Rais Samia ikiwezekana kwepa kuwalenga Wasukuma moja kwa moja kwenye hotuba zako

Wasukuma ni wapambanaji wanaojua kutumia rasilimali za nchi yao tanzania
 
Waandishi wa hotuba za Madam President wanapaswa kuwa makini mno na maudhui yaliyomo ndani yake. Anapaswa kuzungumzia mambo ya msingi kwa kutaja tu sekta husika wala si kwa kutaja kabila.

Wasukuma ni moja ya kabila kubwa na lenye watu wengi hapa nchini. Kutaja tatizo mojawapo linalopelekea uhaba wa maji unaoendelea hapa nchini kunaendana na shughuli zao za ufugaji ni kutokuwatendea haki.

Lazima tuwe wakweli, chanzo cha uhakika cha maji katika nchi yetu kinategemea misimu ya mvua. Mvua zikiwa za kutosha hutasikia kelele kuhusu uhaba wa maji.

Nakumbuka kuna nyakati Mh. Ngoyayi akiwa Waziri Mkuu aliwahi kuleta wazo kutoka Vietnam la kutengeneza mvua ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji. Kwa hiyo basi uhaba wa mvua si kitu kigeni hapa nchini, huwa kinajirudia kutoka kipindi kimoja kwenda kingine. Hakuna haja ya kuwanyooshea kidole Wasukuma.
 
Niliogopa mno aliposema "tena Wasukuma!"
Wasukuma ni AKILI KUBWA hata mama anajua hivo.
Mama Samia bado anahangaishwa na mzimu wa Marehemu Magufuli.
Ni Bora akaacha kuwasakama Wasukuma akawa mpole maana Uchaguzi wa 2025 hauko mbali sana. Asije akaikosesha CCM kura za Urais 2025.
Huu ni ushauri wa bure kabisa.
 
Niliogopa mno aliposema "tena Wasukuma!"
Wasukuma ni AKILI KUBWA hata mama anajua hivo.
Mama Samia bado anahangaishwa na mzimu wa Marehemu Magufuli.
Ni Bora akaacha kuwasakama Wasukuma akawa mpole maana Uchaguzi wa 2025 hauko mbali sana. Asije akaikosesha CCM kura za Urais 2025.
Huu ni ushauri wa bure kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…