Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Anaongelea mambo ya marekani kwamba hajui kwamba tayali watuhumiwa wameshikwa na wanahojiwa 🤔 huku nani ameshikwa hadi sasa hivi kwa mauaji na kupotea kwa watu 🤔Hivi bado kuna wapumbavu bado wanakaza shingo kumtetea bibi yao 🤔
 
Ni kwamba Rais wetu hatambui watu tunatofautiana 'hadhi' na umaarufu? Kifo ni kifo ndio, anataka kusema kifo cha M/kiti wa serikali ya mtaa kinaweza kupokelewa sawa na kifo cha Rais wa nchi?

Nafikiri tumuombee Rais wetu!
 
👆
MENE, MENE, TEKELI & PERESI
 
Tuondokane na CCM sasa hivi hapa!
 
Kwa hiyo, kwa mantiki hii, Chadema alitaka wafanye jambo gani baada ya kuona mauaji yamezidi na yeye Rais wa nchi pamoja na wawakilishi wa wananchi hawaoneshi kulaani, kukemea wala kuguswa na uovu huo?

Kuna kupotoshwa kwa mantiki hapa, si viongozi wa Chadema pekee wanaolaani mauaji ya kiholela na kihuni yanayofanywa na Serikali yake, bali ni sisi sote wapenda amani tunalaani sana jambo hili na tupo nyuma ya Chadema kuwaunga mkono.

Mauaji ya albino na wanaohisiwa uchawi hayawezi kuamsha hasira za waTz wote, kwa sababu wanaelewa wajibu wa kushughulikia kesi hizo ni jukumu la Serikali kikatiba.

Sasa asiingize mifano ya mauaji hayo kututoa katika msingi wa malalamiko yetu ya umma.

Hii ishu inasoma kinyume na alichokiongea, yaani badala ya Serikali kulinda watu, yenyewe ndiyo inageuka wauaji wa raia, kwa hiyo ni ishu mbili tofauti.

Kwa hotuba yake hii leo amejidhihirisha kuwa yeye ndiye kila kitu kwenye mtanziko huu.
 
Kwanini CCM hawatekwi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…