#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

Zaidi ya hayo kwanini Marehemu awe Magufuli pekee na si wengine?
Miaka 20 tunamsema Nyerere , hivi karibuni Mkapa kwanini JPM awe tofauti

Wanaotaka Marehemu Magufuli asisemwe wanasababu moja 'kuficha jambo'' . wanatumia ngao

Magufuli alikuwa public figure aliishi kwa kodi zetu tuna haki ya kumsema kwa kila kitu

Kitu kisicho haki ni kumsingizia jambo au kumzushia!
Kumdai si kumsingizia, wadai wanataka deni lao la haki

Kama ulivyosema ana madeni ya haki!
 

..una hoja nzuri sana.

..lakini tusiwazuie watu kunena mambo mazuri ya Magufuli.

..vilevile tusiwazuie watu kenena mambo mabaya ya Magufuli.

..naamini jamii ina mambo ya kujifunza toka pande hizo mbili.
 
Huyu kabebwa na umakamu wa Rais tu.

Peke yake asingeweza kupenya hata 10 bora endapo angegombea urais.

2025 atapita kwa kubebwa na dola pamoja na tume.

JPM alikosea sana. Na hii iwe wake-up call kwa presidential wannabes wote. Hii habari ya kuteua bora mgombea mwenza ni potential disaster. Rais hana mkataba na Mungu juu ya maisha yake!
 
Huyu ndio raisi tunaemuhitaji, "say as it is." Twende taratibu bi Samia, mwisho wake Watanzania watakuelewa. Wamezoea kuongopewa na kubaki kunong'ona tu bila kuwa na habari kamili.

Ipo siku Bi Samia atatuambia ukweli kuhusu zile wiki mbili za mtafaruki za kutokujua Rais Maghufuli yupo wapi? Ana hali gani? Yupo hai au amefariki? Hali iliyolifanya Taifa kumuamini Kigogo kuliko muhimili wowote ndani ya nchi.

Kutofautiana mawazo baina ya viongozi ni suala la kawaida. Labda ni kwa sababu statement imetolewa ugenini. Marehemu Kambona alitofautiana mawazo na Mzee Nyerere kuhusu mustakabali wa nchi, ikambidi akaishi ukimbizini. Mwalimu Seif na Marehemu Aboud Jumbe sote tunajua yaliyowakuta.Tofauti iliyopo sasa hvi ni kwamba bi mkubwa ndio raisi. Hamna atakaemgusa.

Namuombea Mungu pindi atakappmaliza muda wake wa uraisi, atuandikie na kitabu ili tujue system operate namna gani. Marehemu Magufuli aliuwawa kwa sumu au walimziba pumzi na mto?
 
Na kwasababu hiyo hata ilani ya chama haikubali kwakua ilitengenezwa chini ya uenyekiti wa JPM ambaye yeye amekiri kutokubaliana naye; basi na ajiuzulu kulinda heshima yake ili mwenye kukubaliana na hii iliyopo na iliyopigiwa kura aendeleze utekelezaji wake. Yeye aje agombee 2025 akiwa na mawazo yake hayo tofauti na yale waliyoyachagua wa Tanzania 2020 ambayo yeye hakubaliani nayo; vinginevyo hii ni justification ya wazi kwanini Katiba mpya ni hitaji la sasa na siyo kesho.
 
JPM alikosea sana. Na hii iwe wake-up call kwa presidential wannabes wote. Hii habari ya kuteua bora mgombea mwenza ni potential disaster. Rais hana mkataba na Mungu juu ya maisha yake!
Dawa ni katiba mpya kuweka wazi jinsi ya kuterminate end ya huyo aliyeondoka na kuchagua mwingine.
 
Awe na kifua basi. Akisema mambo ya ndani ya serikali iliyopita ambayo alikuwa namba 2: Itamuongezea nini? Asije akasema na vingine.
Je si kosa kusema mambo ambayo aliapa kuyatunza ili kulinda collective responsibility? Je katiba haijavunjwa hapo? This is going beyond control mtu wakumshauri na apatikane basi otherwise hii precendence ni mbaya sana na implication kwa mtu kama mimi ni kuwa mkuu wa nchi anauwezo wa kufanya apendalo na hakuna wakumwajibisha including kuhujumu nchi.
 
This is bad and very insulting. Unakosoa uuambaji wa Mungu? Wewe hukuzaliwa na mwanamke ? Shame on you! You are disgrace.

S
Kuna watu wanakosa busara kabisa, kwani akiingia period na yeye haendi chooni? What is a difference? Tumhukumu kwa makosa yake na siyo kumdhalilisha kama alivyofanya huyo
 
Kusemwa ni haki, lakini kusema kwamba walishindwa kufanya yaliyo sawa kwasababu yake that means kuna shida kwenye mfumo na kama ndivyo hawa waliopo watashindwaje kurudia yale yale yasiyokubalika kwa wengi kama alivyofanya huyo anayedaiwa haki? Nani anapima haki ya sasa tofauti na ya huyo tunayemdai? KATIBA MPYA NI HITAJI LA SASA KULIKO BAADAYE!
 
Hivi si aliapa pia kutunza siri alizozijua wakati akiwa kwenye nafasi, ama?
Huyu Mama Samia hata hakumbuki aliapa nini hata ukiuliza atakwambia jaji alinipa kilikuwa kimeandikwa akasema nisome kwa sauti hata sikumbuki kilikuwa kinasemaje labda ukamuulize jaji aliyeniapisha
 

Hivi kosa lake ni kusema kwa maneno?
Mbona kila siku anafanya kinyume hakuna tatizo, kutamka tu imekuwa tatizo!

Kawaondoa wapambe wa Magufuli kawarudisha waliondolewa na JPM.
Rais SSH anahimiza chanjo, JPM ahakutaka kusikia kitu hicho
Rais SSH anazungumza wazi ufa wa udini, ukabila , JPM ilikuwa haikuwa hivyo
Orodha inaendelea kurasa 1001

''Marehemu hasemwi, yaliyopita si ndwele, tuangalie mbele'' kwa lengo la kufunika ya nyuma! fiddlestick

UK, PM Sir Churchill '' All men make mistakes, but only wise mean learn from their mistakes''

Nakubaliana JPM ameonyesha ubovu wa mifumo ingawa wengine tulisema miaka 10 iliyopita.

Ni muhimu tujifunze mifumo inavyoweza kutumika vibaya kwa mfano halisi wa Mwendazake

Rais SSH kueleza kilichomtokea ni kawaida. Kuna maswali hawezi kuyajibu bila kueleza 'position' .

JPM ni public figure kama Nyerere na Mkapa hana 'immunity' kwa masuala masuala yenye masilahi ya Taifa. JPM aliomba kazi akijua hadhi , mamlaka, ukubwa , majukumu na uwajibikaji wake ikiwemo kutokuwa na privacy au immunity katika scrutiny

JokaKuu amesema vizuri sana kuhusu deni, wadeni na mdaiwa !
 
Makamu haruhusiwi kuachia ngazi ?

Unless otherwise ni necessary sio uungwana saana to kick a dead man (its political but not diplomatic)
Unajua maana ya sentensi uliyoiwekea mabano???
its... Hii lugha ya watu mnapenda kuiparamia
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli...
Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO 19
View attachment 2188625
Utopolo mtupu.
Wote waliokuwa chini uongozi wa MAGU walikuwa na tabia chafu kusifia sivyo wangeamua kuondoka! Waliunga sana hoja zake Leo inakuweje wanamgeuka mchana kweupeh!!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…