Yes namba za kufikirika ili kujenga hoja.
Hapa pia kuna misconceptions kubwa. Draft ya Warioba ilikuwa ni road map ya structure nzima ya serikali 3
Kazi za Bunge la Katiba ilikuwa kuweka structure katika hali itakayoruhusu kutungwa sheria
Bunge lilipaswa ku test ile basic structure ya Warioba katika uhalisia wa mambo mengi
Hakuna aliyesema structure ya rasimu ilikuwa perfect lakini ilikuwa perfect kama model
Usiangalie Tanzania kwa jicho la US. House of rep ina reps 420 kule US kwa nchi yenye watu milioni 300
Jimbo la California lina watu takribani milioni 40 na uchumi mkubwa Duniani kuliko nchi nyingi Tz ikiwemo
Reps kutoka California ni 55 na senator 2. Kipi cha ajabu kwa Tz kuwa na Wabunge 45?
Tanzania ina watu milioni takribani 50 karibia sawa na California, ina Bunge lenye watu 393, ambao ni 27 pungufu ya US. Tanzania ina Wabunge wengi sana ukilinganisha na US.
Kwa kutazama structure ya US ni rahisi sana kudhani Tanzania ina uhitaji sawa na US !
Tanzania haipaswi kuwa na Wabunge 393 ni wengi sana.
Lakini pia fikiria senate ina 99 senators kipi cha ajabu kwa federal gov ya Tz kuwa na Wabunge 45 ?
Yes Bajeti ya Ulinzi na usalama, Mambo ya ndani na nje, Katiba, fedha na vyama vya siasa (7) itabaki kama ilivyo kwa maana kwamba nchi Washirika watachangia. Kuchangia haina maana ya 'raise fund' ina maana ya contribute kupitia tax
Nimekueleza kuwa kwa vyovyote vile bajeti ya Tanganyika itafidia ile ya JMT kwa ukubwa wake.
Mfano leo ni 41T na Zanzibar ni 2.5. Vyanzo vya pesa za federal ni tax kama zile zinazotumiwa kukusanya pesa za SMZ na JMT leo hii. Tofauti ipo wapi hapo?
Yes na hilo ni jambo jema kwasababu kila upande utakuwa na mzigo wake
Hadi sasa si Zanzibar wana mahakama zao, hizi za JMT zisizo na kazi Zanzibar zinapunguzaje gharama?
Well, Zanzibar wana vikosi maalum pesa wanapata wapi na kwanini hizi za JMT zisiwe za Tanganyika?
Prison kila eneo ina zake, Zanzibar wanaita mafunzo Bara wanaita magereza. Kipi kitakuwa kitu kigeni hapo?
Yes ni kweli na sisi pia tuna muungano wa ajabu unaoitwa 'pekee' duniani. Wapi serikali 2 zinaungana na kutengeneza serikali 2 moja ikiwa na Federal ndani yake? Nionyeshe nchi moja tu yenye kituko tulicho nacho
Hapo juu nimekueleza muungano wetu ni wa 'pekee' . Nionyeshe wapi duniani kuna muungano kama wetu?
Kuhusu federal yoyote inayoendeshwa kwa style ya Warioba, hapa unaangalia mambo kwa 'copy and paste '
Federal ya Nigeria ina states 36. India ina 28 states, US 5O states 26 states kwa uchache tu
Tanzania tuna nchi 2 tu , ni upungufu wa kuona unapojaribu kulinganisha Rasimu ya Warioba na nch nyingine
Kama muungano wetu wa serikali 2 ulivyo wa kipekee, hata wa federal hauwezi kuwa sawa na nchi nyingine
Una hoja nzuri sana kwamba unaangalia federal nyingine duniani, tatizo ni pale unaposhika button ya copy halafu uka paste iwe ni hoja au swali bila kuangalia subject inahusu nini? na hapa ni Tanzania na it's peculiarity
Tunarudi pale pale kwamba una copy & paste. Huwezi kulinganisha federal nyingine zenye state 26,28,36 au 50 na Tanzania yenye '' state 2''. Hizo nchi nyingine states zina mchango mkubwa kwa Federal bila kuathiri uwezo wao
Tanzania ni Tanganyika peke yake yenye uwezo, kutetereka ni kupi kwa Federal? Kwa maana kwamba Tanganyika ndiyo inabeba mzigo, mshirika wake Zanzibar yupo katika mbeleko tu anachangia ZERO anachukua zaidi
Nadhani Rasimu ya Warioba iliangalia mambo mengi sana zikiwemo Federal zingine dunia na kugundua kwamba copy and paste haiwezekani. Sisi tuna state mbili kama utaita hivyo, moja ndiyo inakusanya kodi na rasilimali , nyingine inalalamika tu kugawana!
JokaKuu