Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Kuna namna Hayati Rais Magufuli anachafuliwa kwanini Rais Samia akiri kosa ambalo lilifanywa na Serikali ya ccm ambayo yeye mwenyewe Rais Samia kwa kipindi hicho alikuwa Makamu wa Rais au ndio tuseme bado mzimu wa Rais Magufuli unawaandama.
 
Mama kila siku anapiga kwenye mshono tu.😅😅
 
Kuna namna Hayati Rais Magufuli anachafuliwa kwanini Rais Samia akiri kosa ambalo lilifanywa na Serikali ya ccm ambayo yeye mwenyewe Rais Samia kwa kipindi hicho alikuwa Makamu wa Rais au ndio tuseme bado mzimu wa Rais Magufuli unawaandama.
Kosa la mtu mmoja unataka livae watu wote?

Hata ule uchaguzi kuna siku mama atakuja kutaja yoote🤣🤣
 
Ni sehemu na mihemuko ya JPM na madhafu yake mengine, haifanyi au haindoi kwamba hajawi kuwa na mazuri au hajawai fanya jambo zuri.
Tunapoelekea mama atakuja kueleza yafuatayo
1. Alyempiga Lissu Risasi
2. Aliyetunga kesi ya mbowe
3. Aliyefadhili wizi wa kura na kuharibu uchaguzi
4. Aliyekuwa kiongiozi wa wasiojulikana
5. Aliyeiba 2.4T

Mpaka sasa kashasema
1. Wezi wa BOT
2. Waliotunga kesi za kubambikia watu.
3. .....
 
Mama anapinga kila kitu kama CHADEMA
Hapa ni kwamba wala sio kupinga kwa nia njema, ila huu mjadala wa vifaranga unalenga kuzima mambo ya msingi yanayoendelea nchini kama mgao wa maji, umeme na gharama za maisha kupanda. Wameona kujadili mlango wa ndege na majaliwa haitoshi waongeze kingine wanachohisi kitakuwa na nguvu
 
Wataalamu waliovichoma ndio tatizo!
Labda vilibeba ugonjwa unaosambaa kirahisi na vingeachwa vikae ata one hour tuu labda Nchi yetu ingekumbwa na ugonjwa Hatari sana....Nchi kama Australia wao pia hufanya hivyo..Namshauri RAIS afanye Kazi yake jinsi katiba inavyomwelekeza, sio Busara kuwakosoa watendaji/wataalamu waliopatiwa dhamani katika sekta Mbali mbali kwenye Taifa hili tena mbele za wageni...That goes to all political leaders, Kazi yenu ni kusimamia Sheria na kanuni na kupiga siasa katika wakati muafaka..mkiona kuna mtendaji kavunja Sheria, mnayo dhamana ya kumwajibisha kwa kufuata utaratibu na kanuni zilizopo kisheria... acheni tabia ya ku-politicize issues Bila kutumia taarifa na ushauri halali kutoka kwenye Taasisi zenye Authority. Imagine duniani kote viongozi wakuu wa Nchi wanapopata international audience wanaongelea global issues na jinsi ya kuifanya Dunia kuwa sehemu salama kwa kuishi ,sio kuongelea petty issues....Hilo suala la vifaranga ilitakiwa aandaliwe press conference yenye coverage kubwa VET au afisa mifugo wa wilaya aliongelee kitaalamu with enough facts ili ku-counter attack any diplomatic conflict na Hilo suala ndio lingekuwa limeisha..But kwasababu viongozi wetu ni Misters & Mrs know everything wanapenda kujibia kila issue...ndio maana sometimes wanajikuta kwenye firing line za wananchi wenye hasira Kali just because issues zote inaelekea wenyewe ndio wanaozijua na kuzifanya .... its about time wawaache wataalamu wetu watoe ufafanuzi wa kitaalamu, wao wake nyuma na kuongelea maswala ya jumla na kisera..sio waziri au RAIS unajifanya unajua tatizo na solution wakati hujui lolote zaidi ya kukusanya political mileage.
 
Wakati wa uongozi wa shujaa!! Haambiliki!!
Sawa alikuwa haambiliki kama yeye hivi sasa lakini angetafuta njia nyingine ya kupambana naye kuliko hivi hadharani tena kwenye jukwaa la kimataifa naona hata yeye hashauriki kwa sababu hili hakustahili kulisema hadharani ila kwa kuwa anapambana na Hayati Magufuli haoni shida kwake ni sawa tu.
 
Huyu mama anataka kuficha weakness zake kupitia makosa ya JPM.
 
Vitu vingine ni kumchafua Magufuli haonekane hakufaa, Magufuli anausika nanini kuhusu kuchoma vifaranga? hayo Mambo angeulizwa Waziri wa mifugo na maafisa mifugo, wakati vifaranga vinachomwa yeye alikuwa Ikuru na kushughuli zake pengine alikuja kupata tarifa mambo yameisha tokea,Mimi mwenyewe iliisha wahi kunitokea,nilikamatwa na Mabwana Hafyia wa Samaki,nikaombwa kibali cha kusafirisha hao Samaki,nikawaonyesha kumbe hawana tatizo na kibali wao wanataka rushwa,wakataka ela nyingi nikawakatalia waliona nawakatalia,wakachukua wale Samaki wakawamwagia mafuta ya taa na kuwateketeza eti walikuwa hawafahi kuliwa,hivi kweli ninaweza kutoka hapo ninasema Magufuli ameteketeza Samaki wangu.Mengine tunawatwisha mizigo Rais ambayo hawayafahamu.
 
Kwanini hakuwajibika kwa kujiuzulu kuonyesha hakubaliani na yanayofanywa na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…