Rais Samia ikukupendeza tuondolee DC Magoti hapa Kisarawe, amefeli kila kitu

Rais Samia ikukupendeza tuondolee DC Magoti hapa Kisarawe, amefeli kila kitu

Watu hatuna maji yeye analeta story za uchaguzi. Tuliambiwa kuwa hapo ikulu alikufelisha na wewe ukaamua kuturushia huku Kisarawe huku ni majanga kabisa .

Hapa Kisarawe wilaya nzima hatuna maji yeye yuko size na ishu za uchaguzi utadhani anagombea

Barabara mbovu kila sehemu yeye yupi size na uchaguzi tu na matamko .

Ikikupendeza muondoe tuletee anayeweza kazi

USSR
Sasa Mkuu wa Wilaya atoe wapi pesa za Barabara na Maji.

Hiyo ni kazi ya Mkurugenzi na Waziro wenye mafungu ya budget.
 
MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOSHI KINARA WA MAKUNDI YA KISIASA MOSHI MJINI
Kama tunavyotambua kuwa watumishi wa UMMA hawapaswi kwa namna yoyote ile kujihusisha na siasa hasa zenye malengo ya kuigawa jamii wanayoiongoza ( rejea kanuni za maadili za viongozi wa UMMA)
Ndugu wana Moshi Mtakumbuka kulikuwa na maswali mengi juu ya uwepo wa Group la Whatsapp la Moshi ya Moto ambalo limekuwa na kazi kubwa ya kutukana na kudhalilisha viongozi na watu mbalimbali kupitia maneno, picha na sauti.

Swali lilikuwa je nani anawapa kiburi vijana hawa, nani yuko nyuma yao ambaye anawafanya kujiona wao ni bora kuliko vijana wote wa Moshi?

Katika kutafuta ukweli wa mambo hayo, uchunguzi ulianza kufanyika kuanzia August 2024 hadi feb 24 2025 ambapo pasipo na shaka majibu ya uhakika na kweli yamepatikana ambayo niko tayari kutoa ushahidi kwa mamlaka yeyote juu ya ukweli wa mambo haya ya hovyo ambayo yanaendelea kwenye mji wetu.

Vijana hawa Idirisa Makishe mwenye namba 3 kwenye group na Iddi Chaku mwenye namba 3 kwenye group la moshi ya moto, wanasimamiwa na Priscus Tarimo Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini na Mwajuma Nasombe Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ambao mbali na kuendesha genge la matusi kupitia hawa vijana wamekuwa ni watoa maelekezo na ushauri juu ya namna ya uendeshaji wa program yao ( rejea kielelezo na. 011.

Watu hawa wamefika mbali hadi kuanzisha group la siri ambalo ndio hutumika kujadili na kupanga mipango yao hatarishi huku wakijadili mambo mazito ambayo ukichunguza ndani yake yana sifa za uharifu (ujinai) ( rejea kielelezo 012)

Japo ni haki kwa kila mtu kuwa na group la whatsapp lakini muungano wa Mbunge, Makishe, Chaku, Mwajuma katika group moja na kujadili na kupanga mambo ya kisiasa, kampeni chafu na kutoa maelekezo ni kosa kubwa sana la kimaadili kwa wao ambao ni viongozi wa Umma.

Sote tunatambua wakurugenzi ni watendaji wa kuu kwenye uchaguzi mkuu, vitendo vinavyofanywa na Mkurugenzi kwa kuunda makundi na kushiriki kuhujumu watia nia na kuwagawa wanachama kupitia group la Moshi ya Moto vinaichafua serikali na kuondoa imani kwa wananchi juu ya upatikanaji wa haki katika uchaguzi huu.

Watu wengi wanajiuliza kwa nini kumekuwa na malalamiko mengi juu ya Mkurugenzi huyu kwenye masuala ya kisiasa na upendeleo kwa baadhi ya vijana? Ukichunguza kwa kina utagundua uwepo wa vijana hawa na group lao la Moshi ya Moto ni kinga kwake na baadhi ya watendaji wachache wazembe. Imeshakuwa kawaida kwa mtu yeyote atakaye thubutu kuhoji jambo lolote linalohusu halmashauri mfano Uchafu wa mji, ujenzi usiofata mpango miji, rushwa, matumizi na ugawaji wa maeneo ya wazi, mikopo ya 10%nk wamekuwa wakishambuliwa, kudhalilishwa kwa matusi na maneno makali ikiwa ni mbinu ya kuwanyamazisha wasihoji.

