Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Una mshauri Rais aingilie mhimili wa Mahakama ili mseme Mahakama zetu sio huru? Mbowe akiachiwa kwa order ya Rais hawezi kuwa huru sababu Mahakama ndio inayotakiwa kuthibitishia umma kwamba hakutenda kosa.

Mimi naona Selikari inataka kumlipa Mbowe fidia kwa uharibifu wa mali zake lakini wakaona njia nyepesi ni hii wampe kesi ashinde afungue kesi ya kudai fidia wamlipe mabilion.
Actually, ungetafakari kwa makini, ungeona kwamba ushauri wangu unawanufaisha CCM na sio Chadema, na wala usingesema "ili mseme Mahakama haziko huru". Nemeona kote huko na nimeliweka katika sentensi ya kwanza kwenye thread. Unafikiri Mbowe akiachiwa kwa Raisi Samia kuna watu wa Chadema wataandamana kuwa "Mahakama zetu sio huru"?
 
Bavicha bhana!

Aingilie mahakama?

Acheni gaidi apambane mahakamani
Naweza kutumia maoni ya wana CCM hapa kujua yupi ni mpumbavu asie na uwezo wa kufikiri na kuona mbali na yupi ni mwenye busara mwenye uwezo wa kufikiri na kuona mbali. Tayari nimekata shauri juu yako.
 
Hivi kweliu kweli unadhani Mbowe alipanga ugaidi wa kuua viongozi? Huyu Raisi Samia kuna watu wanamwingiza cha kiume!

Mkuu Mbowe Ni binadamu au malaika. Mtu yeyote anayeingia kwenye Siasa huyo Ni mtu wa kuwa makini naye sana. Narudia yeyote. So please try to hide your mahaba unaonekana mpumbavu.
 
From Chadema's perspective definitely very bad advice. From CCM's perspective definitely very good advice. To a myopic CCM zealot, very bad advice. I am not on either of the two sides.

But then, the good thing about opinion is that it is free, even to those that should not be voicing theirs.

Even if it’s a free thing, still it reflects your life and says a lot about you.
 
Hawezi kuingilia moja kwa moja mpaka mahakama itoe uamuzi. Anachoweza kufanya ni kuongea tu kwamba wanasiasa waachiwe kufanya shughuli zao na mwendesha mashitaka ndiye pekee anaweza kufuta kesi. Lakini kama uamuzi wa mahakama ukitolewa ingekuwa rahisi kwa Raisi kusamahe au mbowe kuachiwa. Tatizo ni kwamba kesi za Tanzania zinachukua muda sana
Umeongea point sana, na ndio maana nikasema mtu anaejua sheria ataona kwamba si vema kuingilia kesi iliyoko Mahakamani.

Lakini kuna njia nyingi za busara na hekima kwa raisi kuingilia kesi iliyoko mahakamani, na hilo ndilo ninalomwambia Raisi Samia afanye.

Kwa mfano, suala la kusema watu wenye kesi za uhujumu uchumi mahakamani wanaweza kukubaliana na DPP, ilikuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama, lakini lilifanyika. Sembuse hili?

Kuna ugumu gani kwa Raisi Samia kusema tumefanya mkutano na watu wa upinzani na kwa maslahi ya utaifa wetu tumekubaliana kuiomba ofisi ya DPP kufuta kesi zote za kisiasa nchini ili tuanze ukurasa mpya wa uhusiano kati ya CCM na vyama vya upinzani
 
Mtu yeyote mwenye kujua sheria anapoona tu kichwa cha thread hii, atasema sio sahihi, Rais Samia hapaswi kuingilia kati suala la mashitaka ya Mbowe ya Ugaidi kwa kuwa hapaswi kuingilia kati mhimili wa Mahakama. Ni kweli.

Lakini pia, Watanzania wengi sana wanaamini kwa dhati kwamba kesi ya uagaidi dhidi ya Mbowe ina mkono au baraka za Raisi Samia. Labda kweli.

