Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Mtu yeyote mwenye kujua sheria anapoona tu kichwa cha thread hii, atasema sio sahihi, Rais Samia hapaswi kuingilia kati suala la mashitaka ya Mbowe ya Ugaidi kwa kuwa hapaswi kuingilia kati mhimili wa Mahakama. Ni kweli.

Lakini pia, Watanzania wengi sana wanaamini kwa dhati kwamba kesi ya uagaidi dhidi ya Mbowe ina mkono au baraka za Raisi Samia. Labda kweli.

Na wanasheria makini, watakuambia kwamba kesi ya ugaidi dhidi ya Mboewe, pamoja na kelele nyingi sana za Polisi, haina mshiko wa kisheria na kama kweli itasikilizwa kwa haki basi ni rahisi kwesi hiyo kutupwa au Mbowe na washitakiwa wenzake wote kushinda kesi.

Sasa unajiuliza, hivi ilikuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali asimshauri Rais Samia kwamba kesi kama hii dhidi ya Mbowe haitakuwa na mshindi? Kwanza inaiweka Tanzania katika darubini ya mataifa makubwa ya nje.

Pili inafanya idadi kubwa ya watu kuamini kwamba Mbowe alikamatwa kwa ajili ya makongamano ya Katiba na ugaidi ni kisingizio tu.

Tatu inaonyesha wazi kwa watu wa ndani na nje kwamba CCM wanaogopa Katiba mpya kwa kuwa wanahofia uchaguzi ukifanywa katika mazingira ya kidemokrasia CCM hawatashinda.

Nne Mbowe akifungwa kwa mashitaka kama haya ambayo yapoyapo tu itampa umaarufu zaidi ndani na nje ya nchi, atakuwa Mandela wa Tanzania.

Tano Mbowe akiachiwa Rais Samia na CCM wataonekana wanabambikia wapinzani kesi.

Sasa kama Mwanasheria Mkuu alishindwa kuona haya na kumshauri Rais Samia dhidi ya kesi ya Mbowe, nina mashaka sana na uwezo wake wa kumshauri Rais, au lengo lake la ushauri aliotoa kwa Rais Samia.

Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.

Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku, lakini pia akiliacha liendelee mahakamani, matokeo yake yoyote, ya kesi kutupwa nje, au Mbowe na wenzake kufungwa au kuachiwa huru, hayatakuwa mazuri kwake Rais Samia na chama chake CCM
 
Tatizo akitolewa washauri wake wa karibu akina Mdude wanaanza kumrushia matusi Mama, mara ooooh! utanyolewa nywele za sijuhi sehemu gani....hawa wahuni wa chadema wanakiharibu sana chama!

Ila naona kama uchomaji mabweni mashuleni umepungua baada ya Gaidi Mbowe kufungwa, huenda kuna mkono wake kama Polisi walivyodai!!?
 
Mama anaweza kuwa ana mawazo yake mazuri tuu. Hata katiba yaezekana angeiruhusu toka moyoni mwake.

Ila hakuna kitu kibaya kama CCM.

Mwanzo alipoingia alionesha mwanga w kimaelewano mana yaezekana alikua ye ndo top ila badae akasomeshwa risala na ccm kuwa wao wanataka watawalaje.

Tatizo sio raisi tatizo CCM
 
Ushauri mzuri Sana lakini Sasa Samia sio zaidi ya ccm, ccm ndio waratibu wa huu ujinga kuingilia anataka ila sukuma gang hawataki na ni kweli Hawa jamaa ni wengi na wana nguvu Sana japo mama ndiye raisin katiba inamruhusu kufanya chochote kwa hiyo kazi ni kwake
 
Basi inabidi Raisi Samia ajiulize sana kama watu wanaomzunguka wapo kwa ajili ya kumsaidia au kumharibia.
 
Washauri wake wana nguvu kuliko yeye.
 
Washauri wake wana nguvu kuliko yeye.
Yeye ndio raisi na mwenye kuamua nani awe mshauri wake. Lakini ikiwa anafanya mambo kwa kutaka aungwe mkono kugombea tena awamu inayofuata, basi imekula kwake. Raisi Samia anapaswa kufanya mambo bila kujali mambo ya kuungwa mkono na CCM kupitishwa kuwa mgombea uraisi 2025. Ukweli ni kwamba Wapinzani wanaweza kutumia U-Zanzibari wake kumshinda 2025, ikiwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki. CCM na washauri wake wanajua hilo.

Hivyo ajikatie tu tamaa kuwa mgombea wa CCM wa 2025 ili afanye mambo sio kwa kujipendekeza kwa wana CCM wenye chama upande wa bara ili wamuunge mkono kugombea kwa tiketi ya CCM 2025.

