Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Oilcom
 
Mods, JF imepewa heshima kubwa sana. Kama Rais huwa anapitia humu kupata maoni yetu kama sehemu ya umma wa Watanzania, hakika nawaambieni, hakuna kiongozi ambaye hatapita JF.

Lakini ili maoni yetu yapewe uzito wa kupewa tafakuri ni lazima Mods walinde hadhi ya jukwaa kwa kuwapa adhabu kale wale wote wanaoligeuza jukwaa lionekane ni la wahuni.

Mtu akitukana au kukejeli, apigwe ban hata ya miezi 6 au mwaka mzima. Kuna watu humu, wanashangaza, wanafikia kumtukana kiongozi, unatafakari na kujiuliza JF siku hizi imebeba watu wa namna gani?

Mods, lirudisheni jukwaa kwenye heshima yake ili kiwe ni chanzo muhimu cha habari kwa wasio na habari, liwe ni jukwaa la ushauri kwa viongozi wa Serikali, vyama na taasisi mbalimbali.
 
Eeeh kiongozi mwenye MYCINE zake za kutosha.😂😂😂
 
Pia waone namna ya kupunguza au kumeneji hizi mada za ngono naapenzi, zimekua nyingi mno na zisizo na mashiko.
 
Alivyoitaja leo najua wengi lazima watapita kujua kinachoendelea, watakutana na matusi, na nyuzi za ajabu ajabu
 
Mbona kama umechukia?
Hapana mkuu. Nimefurahi pia kusikia Rais wa nchi anapita hadi humu kusoma maoni yetu maana inamsaidia kujua kero ambazo chawa wake huwa hawamfikishii kwa maksudi ama wanamficha.

Hapo nilitaka kumwambia member mwenzangu kwamba Rais anapita karibu mitandao yote ya kijamii tena kwa ID orijino kabisa tofauti na huku hata hatujui ameingia kwa Id gani.
 
usikute humu JF ndiyo chaka lake la kupatia usingizi baada ya vurugu za mchana kutwa, asiishie kucheka tu pia atupe ufumbuzi wa changamoto zinazoletwa hapa ili kuipa forum heshima kwa vitendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…