Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Ni hapo akipata hizo taarifa za ki-intelijensia. Naamini taarifa alizonazo sasa hivi ni kwamba polisi pamoja na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka wanao ushahidi kamili kama alivyosema IGP. Hizi assumptions za kama kama kama kama hazitakiwi kuwepo tena.
 
Hivi wewe unawajua waliomzunguka Mama??

Inner circle team ya Mheshimiwa rais unaijua kweli?? I mean kuijua kwa maana ya kuijua!!
 
Pole sana na hii chuki yako, ni bure mbowe wamehifadhi tu hiyo kesi ni kiini macho vuguvugu la katiba lipungue wamtoe
 
Wafuasi wa vyama vya siasa wanafikiria utawala wa sheria ni kuwaweka ndani wale wanaowachukia tu.........

Ukitazama kwa makini utagundua kuwa wanasiasa wetu pamoja na wafuasi wao hawamaanish kile wanachokipigania bali wana ajenda zao nyuma ya kile wanachokipigania.........

Watu walioshangilia kuwa utawala wa sheria umerudi kwa kukamatwa kwa Sabaya na kuachiliwa kwa Mdude Nyangali ndio hao hao wanaotaka utawala wa sheria uvunjwe ili aachiliwe kiongozi wao.......ndio maana nasema siasa za Tanzania zimekosa weledi bali imebakia mihemko tu........

Ni ngumu sana kuwaelewa wanasiasa wa nchi hii na wafuasi wao.......
 
😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄

Eti sasa wanaanza kufanya ugaidi ili iwe kweli. Halafu wakaanza kupiga mabomu ofisi za CCM na nchi ikaingia katika milipuko ya mabomu hahahaahahaha.

Wakati wote huo vyombo vyetu madhubuti vya ulinzi na usalama vimelala?? Jemedari na amir jeshi mkuu Mheshimiwa Mama Samia kipindi hicho atakuwa wapi?? Unajua tunu za taifa la Tanzania wewe???

Amani na upendo!

Jukumu la kwanza kabisa la kiongozi yoyote wa nchi hii ni kuhakikisha amani inatamalaki na katika hilo hakuna kucheka na KIMA.

Sasa hizo hip hop zenu leteni kwenye jamii zetu muone kitakachotokea.

😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Haya ni maneno tu. CCM wameogopaje hilo suala la katiba mpya??

Ni CCM kupitia Mheshimiwa Jakaya ndio aliliweka mezani litatuliwe, wapinzani si ndio waliotoka bungeni maana walitaka vikao viendelee tu ili waendelee kula posho. Wao kuona suala linaelekea kumalizika wakaona mchakato wauharibu. Halafu Leo eti CCM wanaogopa katiba mpya
 
Ni kweli kwamba fedha zilitumika nyingi , sasa si walimalizie basi? haya malumbano ya nini, kukamatwa kamatwa na mengineyo... wamalizie kilichio baki, kiwe kibaya au kizuri- na tuone mwisho wake. Haya ya kupiga hela, pia ni maneno tu...cha msingi, Katiba iliyokwama ikwamuliwe na tuendelee na mambo mengine.
 
Wewe unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Ni hapo akipata hizo taarifa za ki-intelijensia. Naamini taarifa alizonazo sasa hivi ni kwamba polisi pamoja na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka wanao ushahidi kamili kama alivyosema IGP. Hizi assumptions za kama kama kama kama hazitakiwi kuwepo tena.
Kachemka.

Wanaoandamana kwa sababu ya umeme ni wapi huko?

Halafu anajibu swali la Mbowe kirefu, kisha anasema hawezi kujibu swali kwa kuwa kesi iko mahakamani.

Contradiction.
 
Wanasiasa wa Tz huwa wanapambana kwa ajili ya matumbo yao na familia zao.
 
Inaonekana wazi unatumia makalio kufikiri!!!
 
Kufungwa ni kumuimarisha mwanasiasa, ingependeze Mbowe afungwe miaka 30 ili apate umaarufu Kama Nelson Mandela.
 
Acha ushabiki, wewe kila kitu watu wanachoandika unaona kina ajenda ya wapinzani? Jaribu kutumia akili yako vizuri na kuona mambo nje ya box la CCM
Ushauri mzuri sana, kama kufungwa Mbowe kutafanya wananchi wapende upinzani na atapoteza Urais chaguzi ifuatayo. Sioni kwa nini kuna kelele. Wamwache awapeleke wapinzani jela ili wapate utawala.
 
nadhani hata kwa wakati huu mali za Mbowe zote zinapaswa zizuiliwe pomja na acount zake.
lazima sheria ya Ugaidi ifuatwe kikamilifu.

Nilishangaa sana alipo fikishwa nakaona Mbowe anaruhusiwa kukumbatiana na jamaa zake!!
mahakamani lazima gaidi alindwe, nilishangaa pale kisutu inakuwaje Gaidi anapewa nafasi ya kukubatiana na watu mahakamani?!! hili halipaswi kujitokeza. ni muhimu vyombo vyetu vyote vikajifunza kutoka mataifa mengine namna ya kudili na watuhumiwa wa Ugaidi.
kamwe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visikubali kuhadaiwa au kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na mawakili au viongozi wa chadema, lazima sheria ifuatwe kikamilifu kama ilivyo kuwa inafuatwa kwa washitakiwa wengine.
nilishangaa kuwaona watuhumiwa wenzake wa Ugaidi wamefungwa pingu huku Mbowe akiwa hajafungwa pingu, sijafahamu kwa nn,!! kama hakuna ulazima basi wote wasifungwe pingu, sio baadhi wanafungwa wengine hawafungwi!!!
 
Serikali inavyanzo kuliko hili pumba lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…