Ili awe raisi bora ni lazinma ajifungue minyororo ya kutaka kuwa mgombea uraisi 2025. Akifanya hivyo anaweza kujikuta wananchi wanamuunga mkono kuendelea kuwa rais kuliko hata hao washauri wake wa CCM ambae sidhani kama wana nia njema nae.
 
Mtu yeyote mwenye kujua sheria anapoona tu kichwa cha thread hii, atasema sio sahihi, Rais Samia hapaswi kuingilia kati suala la mashitaka ya Mbowe ya Ugaidi kwa kuwa hapaswi kuingilia kati mhimili wa Mahakama. Ni kweli...
Hoja yako iko bias sana. Assumption yako ni kesi kuondolewa au Mbowe kushinda tu. Kwa nini hauzungumzii pia uwezekano wa Mbowe kupatwa na hatia na kuhukumiwa miaka 20 jela. Rais ataonekna ni shujaa wa kuangamiza magaidi kama Mbowe. Tuache mahakama iamue, ndiyo utawala wa kisheria
 
Mwanamke hushawishiwa na hushawishika. Wakati anaingia kwenye jumba jeupe alisifiwa kwa ujio wake nadhani mnakumbuka vigelegele vya Mei mosi. Hivi vigelegele vya meimosi na maneno matamu ya kushughulikia miamala naona kama historia hivi.
 
Yeye ndio raisi na mwenye kuamua nani awe mshauri wake. Lakini ikiwa anafanya mambo kwa kutaka aungwe mkono kugombea tena awamu inayofuata, basi imekula kwake. Raisi Samia anapaswa kufanya mambo bila kujali mambo ya kuungwa mkono na CCM kupitishwa kuwa mgombea uraisi 2025. Ukweli ni kwamba Wapinzani wanaweza kutumia U-Zanzibari wake kumshinda 2025...
Kama kwa kuchukua msimamo huu ndiyo umaarufu wake utashuka na kufanya upinzani kuchukua urais 2025, nadhani hii ni habari njema kwa upinzani. Kwa nini mnalilia sasa. Subirini mpate hiyo advantage. Yaani wewe ni mpinzania lakini unataka Rais asifanye vitu vya kumwangusha 2025, hiyo ni akili kweli?
 
Hoja yako iko bias sana. Assumption yako ni kesi kuondolewa au Mbowe kushinda tu. Kwa nini hauzungumzii pia uwezekano wa Mbowe kupatwa na hatia na kuhukumiwa miaka 20 jela. Rais ataonekna ni shujaa wa kuangamiza magaidi kama Mbowe. Tuache mahakama iamue, ndiyo utawala wa kisheria
Hujasoma vizuri, na labda umesoma kichwa cha thread tu. Singeweza kukirefusha zaidi ya hapo. Ukiangalia thread yote nimesema Mbowe ashinde au ashindwe, au kesi itupwe, yote ni mbaya kwa Samia

Nisawa na kukutwa shambani kwa Mmakonde na kuambiwa ukikimbia nchale, ukichimama nchale, ukikaa nchale!
 
Mama anaweza kuwa ana mawazo yake mazuri tuu. Hata katiba yaezekana angeiruhusu toka moyoni mwake.

Ila hakuna kitu kibaya kama CCM.

Mwanzo alipoingia alionesha mwanga w kimaelewano mana yaezekana alikua ye ndo top ila badae akasomeshwa risala na ccm kuwa wao wanataka watawalaje.

Tatizo sio raisi tatizo CCM
Tatizo ni Dreva au Gari
 
Kama kwa kuchukua msimamo huu ndiyo umaarufu wake utashuka na kufanya upinzani kuchukua urais 2025, nadhani hii ni habari njema kwa upinzani. Kwa nini mnalilia sasa. Subirini mpate hiyo advantage. Yaani wewe ni mpinzania lakini unataka Rais asifanye vitu vya kumwangusha 2025, hiyo ni akili kweli?
Acha ushabiki, wewe kila kitu watu wanachoandika unaona kina ajenda ya wapinzani? Jaribu kutumia akili yako vizuri na kuona mambo nje ya box la CCM
 
Mleta mada uwe na adabu.. Raisi wa nchi kubwa kama hii hawezi kupewa ushauri wa hovyo hivi afu ukahisi ataukubali. Ni muda sasa wale mliokuwa mnaishi na kula kupitia mfuko wa Mbowe, mtafute vibarua vingine vya kuwaingizia riziki ya siku. Kulalamika na kuleta ushauri wa kijinga hakutawasaidia kitu wala kumuongezea na kumpunguzia chochote raisi Samia.
 
Mleta mada uwe na adabu.. Raisi wa nchi kubwa kama hii hawezi kupewa ushauri wa hovyo hivi afu ukahisi ataukubali.
Mimi sio raisi kwa sababu sitaki kujiingiza kwenye siasa. Umewahi kujiuliza kwa nini wewe sio hata mwenyekiti wa kijiji au foreman?
 
Back
Top Bottom