Rais Samia, kama walivyofanya Malawi na sasa Kenya, nasi kama vijana wa Tanzania, tupo tayari kwenda Israel kuwa vibarua

Rais Samia, kama walivyofanya Malawi na sasa Kenya, nasi kama vijana wa Tanzania, tupo tayari kwenda Israel kuwa vibarua

Ni ukweli kabisa, mimi nikiwa tayari kabisa kwenda Israel na kuwa kibarua kwenye mashamba ya Wayahudi hao wa mashariki ya kati,

Kwa mshahara wa 4M!! Usinitanie bhana!

Nawasemea vijana lukuki wa Kitanzania na ambapo wengine wakiwa maofisini na wengine mitaani wakihangaika kutafuta ajira wasipate, huku walioko maofsini wakilipwa mshahara kidogo ukilinganisha na mshahara wa kibarua wa mashamba huko Israeli

Mh Rais, unapoamua maamzi haya, ni kutusaidia sisi vijana ili kujipatia kipato, kujijenga kiuchumi na kuijenga nchi yetu.

Kama tunakopa na ili tufanye maendeleo, maana yake ni kwamba, bado tupo chini ya mataifa hayo tunayoyakopa na hatujajikomboa kutoka katika hali ya umasikini.

Kwa mantiki hiyo, unapotoa fursa hiyo kwa vijana, ni umetoa nafasi ya wao kujikomboa kutoka kwenye umasikini wao.

Huo sio utumwa, maana hata hapa nchini, kazi za kufanya kazi ya mashamba ya watu ipo na inaendelea.

Kama kufanya kazi kwenye mashamba ya wayahudi hao ni utumwa, vipi wale wanaofanya kazi hizo hizo kwenye mashamba ya waswahili wenzao na kwa malipo kidogo!

Binafii, nipo tayari hata ikiwa ni leo usiku.
Labda mkafanywe mashoga
 
Badala ya kumuomba Rais aharakishe zoezi la Upatikanaji wa Katiba Mpya pamoja na kurekebisha sheria zote za nchi hii ili kuweka Mazingira mazuri na wezeshi ya watu kuweza kujiajiri wao wenyewe au kuajiriwa kwa urahisi hapa hapa nchini, wewe unaomba kupelekwa utumwani Israel.!! Akili mbovu za namna hii zitaondoka lini kwa vijana wa Tz???? Hakuna nchi hata moja hapa duniani ambayo imeendelea kwa bahati mbaya.
Mapinduzi ya Fikra yanahitajika sana kwa Watanzania ili tutoke hapa tulipokwama.
Kwa makasiriko haya hapa, ungelikuwa umeyafanya kipindi Chadema wanashinikiza maandamano, tungekuwa tumeshapata dai lako mkuu,

Kwa sasa, vijana tunamuomba Rais wetu atoe kibari twende Israel, mengine fanya wewe
 
Kama tunakopa na ili tufanye maendeleo, maana yake ni kwamba, bado tupo chini ya mataifa hayo tunayoyakopa na hatujajikomboa kutoka katika hali ya umasikini.
Mkuu 'Nsanzagee', mimi sikulaumu wewe kwa maoni yako uliyo wasilisha kwenye mada yako; pamoja na kwamba msingi wa mada hiyo sikubaliani nao.

Ninachokubaliana nawe ni maoni kama hili uliloliweka katika mstari nilionukuu hapo juu.

Sasa naomba nikuulize swali: wewe unadhani "tutajikomboa" lini, na kwa njia zipi? Kwenda kwako kufanya kazi Israel kwa muda na kupata utakachopata huko, inawezekana ikawa nafuu kidogo kwako kwa muda, lakini utakaporudi hapa utaikuta hali ni hiyo hiyo kama ulivyo iacha kama hatutachukua hatua zaidi ya hizi tunazofanya sasa za kutegemea kuwapeleka nguvu kazi wetu huko nje.

Hivi Israel kuna kipi hasa cha ziada tusichoweza kuwa nacho sisi hapa?
Ardhi nzuri sana tunayo. Maji yapo chungu nzima.

Ni nini hasa kinachokosekana hadi kilimo chetu kisiwe na manufaa kuweza kutusaidia kama kinavyo wasaidia hao Israel?

