DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 949
- 1,260
Mtu yeyote mwenye kujua sheria anapoona tu kichwa cha thread hii, atasema sio sahihi, Rais Samia hapaswi kuingilia kati suala la mashitaka ya Mbowe ya Ugaidi kwa kuwa hapaswi kuingilia kati mhimili wa Mahakama. Ni kweli.
Lakini pia, Watanzania wengi sana wanaamini kwa dhati kwamba kesi ya uagaidi dhidi ya Mbowe ina mkono au baraka za Raisi Samia. Labda kweli.
Na wanasheria makini, watakuambia kwamba kesi ya ugaidi dhidi ya Mboewe, pamoja na kelele nyingi sana za Polisi, haina mshiko wa kisheria na kama kweli itasikilizwa kwa haki basi ni rahisi kwesi hiyo kutupwa au Mbowe na washitakiwa wenzake wote kushinda kesi.
Sasa unajiuliza, hivi ilikuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali asimshauri Rais Samia kwamba kesi kama hii dhidi ya Mbowe haitakuwa na mshindi? Kwanza inaiweka Tanzania katika darubini ya mataifa makubwa ya nje.
Pili inafanya idadi kubwa ya watu kuamini kwamba Mbowe alikamatwa kwa ajili ya makongamano ya Katiba na ugaidi ni kisingizio tu.
Tatu inaonyesha wazi kwa watu wa ndani na nje kwamba CCM wanaogopa Katiba mpya kwa kuwa wanahofia uchaguzi ukifanywa katika mazingira ya kidemokrasia CCM hawatashinda.
Nne Mbowe akifungwa kwa mashitaka kama haya ambayo yapoyapo tu itampa umaarufu zaidi ndani na nje ya nchi, atakuwa Mandela wa Tanzania.
Tano Mbowe akiachiwa Rais Samia na CCM wataonekana wanabambikia wapinzani kesi.
Sasa kama Mwanasheria Mkuu alishindwa kuona haya na kumshauri Rais Samia dhidi ya kesi ya Mbowe, nina mashaka sana na uwezo wake wa kumshauri Rais, au lengo lake la ushauri aliotoa kwa Rais Samia.
Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.
Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku, lakini pia akiliacha liendelee mahakamani, matokeo yake yoyote, ya kesi kutupwa nje, au Mbowe na wenzake kufungwa au kuachiwa huru, hayatakuwa mazuri kwake Rais Samia na chama chake CCM
Una mshauri Rais aingilie mhimili wa Mahakama ili mseme Mahakama zetu sio huru? Mbowe akiachiwa kwa order ya Rais hawezi kuwa huru sababu Mahakama ndio inayotakiwa kuthibitishia umma kwamba hakutenda kosa.
Mimi naona Selikari inataka kumlipa Mbowe fidia kwa uharibifu wa mali zake lakini wakaona njia nyepesi ni hii wampe kesi ashinde afungue kesi ya kudai fidia wamlipe mabilion.