Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Hii nadharia unayosema ndio imetufikisha hapa leo watoto wa kike kupata mimba mapema na kuzidi kuharibikiwa.Kwasababu wasichana wapo more vulnerable kuliko wanaume.
Msichana akipata elimu jamii nzima inaendelea.
Nitaeleza kidogo.
Kwa mfano, ikiwa watoto wote wawili wa kike na kiume wakaishia form 4, unadhan yupi ataathirika kwa haraka zaid kuliko mwingine? Hasa linapokuja suala la uzazi? Na hivyo kuongezea serikal mzigo wa kulea watoto mapema.
Lakini pia, kazi na ajira nyingi semi skilled zinambeba zaid mtoto wa kiume kuliko wa kike.
Ufundi, Udereva, Umachinga, Ubaharia, uvuvi, kufuga, kulima, misitu nk
Nadhani uamuzi huo ni wa busara sana.
Unajua kwamba kusema kumuendeleza mwanamke tafsiri yake ni kumtoa nyumbani na awe nje ya nyumba kwa zaidi ya masaa 12 ya siku. Yaani kutwa nzima. Umeona impact yake kwenye malezi ya watoto miaka hii?
Na je, serikali kama imeshindwa kuwapa ajira hawa wakiume waliopo je hao wa kike itaweza kuwapa ajira wote?!
Nadhani tunaishi kinadharia sana ila uhalisia wetu haupo sawa na hizi nadharia.
Tunahitaji familia imara. Watanzania kwa wingi wetu idadi kubwa ni masikini tupata tu hela za kubadili mboga na mavazi ila kiuhalisia ni masikini. Hata hawa wenye pesa je wanazipata kwa miradi au madili ya wizi wizi?
Nadhani tufike wakati tutambue tupo eneo gani kijamii na tunatakiwa kuishi kwa mfumo gani.
Eneo la familia hizi mbinu za Women empowerment hazishabihiani kabisa na mazingira yetu na ndio maana zinazalisha migogoro zaidi badala ya suluhisho. Jambo likiwa ni suluhisho huwa lina zaa matunda mazuri ila kama sio suluhisho litazaa tatizo kubwa zaidi. Kwa kifupi tunatibu maralia kwa kutumia Dawa za TB mwisho wa siku maralia haiponi na dawa za TB zinachosha mwili.