Mashamba Makubwa Nalima
JF-Expert Member
- Mar 19, 2024
- 4,978
- 2,411
Kauli zao hazijifichi mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kauli zao hazijifichi mkuu
Hivi kwani i mnamwita Mama na Sio Samia au Rais, mnampetpet sana hamna mama zenu nyie.
Aliyetegemea atasema tofauti akapimwe akili
Wanalipwa vizuri mkuuAnaongelea mambo ya marekani kwamba hajui kwamba tayali watuhumiwa wameshikwa na wanahojiwa 🤔 huku nani ameshikwa hadi sasa hivi kwa mauaji na kupotea kwa watu 🤔Hivi bado kuna wapumbavu bado wanakaza shingo kumtetea bibi yao 🤔
Mmoja wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kutekwa hadharani na baadae mwili kuokotwa namna Ile hakiwezi kuwa kifo cha kawaida.
Mna uhakika hayo maneno yametamkwa na Rais wa nchi?
Alikuwa anasoma au anatoa kichwani?
Ku undermine kifo cha mzee kibao shows rais anajua watekaji....na serikali yake iko responsible kwa utekaji
kwamba tukisikia watu wametekwa na kuuawa tunyamaze tu
Sasa kama haya matukio ya mauaji yanawauma mbona hawaachi kuua? Si waache basi? Wewe unaua unaumia halafu unaendelea kuua? Uchizi huo sasa."Siku kadhaa zilizopita ndugu zangu nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa wawakilishi wa baadhi ya mataifa ya nje wanaowakilisha nchi zao hapa kwetu. Nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyike na ndivyo inavyofanyika Duniani kote."
“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”
“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “
“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”
“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024
My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa tu, kutoka "drama"" mpaka "mtu mmoja tu".
PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana