#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

Magufuli alitofautiana na bitozo siyo kwasababu ya covid
Naomba niishie hapo.

ila ukiipata story yote inabidi uwe na kifua cha kuitunza
Tumwagie Mzee,yule jamaa alikuwa ni taahira Sana..

Kutofautiana kupo ila mambo mengine inakuwa ni too much,hata sasa VP bila shaka anatofautiana na Rais but Rais anatoa mda wa kuwasikiliza ila sio kudharirisha.
 
Hata kama ni kuwashobokea sio kwa alichofanya hata wao wanamdharau ndio mana wanampa makamu apige nae story mwenyeji yuko busy
Kwani kafanyaje? Kusema walitofautiana mawazo na Mwendazake au? Kwamba hili ni kosa au?

VP sio mtu mdogo,Tzn ina umuhimu gani hadi Biden iwe lazima kuongea na Rais?
 
Awe na kifua basi. Akisema mambo ya ndani ya serikali iliyopita ambayo alikuwa namba 2: Itamuongezea nini? Asije akasema na vingine.
Hili la corona ni jambo dogo kwani Lina shida gani kusema kila mtu alikuwa na Maoni tofauti kwenye njia za kukabiliana?

Kwani ni Siri? Si kila mtu Duniani anajua Mwendazake alikuwa kinyume na wenzie? Kwani wapinzani wakiwemo akina Lissu ,Mbowe nk si walikuwa wanakosoa style ya Mwendazake?

Kwa hiyo kosa liko wapi hapo kusema Tulikuwa tumetofautiana njia za kukabili na ndio maana mimi nimechukua njia tofauti?
 
Huyu Mama Samia hata hakumbuki aliapa nini hata ukiuliza atakwambia jaji alinipa kilikuwa kimeandikwa akasema nisome kwa sauti hata sikumbuki kilikuwa kinasemaje labda ukamuulize jaji aliyeniapisha
Timu wavamizi wa chama mtateseka sana, CCM ina wenyewe na ndiyo hao wameshika hatamu. Malalamiko yenu pelekeni Chato kaburini
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli.

Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO-19.

View attachment 2188625
Basi kwa unafiki wa watz na huyu atamnanga mwendazzake wee! Unafanya na mtu unashindwa kumshauri tena unaitwa makamu!?? a strange continent/country. Vyombo vya kimangaribi watachokonoa hadi kinyesi
 
Huyo mama naona hana busara tu.
Kwanza anashindwa kuelewa, bila huyo Magufuli, yeye leo asingekua Rais wa Tanzania.
Sema bila Corona kumfyekelea mbali dhalim yeye angekuwa bado Makamu na angeendelea ku compromise na dhalim.
 
Wale vijana wa pale kariakoo wamenda wapi?

Hofu ya Mungu alafu anachomea watu masoko?
Tofauti ni kuwa kipindi cha Magu akipotea mtu kapotezwa na Magu,sasa hv akipotea ni kimya kimya
 
Pikipiki ya boxer inauzwa milion 11 siku izi, Hili ndilo taifa analiongoza mama kweli anaupiga mwingi
 
Hata Hitler wanamsigina kokote kule kwa kutolewa mfano mbaya,iwe ndani au nje ya Ujerumani.
Dhalim alikuwa mwovu na aliharibu umoja wa kitaifa na misingi ya utawala Bora, lazima kila mpenda nchi lazima akemee maovu haya yasijejirudia tena. Wacha Mama aliponye Taifa.
 
Kwahiyo ameshindwa kabisa kuzungumzia dira yake mpaka kila mara amtaje marehemu asiyeweza kujitetea? Yetu macho ....
Dira ipo kwenye ilani na vision 2025,dila gani nyingine unataka wewe?

Kwa hiyo kila Rais atakuja na dila yake au?
 
Kwa issue ya Corona kweli mama Samia alikuwa kutwa akihutubia anasema kagonjwa Kapoo!!!!

Magufuli hajawahi sema Corona haipo uongo alisema dawa haijapatikana tutumie maombi na dawa za asili zetu wenyewe sababu Tatizo kubwa huko kwenye wataalamu wanakufa na kuanguka maiti mabarabarani

Mama Samia dini hana akawa anaamini dawa za wazungu na barakoa
Magufuli akasema tusali Siku Tatu na kujifukiza na kunywa dawa ya kienjyeji ikatusaidia.Hakukuwa na lockdown wala nini

Corona Tanzania bila Mungu kuingilia kati tungekufa kama mbwa kwenye kuaga marehemu Magufuli. Ule msongamano hakuna ambaye ⁶angekuwa hai leo akiwemo mama Samia sababu hakuweko aliyechanja wala kuvaa barakoa.Hakukuwa na lockdown watu wanajazana kwenye daladala Mungu akatuepusha

Kwenye Corona tofauti ya Magufuli na mama Samia ilikuwa ya kidini kati ya mtumaini Mungu magufuli na mpagani mama Samia ambaye hakuona umuhimu wa Mungu kwenye kukabiliana na Corona na matumizi ya njia mbadala local grown mwabudu wazungu na solution zao za Corona
Mkuu yaani umesahau, watu waliokuwa wanavaa barakoa kwenye hadhara yake walivyokuwa wanadhalilishwa wakati jambo la afya ya mtu ni personal?
Hili la kusema watu fulani hawakuona umuhimu Mungu, ni kujaribu kumsemea Mungu wakati mwenyewe anatuona. Unaweza ukasema hadharani unamtanguliza Mungu lakini matendo yako ya sirini yanasema kitu kingine kabisa.
 
Yeah

Watu wanajipigia tu

Magufuli hana tofauti na, mume mwenye mke pisi kali

Anambana mkewe, anamwonea wivu kama wote,hataki aongee na wanaume wengine na hayuko. Tayari kuona anashare utamu na wana wa kitaa

Ila siku akifa, mkewe watu wanajinyofolea tu
Huu ndio mfano wa raia wa Tanzania anayefikiria kutembea na wake za watu ni sifa kwa jina la pisi kali ,nimeamini tajiri mmoja aliposema mawazo ya waafrika wengi ni ngono na pombe
 
Dhalim alikuwa mwovu na aliharibu umoja wa kitaifa na misingi ya utawala Bora, lazima kila mpenda nchi lazima akemee maovu haya yasijejirudia tena. Wacha Mama aliponye Taifa.
Umoja upi uliharibiwa?
 
Back
Top Bottom