Rais Samia, jaribio lolote la kuipa Zanzibar mamlaka kamili ndilo litakuwa anguko lako

Rais Samia, jaribio lolote la kuipa Zanzibar mamlaka kamili ndilo litakuwa anguko lako

Huo ni wasi wasi usio na mashiko, na nitatoa mifano; Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji ni nchi huru tumepakana nao kwa ardhi ni mpaka upi wa hatari kuliko mwingine kwangu mimi naona ardhi ni hatari zaidi. Pili kama haya ndio matakwa yao wewe Mtanganyika unazuiaje au uhatarishi unatoka wapi (enzi zile za Cold war umepita kama wao wanataka kuurudisha Usultani sisi unatuhusu nini?) mfano mwingine COMORO ni taifa huru just nearby. Ni bora wakawa na serikali yao kamili na sisi tukawa na yetu na kama kuna haja ya ushirikiano maalum basi uwekwe kwa maslahi ya wote, tunaweza kushirikiana through EAC kwa mfano. Sio kuwaburuza. Kwa Technolojia ya sasa, makombora ya masafa marefu/mafupi ni nani alie salama ukaribu au umbali sio kigezo tena cha usalama. Kigezo kikubwa cha usalama ni kuishi na wengine kwa kuheshimiana bila kuumizana (win win situation).
Inshu sio mipata ya ardhi..inshu ni mipaka ya ardhi..muungano utadumu maisha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe jamaa umepagawa pakubwa sana Yani Zanzibar ijitenge ikiwa chini ya mzalendo Dr Husen Mwinyi?Unamjua Mwinyi vizuri?Hiyo haitayokea na chini ya Rais Samia na Mwinyi.
 
Laanatullahi Nyerere aliivamia Zanzibar Na kuuwa maelfu ya watu.na ndio akawa anaogopa kuvunjika kwa uvamizi aliouita muungano kwani angalishitakiwa
Nje ya Muungano, hakuna Zanzibar isipokuwa kuna Unguja na Pemba. Kama wanadhani sumu inaonjwa, wajaribu waone. Haitaisha miaka mitano kabla Tanganyika haijapokea wakimbizi kutoka upande huo!
 
Kuna kila dalili Zanzibar ikajitenga na kuwa nchi kamili kwa maslahi ya Viongozi wetu wa awamu hii.

Ni zaidi ya hatari endapo Zanzibar itaruhusiwa kuwa na mamlaka kamili kwa usalama wa Tanganyika!

Na hapa nisipepese macho NAONA KILA DALILI RAIS WETU WA SASA ANATAKA ZANZIBAR IWE NCHI HURU.

Kwenu Tiss.
Ndio maana yule mpemba kasema mchakato wa katiba ufukuliwe😂😂😂😂
 
Kanisa katoliki Na Padri Laanatullahi Nyerere ndiyo maneno yao hayo katika vita vyao dhidi ya uislamu Zanzibar
Chuki humtafuna nanayeihifadhi..pole sana.

Muungano utadumu maisha..atakaye jaribu kuuvunja atakuwa ni muhaini unajua adhabu ya wahaini?.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuna kila dalili Zanzibar ikajitenga na kuwa nchi kamili kwa maslahi ya Viongozi wetu wa awamu hii.

Ni zaidi ya hatari endapo Zanzibar itaruhusiwa kuwa na mamlaka kamili kwa usalama wa Tanganyika!

Na hapa nisipepese macho NAONA KILA DALILI RAIS WETU WA SASA ANATAKA ZANZIBAR IWE NCHI HURU.

Kwenu Tiss.
Kwa wakati huu wakiondoka ktk muungano, hiyo ni neema kwetu Bara. Wanakuja kuishi vijijini kwetu wakati wao ni wabaguzi! Hiyo ni sawa kabisaaa! Achana nao, waende zao. Hata hivyo wajiandae maana hatutawaruhusu tena kununua mchele wa shinyanga na nyama ya Kariakoo bila kodi. Mkaa wanaosafirisha kupeleka Oman pia tutapiga stop!
 
You must be kidding! Kumbe hata jambo rahisi nalo ni rocket science?

Hujui kwamba Muungano wa Serikali tatu maana yake:
1. Three legislative branches?
2. Three executive branches?
3. Three judiciary branches?
Yes , kwasasa Zanzibar ina vitu hivyo 3
Tanganyika ina vitu hivyo 3 kwa jina la Tanzania

Lakini Tanganyika imebeba vitu 3 vya JMT ya muungano
Gharama zitaongezeka vipi?

Tanganyika itahudumia mambo yake kama vile Zanzibar haipo
Zanzibar hadi sasa inahudumia mambo yake kama vile Tanganyika haipo

Kitakachokuwa cha ziada ni serikali kuu ya JMT itakayokuwa na mambo 7 yatakayohudumiwa na Washirika
Kwasasa Tanganyika ndiyo imebeba mzigo huo

Kama utasema Zanzibar kushiriki katika JMT kwa mambo 7 ni mzigo kwao nitakubaliana nawe ! Tofauti na hapo muungano ukivunjika leo kila upande utakuwa na mambo hayo 3 sasa gharama zinaongezeka vipi?