Na wanasheria makini, watakuambia kwamba kesi ya ugaidi dhidi ya Mboewe, pamoja na kelele nyingi sana za Polisi, haina mshiko wa kisheria na kama kweli itasikilizwa kwa haki basi ni rahisi kwesi hiyo kutupwa au Mbowe na washitakiwa wenzake wote kushinda kesi.

Sasa unajiuliza, hivi ilikuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali asimshauri Rais Samia kwamba kesi kama hii dhidi ya Mbowe haitakuwa na mshindi? Kwanza inaiweka Tanzania katika darubini ya mataifa makubwa ya nje.

Pili inafanya idadi kubwa ya watu kuamini kwamba Mbowe alikamatwa kwa ajili ya makongamano ya Katiba na ugaidi ni kisingizio tu.

Tatu inaonyesha wazi kwa watu wa ndani na nje kwamba CCM wanaogopa Katiba mpya kwa kuwa wanahofia uchaguzi ukifanywa katika mazingira ya kidemokrasia CCM hawatashinda.

Nne Mbowe akifungwa kwa mashitaka kama haya ambayo yapoyapo tu itampa umaarufu zaidi ndani na nje ya nchi, atakuwa Mandela wa Tanzania.

Tano Mbowe akiachiwa Rais Samia na CCM wataonekana wanabambikia wapinzani kesi.

Sasa kama Mwanasheria Mkuu alishindwa kuona haya na kumshauri Rais Samia dhidi ya kesi ya Mbowe, nina mashaka sana na uwezo wake wa kumshauri Rais, au lengo lake la ushauri aliotoa kwa Rais Samia.

Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.

Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku, lakini pia akiliacha liendelee mahakamani, matokeo yake yoyote, ya kesi kutupwa nje, au Mbowe na wenzake kufungwa au kuachiwa huru, hayatakuwa mazuri kwake Rais Samia na chama chake CCM
Rais hapaswi kuingilia mhimili wa Mahakama.

Lakini, kama kesi serikali ndiyo inashitaki, na rais ndiye kiongozi wa serikali, rais, kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashitaka, anaweza kushauri au kuagiza kesi ifutwe kama kuna sababu za msingi za kufanya hivyo.

Mathalan, rais akipata taarifa za ki intelligentsia kwamba kesi hii Mbowe am3bambikiwq bula ushahidi wala haki, na kabambikiwa na Polisi waliofikiri wanafanya anachitaka rais, wakati rais hataki hivyo, rais anaweza kuwa sawa kuagiza Mkurugenzi wa Mashitaka kufuta kesi na Polisi waliohusika wawajibishwe.

Hilo litapelekea kesi kufutwa na Mkurugenzi wa Mashitaka, bila rais kuingilia Mahakama.
 
Rais hapaswi kuingilia mhimili wa Mahakama.

Lakini, kama kesi serikali ndiyo inashitaki, na rais ndiye kiongozi wa serikali, rais, kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mashitaka, anaweza kushauri au kuagiza kesi ifutwe kama kuna sababu za msingi za kufanya hivyo.

Hilo litapelekea kesi kufutwa na Mkurugenzi wa Mashitaka, bila rais kuingilia Mahakama.
Umetoa point murua kabisa, na hicho ndicho exactly kilichokuwa akilini kwangu niliposema ni kweli Raisi hapaswi kuingilia muhimili wa Mahakama, Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama,
 
Swali nimeshauliza, sasa unatakaje?
Nataka ukisoma uwe unaelewa. Sasa wewe unaulizaje kitu ambacho tayari nimeshasema Raisi Samia akiingilia kati ni kweli anaingilia uhuru wa Mahakama? Hujaona parapgraph za mwisho?

"Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.

Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku, lakini pia akiliacha liendelee mahakamani, matokeo yake yoyote, ya kesi kutupwa nje, au Mbowe na wenzake kufungwa au kuachiwa huru, hayatakuwa mazuri kwake Rais Samia na chama chake CCM "
 
Liinsha hili lote la nini?
 
