Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Rais Samia amesema amri ya kuchoma vifaranga 6400 vilivyoingizwa kutoka Kenya miaka mitano iliyopita ilikuwa sio sawa.

Rais Samia kasema hawakushulikia vizuri uingizaji ule wa vifaranga maana pia vifaranga vinavyo haki ya kuishi.

Rais Samia alizungumza haya wakati akiongea na mawakili wa ukanda ya Afrika Mashariki.

"Afrika Mashariki tuna soko la pamoja ambalo linatusaidia kufanya biashara zetu, tunakubaliana kwenye mambo ya customs na taxation lakini we had a lot of NTB's na ni tariff barriers ambazo mnajitahidi kuzifanyia kazi kuziondosha.

Ni kitu kidogo tu, ni mmoja kutoka kwenda kwa mwingine. Wakati mimi sikuingia, biashara yetu na Kenya ilikuwa ngumu sana, ngumu sana. Fika vifaranga mipakani pale, makaratasi hayasomi vizuri, vimetoka wapi haisemi vizuri, kunapita vifungu vya sheria as if sheria is everything. No no no sheria hairuhusu, solution hata hatuogopi dhambi, choma hivyo vifaranga.

Tumejisahau, vifaranga pia ni viumbe vya Mungu, walikuwa na life tukachoma"


Alisema Rais Samia


View attachment 2427229
Mbona yeye kachoma vifaranga 50000
 
Yaani hadi huruma. Vifaranga Vimechomwa moto huko Moshi Juzi kati. Maboksi Kwa maboksi eti sababu Vifaranga wa Bongo wanakosa Soko. Hii Nchi Ina Utawala Binafsi au wa Majimbo? Rais alishasema isitokee Tena Bado ikatokea why? Why0?
 
Back
Top Bottom