Kumbuka kwa sasa Tanganyika inabeba gharama zote peke yake , sasa zipi zitaongezeka?
 
Masikin wanzanzibar wanachukua kigamboni yao tutabaki wakiwa mji wa kisasa utakua zenj
 
Kanisa katoliki Na Padri Laanatullahi Nyerere ndiyo maneno yao hayo katika vita vyao dhidi ya uislamu Zanzibar
We kabila gani? Unadhani Uislamu ni wa maana kuliko kabila lako? Au unakuweka karibu na waarabu? Signs of fallacy!
 
Hayo ni maneno ya Laanatullahi aliyevamia Zanzibar Na kuuwa maelfu ya watu. Laanatullahi Nyerere kwani kablar ya kuivamia Zanzibar hiyor Unguja Na Pemba haikuweko?

Zanzibar ya Sultan na Zanzibar ya baada ya Sultan hazilinganishiki.
 
Yes , kwasasa Zanzibar ina vitu hivyo 3
Tanganyika ina vitu hivyo 3 kwa jina la Tanzania

Lakini Tanganyika imebeba vitu 3 vya JMT ya muungano
Gharama zitaongezeka vipi?

Tanganyika itahudumia mambo yake kama vile Zanzibar haipo
Zanzibar hadi sasa inahudumia mambo yake kama vile Tanganyika haipo

Kitakachokuwa cha ziada ni serikali kuu ya JMT itakayokuwa na mambo 7 yatakayohudumiwa na Washirika
Kwasasa Tanganyika ndiyo imebeba mzigo huo

Kama utasema Zanzibar kushiriki katika JMT kwa mambo 7 ni mzigo kwao nitakubaliana nawe ! Tofauti na hapo muungano ukivunjika leo kila upande utakuwa na mambo hayo 3 sasa gharama zinaongezeka vipi?

Kumbuka kwa sasa Tanganyika inabeba gharama zote peke yake , sasa zipi zitaongezeka?

Ugumu wa kuelewa uko wapi hapa? Huoni kwamba kutakuwa na three branches za federal government, three branches za Tanganyika government na three branches za Zanzibar government?
 
Ugumu wa kuelewa uko wapi hapa? Huoni kwamba kutakuwa na three branches za federal government, three branches za Tanganyika government na three branches za Zanzibar government?
Kwani sasa hivi ipoje?

Nimekuambia Zanzibar wana 3 branches tayari. Tanganyika wana 3 branches tayari, ila ya JMT imefichwa ndani ya Tanganyika. Kwa maana kwamba Tanganyika imebeba gharama za branches zake na ile ya JMT

Kukiwa na serikali 3 kutakuwa na Tanganyika itakayokuwa na branches zake na gharama zake. Zanzibar tayari wanazo zao. Ile ya JMT itachangiwa na itakuwa na majukumu machache sana ndivyo federal system inavyofanya kazi

Rasimu ya arioba ina mfano mzuri sana. Kutakuwa na Mabunge ya Tanganyika na Zanzibar ambayo yapo hadi sasa

Lile la JMT litakuwa na wajumbe 75 tu ambao ni wachache kuliko Wabunge wa Zanzibar waliopo Dodoma leo
Kama sikosei rasimu inasema 45 ni Wabunge wa Tanganyika watakaohudumiwa na Tanganyika
30 ni Wabunge wa Zanzibar watakaohudumiwa na Zanzibar. Kwasasa hao 30 ni mzigo wa Tanganyika

Tuonyeshe gharama zinaongezeka wapi?
 
Hakuna sehemu nimetaja TISS hapo mkuu, nilichosisitiza ni kwamba SHH hawezi kuuvunja muungano kivyakevyake kwa kutegemea hako ka kiti ka urais, HAWEZI.

Kuna jamaa mmoja angekuwa hai angekusimulia (mnaemuita jiwe)
Anaweza sana, na hakuna anayeweza mpinga. Hii nchi haina deep state Wala system Ina watoto wa makada kwa hiyo wanaloamua wao Lina consensus ya mafisadi wote. Kama kikwete alikua Rais kwa miaka 10 unadhani kuna wa kuzuia lolote?
 
Ujinga ni mzigo, Tanzania bara imepakana na nchi ngapi lakini hazijawahi kuwa tishio kiusalama? Kwanini kupakana na Zanzibar iwe tatizo kiusalama?! Kwamba Zanzibar ikija kuwa nchi kamili Tanganyika itakuja kuwa week kijeshi?
Andika kiswahili, week ni zile siku Saba za wiki.
 
Back
Top Bottom