Umetoa point murua kabisa, na hicho ndicho exactly kilichokuwa akilini kwangu niliposema ni kweli Raisi hapaswi kuingilia muhimili wa Mahakama
Mpaka sasa rais kutofanya hivyo maana yake ni kwamba ama anaamini kweli Mbowe inawezekana akawa gaidi, ama anaelewa kuwa hii ni michezo ya kisiasa ila anaibariki.

Yote mawili haya ni mabaya.

La kwanza litamaanisha rais ni mjinga sana.

La pili litamaanisha rais ni muovu sana.
 
Kukamatwaa kwa Jemedari Mbowe si uggaiddi hhata kidogo.Wanaaccm wanajua kilio cha katiba ni kaabburi lao.hivyo wamekaa na kutafakari wanzie wapi, kipropagandda wametoka na Mbowe maana wanajua ushawishi mkubwa alionao. Hoja ya katiba mpya imezimwa kwa kukamatwa Mwamba hyo. Subbirinii mwone!
 
Kuna mtu nimemuuliza humu kuwa hivi kweli unadhani Mbowe ni gaidi, bila kutumia akili akajibu haraka kuwa nina mapenzi na Mbowe.

Hivi watu wanadhani Mbowe na Cjadema wakiamua kuwa magaidi watafanya ugaidi kwa nmana ambayo huyu IGP anasema wanafanya na ushahidi tunao? IGH inaonekana anaangalia sana habari za Bokoharam na anatafuta cheap popularity.

Na suala la Mama kuwa makini na maamuzi yake yanayotokana na ushauri anaopewa ni muhimu sana. Sijui ana tatizo gani hapo. NIme speculate kwamba usikute hawa waliomzunguka anawasikiliza sana ili apate kuungwa mkono kuwa mgombea wa CCM 2025. Kama ndivyo atakuwa anapotea sana.
 
Mtu yeyote mwenye kufikiri anajua hakuna ugaidi wala nini hapo, na kwamba hii njia ambayo CCM wameamua kuitumia inaweza ika-backfire big time.
 
Kuna mtu nimemuuliza humu kuwa hivi kweli unadhani Mbowe ni gaidi, bila kutumia akili akajibu haraka kuwa nina mapenzi na Mbowe.

Hivi watu wanadhani Mbowe na Cjadema wakiamua kuwa magaidi watafanya ugaidi kwa nmana ambayo huyu IGP anasema wanafanya na ushahidi tunao? IGH inaonekana anaangalia sana habari za Bokoharam na anatafuta cheap popularity.

Na suala la Mama kuwa makini na maamuzi yake yanayotokana na ushauri anaopewa ni muhimu sana. Sijui ana tatizo gani hapo. NIme speculate kwamba usikute hawa waliomzunguka anawasikiliza sana ili apate kuungwa mkono kuwa mgombea wa CCM 2025. Kama ndivyo atakuwa anapotea sana.
Kuna rapper mmoja Mmarekani anaitwa Jadakiss, alisema katika moja ya nyimbo zake:-

"If I wasn't on some shit, I'm getting on it".

Alikuwa analalamika kuhusu mambo aliyokuwa anazushiwa. Akasema kwamba, sasa, kwa sababu watu wanamzushia sana, ataanza kufanya kweli hayo anayozushiwa ili lawama anazopewa zisiwe za bure, ziwe za kweli.

Nilivyoifikiria kesi hii ya ugaidi ya Mbowe nikakukmbuka mstari huo wa Jadakiss.

Nikasema, hawa CHADEMA wanaozushiwa ugaidi, hivi wakisema sawa, mnatuzushia ugaidi, sisi si magaidi, lakini kwa sababu mnatuzushia, sasa tunaanza kufanya ugaidi kweli ili kutimiza uzushi wenu.

CHADEMA wakaanza kupiga mabomu ofisi za CCM na nchi ikaingia katika milipuko ya mabomu.

Hao wanaozusha ugaidi watafurahi kuona uzushi wao unatimia?

Maana haya mambo mengine ni kama kunuia kitu kitokee, na hata mazungumzo ya ugaidi tu yanaweza kuanza kufanya watu wafanye kweli.

Back
Top Bottom