Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
May be! but unaposhindwa kujibu hoja kwa mantiki ! inafikirisha.
Kwa mtazamo wako ni kitu rahisi sana kwasababu ni copy and paste na ndiyo maana nakueleza jaribu kuangalia mazingira ya suala zima h kwanza. Kuna tofauti ya Federation ya US, Canada, Nigeria, India hata kama ukiangalia kwa haraka unaona inafanana. Nilifundishwa darsa la sita ''attention to detail''
Mzee Warioba, Mzee Salim Ahmed, na Maprofesa wa katiba walioma namna fedeal system inafanya kazi
Walichokiona ni tofauti na mazingira tuliyo nayo.
Mfumo wa Nigeria una states 26 unawezaje kufananisha na Tanzania yenye Tanganyika kubwa na Zanzibar?
Nyerere alipofanya Union waliangalia mazingira ya reservations kwa Wazanzibar wakawapa semi autonomous.
Katiba ya Tanganyika ikafanywa ya JMT 1964 kukiwa na mambo 22 ambayo yaliongezeka na kufikia 36.
Mwaka 2010 katiba ya Zanzibar ikatoa mamlaka ya kuanzisha taasisi na sehemu kubwa ''KUJITOA' katika muungano isipokuwa pale tu Zanzibar inaponufaika.
Hili limeleta tatizo na ndipo timu ya Warioba ikasema lazima kuwe na serikali 3 ili ile ya Tanganyika iwe na shughuli zake na iwepo ndogo ya JMT itakayokuwa na mambo 7
Federation ya Warioba haiku copy ile ya US unayoijua au Australia kama una kaufahamu.
Hii imesema mambo 7 tu
Huku ndiko kukariri kwasababu unasoma federal ya US basi unataka ifanye kazi kwa nchi mbili ambazo moja ni ndogo sana. Tazama mbali zaidi ya urefu wa pua.
Kwa hoja yako hapo juu ,hebu fafanua haya
1. Kwanini unadhani lazima tuwe na Tanganyika Police, Zanzibar Police na Tanzania Police
Note kwasasa tuna Tanzania Police, kipi unadhani kinahitaji ili kuwe na police katika nchi mbili
Kwa taarifa pia, Zanzibar wana vikosi maalum nje ya vikosi vya ulinzi na usalama. Hivyo vinagharamiwa na SMZ japo kwa kujiaminisha ingawa indirectly ni gharama za Mtanganyika. Je kwa kuwa na vikosi maalumu kumeathiri vipi uwepo wa JWT na Police?
2. Kwanini unadhani tunahitaji JWTZ Tanganyika, JWTZ Zanzibar na JWT Tanzania?
Kukiwa na JWTZ moja kunaathiri vipi mfumo wa sasa na ule ujao?
Je Marekani kuna majeshi ya States yanayo operate na ku overlap shughuli za jeshi la federal?
3. Kuwa na kamishana wa Uhamiaji Tanganyika na kule Zanzibar halafu kuwa na Kanishana jenerali kunaongeza vipi gharama za uendeshaji?
Kwanini unadhani tunahitaji Uhamiaji Tanganyika, Uhamiaji Zanzibar na Uhamiaji Tanzani?
Kumbuka rasimu ya Warioba imeweka taasisi za washirika kwa kila nchi kitu ambacho mtu anayefikiri sawa sawa hawezi kubisha.
Taasisi zote za JMT zina mbadala Zanzibar kwa mujibu wa katika ya Zanzibar ya 2010.
Hivyo hizi za JMT ni za Tanganyika , ingawa zinakuwa abused na Wazanzibar kwa kuzitumia kwa mafao bila huduma au manufaa yoyote kwa Tanganyika. Yaani ni kama kapu la bibi . Wana abuse sana
Abuse imefikia mahali wanaleta bili za umeme za majumbani mwao zilipwe na walipa kodi wa Tanganyika
Kwa mantiki hiyo structure yetu ya federal ipo tayari inahitaji 'minor tweaking' katika maeneo machache sana
Structure ya Federal inahusu mambo 7 ambayo ni 3 tu yenye gharama kubwa 4 tayari yana wizara sasa hivi.
Kwa masingi huo Bunge la federal lina wajumbe 75 wanaojadili bascially mambo 3 na 4 ya ziada, hatuhitaji wabunge 400 kwasababu tu Tanganyika ni kubwa kama unavyodhani.
Umekaririri tu muundo wa federal lazima uwe abcd you don't try to give your brain a room to breath, to contemplate or digest information. Ndiyo maana huwezi kujibu hoja kwasababu ya acquired myopic
Hebu jibu hoja moja kwa nukta kwanza
Unaposhindwa kujibu hoja unavutika katika ''loose talk '' in lieu of cogent reasoning
Sisi wa std 7 hatuwaelewi, kwanini una ninashauri ninunue combine harvester kama settler wa Marekani wakati nina ekari 75 za shamba? Vipi kama nikitumia plough?
Natamani aliyenzisha computer angefuta button za copy and paste! I wish
[emoji3578]Tutakuwa na 3 constitutions and 3 sets of laws. Unataka hizi zote ziwe enforced na federal police? Kama ndivyo, tunahitaji federation ili iweje? Kwenye federation, mambo hayaendi hivyo. Ndiyo maana hata sasa hivi, pamoja na kwamba structure iliyopo ni ya ajabu ajabu, Zanzibar wana mahakama zao na magereza yao wenyewe, yanayoendeshwa kwa mujibu wa Katiba yao na sheria zao. Tukishakuwa na federation, Tanganyika nayo itatunga Katiba yake na sheria zake na kusimama kivyake. Ikirithi institutions zilizopo, well and good, lakini federal government itabidi iunde institutions zake yenyewe.
[emoji3578]Number of states zilizomo kwenye federation sio determinant ya governing system. Kitu muhimu ni existence of states. Ziwe mbili, tatu or hundreds of them, it doesn’t matter; each of them is independent of the others and of the federal government. Kama number of states ingekuwa kigezo cha degree of independence, basi states za Nigeria zingekuwa less independent than their counterparts in America or other bigger federated nations. That isn’t the case!
[emoji3578]JWTZ, Foreign Affairs, Immigration, BOT na institutions zingine zilizo chini ya JMT hazina complications zozote. Ugumu hapa uko wapi? Hizi zinakuwa governed na federal laws tu. Hakutakuwa na sheria yoyote ya Tanganyika au Zanzibar inayohusu hizi taasisi. Popote utakapoona installation yao, hiyo ni federal government property.
[emoji3578]Structure ya utawala wa Tanganyika lazima itabadilika. Hatuwezi kuendelea kutawaliwa na utitiri wa presidential appointees. Vinginevyo, federation itakuwa haina maana yoyote.
[emoji3578]Tukiwaondoa unelected officials na kuchaguwa viongozi huko mikoani na wilayani, hao elected officials itabidi wawe wanawajibika kwa vyombo vya uwakilishi wa wananchi kwenye maeneo yao. Hatua hii ndiyo itakayosababisha representation yetu kubadilika. Sasa hivi, RCs na DCs, kwa mfano, wanawajibika kwa Rais badala ya kuwajibika kwa wananchi wanaowaongoza. Kwenye federation, utamaduni wa kumfanya Rais kuwa ndiyo everything haupo!
[emoji3578]Si la saba wote wana uelewa mdogo. Wale waliokuwa wakisikiliza walimu wao kwa makini, hawawezi kushindwa kufuatilia hoja ambazo ni basic kama hizi.