Naona hapo juu tayari uazungumzia ukosefu wa mitaji ya kuwekeza; na pengine utaalam wa kilimo kama walivyo vavyo Israel.
Kwa nini sis tusiwe navyo hivi? Tuna chuo kikuu cha Sokoine, na vyuo mbalimbali nchini, na kila mwaka watu wanahitimu huko. Hiyo elimu ya kilimo ya Israel wao wanaipata wapi?

Ngoja nimalize: Mazao yanayozalishwa kwa mazingira kama yalivyo Israel, yasingeweza kamwe kushindana na mazao yetu katika soko; kwa sababu mazao yetu yangekuwa na bei nafuu zaidi ya hiyo wanayouzia Israel

Kwa hiyo, sikulalamikii wewe katika msimamo wako wa kutaka kwenda kuwa kibarua. Ninawalalamikia hao wanaokunyima fursa ili usijitoe kwenda kuwa manamba. Na ninakuomba hili ulifikiri vizuri hata wakati ukiwa huko Israel.
 
Sio Kila kitu umwombe rais, tafuta passport, nenda ubalozi wa Israel au wasiliana nao ubalozi wa Israel nchini Kenya , ukatafute maisha. Nilikuwa na namba yao ya WhatsApp bahati mbaya nimepoteza wako sharp kujibu sms.
 
Kwa hiyo, sikulalamikii wewe katika msimamo wako wa kutaka kwenda kuwa kibarua. Ninawalalamikia hao wanaokunyima fursa ili usijitoe kwenda kuwa manamba. Na ninakuomba hili ulifikiri vizuri hata wakati ukiwa huko Israel
😢😢

Mkuu, yatosha tu, sasa tufanyeje?
 
Kwa sasa, vijana tunamuomba Rais wetu atoe kibari twende Israel, mengine fanya wewe
Ahaaa, kumbe tatizo lako lipo hapa? Wewe ni CHAWA?

HOVYO KABISA! Kila kitu ni Rais kafanya hivi, Rais afanye hivi; hata ukitaka kwenda msalani unaanza kumfikiria Rais kama atakuruhusu. Hili limekuwa taifa la kipumbavu kwelikweli.
 
Mama yako
Siku zote mtu mwenye akili kisoda na aliyepigwa kimaisha, hatuhangaiki kuwajua watu hao,

Mfano mdogo tu, mama yangu kaingiaje hapo mkuu

Mimi sikulaumu na hutoona tusi lolote kutoka kwangu, halafu tuone utavuna pesa kiasi gani kwa kutukana watu
 
Ahaaa, kumbe tatizo lako lipo hapa? Wewe ni CHAWA?

HOVYO KABISA! Kila kitu ni Rais kafanya hivi, Rais afanye hivi; hata ukitaka kwenda msalani unaanza kumfikiria Rais kama atakuruhusu. Hili limekuwa taifa la kipumbavu kwelikweli.
Hizi ni fikra zako, naziheshimu pia
 
Hapana kwa kweli, unajua Tz huwa tunajivuta sana kwa kila kitu, aidha kiwe kibaya au kizuri kwa manufaa yetu lakini bado huwa tunasita sana kufikia maamuzi
Yaani tunaweza kukaa hata miaka 30 kwa kukataa maslahi mapana.
Ila kwa hili acha serikali ijivunge tu na kutopeleka wala kuomba hizo kazi

Ikumbukwe Waisrael waliwaendea kwa mbwembwe ndugu zao Falasha wa Ethiopia na kusema hawa ndio damu yetu kabisa
Sasa kama hao ndugu zao waliwatoa vizazi ili wasizae na wanaume wa kiisrael je nyie wamakonde mtaachwa salama si watang'oa kabisa hizo balls?

Naona kwa hili serikali ijivute tu na kuwaza kwa miaka 20 kama linavyowaza dual citizenship
Maana kwa kujivuta hawajambo, wanapita marais ila akili zile zile
 
Siku zote mtu mwenye akili kisoda na aliyepigwa kimaisha, hatuhangaiki kuwajua watu hao,

Mfano mdogo tu, mama yangu kaingiaje hapo mkuu

Mimi sikulaumu na hutoona tusi lolote kutoka kwangu, halafu tuone utavuna pesa kiasi gani kwa kutukana watu
Hayo maneno lamsimuloe baba yako
 
Mwambie shangazi yako
Punguza jaziba kwa kuwa na muda wa kupumzika, hata uso wako utachangamka, hata huko kukunjamana uso wako, utatoka na utakuwa sawa

La sivyo, watakuzika mapema mno
 
Back
Top Bottom