Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Rais Samia: Hakuna kisichowezekana kwenye mazungumzo, tumeshuhudia nchi kadhaa zimeingia kwenye vita hawakupata suluhu, suluhu imepatikana kwenye mazungumzo kwahiyo tuendelee kuzungumza. Najua si rahisi kabisa watu kuja na utamaduni huu mpya ukakubalika mara moja, si rahisi, kwenuu kuna vikwazo kwangu kuna vikwazo.

Huwa napitia Jamiiforums naangalia maoni yenu kule ndani, nasoma nnacheka, nasema lakini huu ni utamaduni mpya, si rahisi kukubalika kwa ghafla, kwahiyo pande zote Tanzania nzima si rahisi kukubali utamaduni huu mpya kwa haraka.

Your browser is not able to display this video.

======


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanawake wa CHADEMA, viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.

Rais Samia alihudhuria kongamano hilo akiwa mgeni rasmi aliyealikwa na wanachama hao, Rais Samia amesema utamaduni wa mazungumzo ni mgeni kwa nchi yetu na unaletewa vikwazo kwenye pande zote mbili
yaani mamlaka pamoja na CHADEMA, lakini amesisitiza ndio njia salama ya kufikia makubaliano katika kutatua changamoto na kuahidi kuendelea na mazungumzo ili kufikia maridhiano.

Katika kongamano hilo Rais Samia amewaambia wanachama hao kuwa amekuwa akipita katika mtandao wa Jamiiforums.com na kusoma maoni yao huko ndani na kisha anacheka. Kauli hiyo imeamsha ari ya wanachama na watanzania wengi na kuwaongezea motisha katika kutumia mtandao wa Jamiiforums kwa kuona kuwa ni sehemu salaa na ya uhakika ambayo wanawasilisha mawazo na maoni yao moja kwa moja na kusomwa na Rais na viongozi wao mbalimbali ivyo kupata uhakika wa mawazo yao kufanyiwa kazi.

Baadhi ya maoni ya wanachama wa Jamiiforums.com

Pia soma: Moshi: Yanayojiri katika Kongamano la BAWACHA Siku ya Wanawake Duniani Machi 3, 2023; Rais Samia mgeni rasmi
 
Ameyaweka wazi hayo katika mkutano wa Bawacha katika siku ya mwanamke duniani.

Rais Samia akihutubia taifa kupitia mkutano huo amewaambia kuwa huwa anasoma maoni ya katiba mpya, wabunge wa Covid19 na mengineyo kuhusu Serikali yake kupitia mtandao maarufu wa JamiiForums.

My take:
Leo ndio nimejua kuwa kumbe Rais Samia nae ni mdau wa JamiiForums.

Hii imetuinua sana wana jukwaa hili.
 
Nasikiliza hapa kwa redio mh rais anasema Huwa anapita humu kuangalia baadhi ya maoni ,

Anasema Huwa anacheka sana kuona wanaomkosoa

Mimi napenda kusema kosoa kwa staha
Tema madini yako
Huenda mkuu akakuona unafaa akakuchagua kutoka humu jamiiforums

Inawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…