Rais Samia, imulike Bandari ya Dar nchi inahujumiwa, kaweke Kambi pale Bandarini

Ikiwa tunaamini kila kitu anadanganywa, hata akienda huko bandari atadanganywa tu.
 
Umeongea kitu kikubwa sana, shida sio ukali na shida sio upole.
Hapondio balaa lilipo, na bahati mbaya wa kutumia akili ili mambo yaende hayupo
 
Chanzo ni nini?

Kwani awamu ipi ilijaa sera za kishenzi za kufukuza wawekezaji?

Awamu ipi tumeshuhudia wawekezaji wakitimkia kwao?

Tuanzie hapo msitake kutusahaulisha.
 
Hapo kwenye udadisi ndio ninamashaka makubwa sana.
 
Yaani rais ajue taratibu za kila kitengo kila sekta nchini,asitegemee wasaidizi,unafikiri sawasawa!?
 
Kwani tatizo ni nini haswa? Hizo meli wanazichelewesha makusudi kukaa hapo au namna gani?
 
Si tuliambiwa gati zimejengwa mpya na vifaa vya kisasa vya kupakua mizigo, imekuwaje tena!
 
Tatizo ni siasa za nchi hii zinatukwamisha…hv kwanini watanzania tusikabidhi jeshi lituongoze kwa miaka 20….hawa jamaa wamepitia mikiki mingi jeshini wana uzalendo wakupindukia hawana tamaa km za wanasiasa…halafu Putin awe baba wetu wa kiroho
 
Umemjibu vizuri sana, natumaini atakuwa amekuelewa vyema kabisa.

Samia hana mpango, na hata uwezo wa kufanya hayo anayolilia huyo mleta mada.

Hivi wale watu waliokuwa wameweka mrija kwenye bomba la mafuta kule Kigamboni walifanywa nini hadi leo?

Naona hata yule binti, mkuu wa wilaya alihamishwa toka eneo hilo!

Samia anajenga 'Oligarch' wake, usitegemee lolote jingine kutoka kwake.
 
Jinsi kamba yako inavokuruhusu ndio kadri unavokula, nikasema lakini mbona mnakula sana, mnavimbiwa, sikweli kwamba hampati kwenye maeneo yenu,mnapata, lakini jipimie,, JIPIMIENI - Rais Samia Suluhu Hassan

Mkuu bandarini nao wanajipimia,,meli zitakuwa zinapakuliwa kwa Connection
 
CCM mliponea chupu enzi za JK lakini kwa mwendo huu sijui mtapona vipi! Litakuja wimbi ambalo hamtaweza kuli manage.

Tatizo hakuna upinzani Tanzania kwa sasa. Kungekuwa na upinzani makini wanachukua nchi hii 2025.
 
[emoji437][emoji436]
 
Ila ilisaidia kwa namna flani
 
Ni wiki kadhaa zilizopita viongozi wa Bandari walikuwa Zambia waki'promote' nchi hiyo itumie bandari yao; hivyo hivyo taarifa zimechapishwa magazetini Uganda wakihimizwa kutumia bandari ya Dar.

Kwa hiyo tuseme hawa viongozi wa bandari wana'promote' bandari isiyokuwa na ufanisi wowote wa kazi? Hawa jamaa wa bandari mizunguko yao hii ni kutafuna hela tu?

Mwisho wa siku tutaambiwa yote yanayotokea bandarini yamesababishwa na Vladimir Putin, na sote tutaelewa yanakotokea matatizo yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…