"Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”
“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024.