Vijana hawa wamekuwa wakimtukana na Kumdhalilisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mhe. Zuberi Kidumo na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi mjini kwa nyakati tofauti hali inayozidi kushangaza watu kuona Mkurugenzi ambaye ni katibu wa Meya kwenye baraza anakuwa na vijana ambao wana mdhalilisha Mwenyekiti wake huku wakimshangaa Mhe. Mbunge kwa kufadhili group ambalo lina mtukana mwenyekiti wake wa CCM wilaya mzee FARAJI SWAI.

Kwa namna yoyote ile wanamoshi kwa ujumla hatuko tayari kuona watumishi wa UMMA wakiunda makundi na kuwagawa wana Moshi kwa misingi ya kisiasa ,kidini au kiukabila..
Tunatoa rai kwa Viongozi wa Umma kuzingatia sheria na kanuni za utumishi na kujiepusha na kuingilia siasa.

Tunaomba mamlaka zifanyie kazi taarifa hii na kuchukua hatua za haraka ili kurejesha imani kwa wananchi iliyopotea kutokana na watendaji wasio waadilifu.
Chama cha Mapinduzi kinapaswa kumuita Mbunge na kumuonya juu ya ufadhili wake wa viongozi wa moshi ya moto na kumwagiza kuwaelekeza vijana wake kuacha mara moja tabia ya kumtukana mwenyekiti wa CCM Wilaya ya moshi mjini.

Tunaomba ofisi ya RCO kuchunguza kwa kina juu ya group hili la siri kwani miongoni mwa mazungumzo. yanahusiana na matukio kwani ukisoma kwa kina utagundua kuna siri inaificha.

Mwisho tuna Muomba Mkurugenzi Mwajuma ikiwa anataka kugombea Ubunge wa Moshi mjini ajiuzuru nafasi yake ili afanye siasa..maana hiki anachofanya ni kuidhalilisha mamlaka iliyomteua.
 
Kweli kabisa .
Kumshambulia Magoti peke yake ni chuki binafsi .

Mimi kwa mtizamo wangu wakuu wote wa mikoa na wilaya wamefeli Sana hawstahili kukalia hizo nafasi .

Nafasi za Ukuu wa Wilaya na Mikoa zinastahili kupewa wanajeshi ,Polisi na usalama wa Taifa basi ((Usalama wa Taifa waliosomea medani za kivita na usalama wa nchi kwa ujumla sio wapambe kama wale wahuni wa Green Guard na red Guard 😂😂😂)).

Nafasi za Ukurugenzi wanatakiwa Wapewe Walimu hasa Mahead master waliofanya vizuri kwenye mashule ya serikali kwenye usimamizi ndani ya Halmashuri zao au Maafisa Elimu waliosimamia vizuri kazi za maendeleo ya Elimu kwenye Halmashuri zao . Lakini Pia Wakurugenzi wanatakiwa wawe ni maofisa ndani ya Halmashauri kama Vile maafisa kilimo ,mdaktari na mafisa wazoefu ndani ya Halmashuri .


Kwa Tangu Kikwete hizo nafasi zimekua za kupeana kama zawadi au ushkaji na hata nyumba ndogo .
Hali inayosababisha usimamizi toka juu unakua mgumu sana.
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wengi wapo kama Machawa wa Rais na sio wawakilishi wa Rais .
Matokeo yake miradi ya serikali inajengwa kwa kiwango cha chini sana . Rais anazindua jengo leo na bada ya miaka mitatu lina nyufa kama Chekecheke wakati mkuu wa Wilaya yupo .

Yote ni kwa sababu ya dharau kubwa ya wanasiasa kwa majeshi yetu na pia kupandikiza Machawa ndani ya majeshi hivyo kuyaona sio chochote sio lolote .
Watu wote wanaokua chini ya Rais wanatakiwa wawe ni wawakilishi wa Rais na wanaopokea amri ya Rais na kuisimamia kama yeye mwenyewe kwa usahihi na kwa utii.

Ndio maana wakati wa Mwalimu walikua na Elimu ya kawaida lakini walisimamia miradi ya maendeleo kwa uzalendo mkubwa . Hata ukiangalia miradi ya enzi za mwalimu zilijengwa kwa ubora zaidi japo Bajeti ilikua finyu na teknolojia ndogo na mawasiliano madogo.

Mtu hajawahi kuwa hata Afisa mtendaji wa kata leo anakua mkuu wa Wilaya .!!
Umeangazia mambo mengi na kumshauri Rais vizuri, mimi sijui lakini naamini huwa anapita pita humu atayaona haya. Mwisho kabisa ingelipendeza sanaa kuwe na ufafanuzi wa majukumu ya DCs na RCs. Mada kama hii kwa dunia ya leo inadhihirisha kuna mambo hayapo sawa kwenye elimu ya Kiraia.
 
Back
Top Bottom