Kwanza ahsante, kuna kitu ulichoshindwa kuthibitisha, ongezeko la gharama! hujaweza kuthnitsha bali una hisia
Nimekuwekea wazi kwamba Tanganyika inabeba 100% ya gharama za kinachoitwa Tanzania
Kuna gharama gani itakayoongezeka? Kugawana gharama kunapunguza au kuongeza?
Zanzibar inasimama na taasisi zake, na Tanganyika ina zake kwa jina la Tanzania. Unapokuwa na federal government Tanganyika inaathirika vipi ikiwa sasa hivi imebeba zigo la Zanzibar yenyewe.
Nadhani umeuelewa mfumo wa federal tofauti. Marekani ina federal na states, lakini katika federal ni ndogo kuna mambo ukiachilia zile za ulinzi.
Tunapozungumzia federal kwa Tanzania tuna maana ya mambo 7 ambayo ni Ulinzi na usalama, Mambo ya ndani, mambo ya nje, Fedha, Katiba na vyama vya siasa. sehemu kubwa ni Ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje.
Iwepo mechanism ya kupata kodi za ku run federal government kutoka kwa washirika tofauti na sasa ambako ''federal' inalipiwa na Tanganyika peke yake. Weka % katika kodi za washirika kutoka pande zote
Unajaribu kukuza tu kwamba kutakuwa na mahakama kubwa ya federal, si kweli, kwasababu hata sasa mahakama kuu haifanyi kila kazi za mahakama zingine kama ilivyo US kwa circuit courts.
Kutakuwa na Bunge kubwa , nimekuonyesha kwamba wapo 393 hadi sasa , Zanzibar inapeleka wasikilizaji 80+ wengi kuliko Bunge la rasimu ya Warioba ambapo Zanzibar italeta 30 tu.
Tanganyika itapunguza mzigo wa kuwa na wasikilizaji tu kwa ajili ya ajira
Wewe unadhani kuhudumia Wabunge 80+ wa Zanzibar pale Dodoma ni nafuu kuliko Wabunge 45 wa Tanganyika katika ' federal parliament', hesabu hizi ni kutoka wapi.?
Tatizo lipo wapi? Kutunga sheria au kurithi na kufanyia marekebisho tena sehemu kubwa ni kuondoa jina Zanzibar kuna taabu gani. Taasisi zote zinazoitwa za muungano ni za Tanganyika, zinakuwa za Tanzania pale tu Zanzibar inapohitaji manufaa si kugharamia wala kuwajibika.
Swali muhimu kwako, nitajie taasisi ambayo haina mbadala Zanzibar! moja tu!
Taasisi za muungano ni kwa ajili ya ajira kwa Wazanzibar na Wazanzibar hawawajibiki wala hawajui gharama.
Bajeti yao ya 20/23 ni 2.5T hakuna mahali wameonyesha ghamara zozote za muungano! hata senti moja
Bajeti yao ni maji, elimu, afya ! gharama zingine zote zinalipwa kwa kodi za Watanganyika.
Soma bajeti yao! utaelewa kwanini Tanganyika inabeba mzigo kwa serikali 2.
Mwaka 1964 kulikuwa na katiba ya mpito ambayo ile ya Tanganyika ilifanywa ya JMT.
Kufanya tweaking haina tatizo ni kuondoa jina Zanzibar au Tanzania! period. Hakuna kitu kingine chochote
Federal government itatunga sheria si za kila jambo bali mambo ya federal.
Kwanini unadhani federal inatakiwa isimamie Tamisemi? Kwasasa Zanzibar hawajui Tamisemi, ukisikia wanazungumzia ujue kuna mafao tu, hawajui gharama zozote zile.
Tuonyeshe kwa namba gharama zitaongezeka wapi? Hajaweza unahisi tu. Gharama gani zinaongezeka na wapi?
Kwa Serikali 2, unaridhika kwamba Tanganyika ilipe kodi za kuendesha mambo yake na ya muungano hiyo ni sahihi? kwa hesabu gani.
Imefika mahali bill za umeme za Wazanzibar zinalipwa na Watanganyika, huo ndio unafuu!
Madeni ya Zanzibar yanalipwa na JMT ambayo ni Tanganyika
Tunawapa 4.5% ya pato kwajili ya kuendesha nchi yao. Piga hesababu 4.5% ya pato la Tanganyika kila mwezi
Wanapata 21% ya ajira za muungano, hawajui gharama ya hata mtumishi mmoja , ni zigo la Tanganyika
Unawaambia Watanganyika kuna unafuu!! please .
Unafuu upi kwa mchango gani ukilinganisha na Lindi, Singida, Simiyu , Tarime , Handeni au Njombe?
Tuonyeshe kwa kwa namba wa serikali 2 , wapi Zanzibar inachangia kiasi kwamba serikali 3 zitaongeza gharama.
Ikiwa Tanganyika inabeba mzigo wote wa gharama, kugawana majukumu ya federal kuongezaje gharama?
JokaKuu Pascal Mayalla