa barakoa na social distance tumeshashinda matokeo yake wote tunayajua?
Mbowe karibu damu itaganda kwa chanjo.
 
Hoja ya kijinga sana hii. Nchi hii wapuuzi hawataisha, mleta mada mmoja wapo
People have to talk so that tufahamu which is which.
Uzuri mule ndani wote wana kinga za kusema chochote, kama walivunja sheria wangeliambiwa kutengua kauli.
 
Mtoa hoja ninaamini sio mganga wa kienyeji,wewe umejuaje hisia na malengo ya hao uliowataja?je wewe ni spokesperson wao?kwani katiba ya ccm inawazuia kugombea urais au nafasi yeyote ile?watanzania tu watu wa ajabu mno na tunakokwenda tutakua Taifa la walalamikaji na mbaya zaidi kulalamika bila FACTS.
Pia, for record, Makamba alisema kabisa tusihukumu dhamira za wanao sifu au wanaokosoa!
 
Back
Top Bottom