Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

CCM ni uozo kuanzia kichwa hadi kwenye unyayo
 
Mifumo ipi mkuu? Kwamba raisi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi mtu alietafuna fedha za umma na kuagiza vyombo vya ulinzi vimkamate na kumhoji na ikiwezekana afikishwe mahakamani nayo inahitaji kubadilisha mfumo?
Muulize ni mfumo gani uliomfikisha mahakamani sabaya na kumkamata na kunyimwa dhamana?
 
Dah! Umejibu vizuri Sana sijui nani kawadanganya CCM pekee ndio tatizo
Kweli mkuu. Kumuamini mwanasiasa yoyote wa chama chochote ni sawa sawa na kuamini kuwa jogoo anaweza kunyonyesha.
 
Hii kazi unayotupa sio yetu kabisa, hao wenye madaraka na mamlaka ndio wanaobadilisha mfumo na mara zote wamejikinga kuzuia waendelee na mambo yao. Raisi atambue mamlaka na madaraka yake kwanza, na achukue hatua kama amiri jeshi yeye ndie katiba imempa kinga hao waliopiga pesa anawajua sasa anaweza hata kuamuru wapigwe risasi hadharani.
Sie huku ni kujaza thread JF, hakuna kitu mifumo wala nini kama chawa na yeye katengeneza wake, kama kusifiwa we shahidi sasa ajipime mwenyewe na ajichukulie hatua.
 
Mifumo ipi mkuu? Kwamba raisi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi mtu alietafuna fedha za umma na kuagiza vyombo vya ulinzi vimkamate na kumhoji na ikiwezekana afikishwe mahakamani nayo inahitaji kubadilisha mfumo?
Hapo ndo ipo shida ya mfumo, rais akimsimamisha au kumfuta mtu kazi (sijui kama lipo kisheria) ila wanaoenda kumkamata, kumhoji, na kumshitaki kama hawataki ashindwe basi atashinda na atalipwa pamoja na mafidia mengi atakayogawa kwa wanamfumo waliofuma ushindi. Usipoelewa hivi shauri yako ila ndo mfumo wenyewe sasa.
 
Hatukamati watu kwa tuhuma tuu, sasa ni mpaka uthibitisho!.

P
Itathibitishwaje ikiwa raisi mwenyewe anashauri kuwa watuhumiwa washushwe tu vyeo au wahamishwe ofisi na kupelekwa ofisi nyingine, badala ya kuagiza wasimamishwe wachunguzwe na ikithibitika kuhusika basi hatua zichukuliwe juu yao!

Unategemea kumshusha cheo au kumuamisha ofisi mtuhumiwa ndio njia nzuri ya ku deal nae?

Mkuu soma post yangu namba #29 nimelielezea vizuri.
 
Wezi wenyewe jamii ya kina joka la makengeza utaweza kuwakuta na hatia kweli?
 
Hata wakikutwa na hatia adhabu ya aliyeiba bilioni alipe milioni mbili au jela miaka miwili, hakuna mwenye nia ya dhati ya kupigana na uwizi wa mali ya umma nchi hii
 
Na kuvuna mabua ndio kunakofanyika kwa sasa !! Nchi hii ukiwaambia mimi sikuzowea kufukuzana fukuzana na kufokeana fokeana hapo ujue umewawashia taa ya kijani mijizi ya pesa za umma !!
Nchi imerudi katika mikono ya shamba la bibi.
 
Nimesononeka baada ya kusema hao wapigaji waondolewe sehemu zenye ulaji mwingi wapelekwe sehemu zisizona neema ili wakapate tabu kidogo

Kwanini wasishitakiwe?
 
Acha kuleta porojo. Yaaani unataka ushahidi gani hata kama kuna premafacie evidence?
Hata mimi nimemshangaa anko Pascal Mayalla . Yani anaridhika raisi kushauri watuhumiwa wabadilishiwe ofisi, badala ya kusimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zao, na ikithibitika kuwa walihusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Muulize ni mfumo gani uliomfikisha mahakamani sabaya na kumkamata na kunyimwa dhamana?
Ndio kuna sehemu nimemjibu kwamba vipi kuhusu Sabaya? Mpaka sasa bado hajarudi kujibu.
 
Nimesononeka baada ya kusema hao wapigaji waondolewe sehemu zenye ulaji mwingi wapelekwe sehemu zisizona neema ili wakapate tabu kidogo

Kwanini wasishitakiwe?
Imagine unamtoa mwizi kwenye nyumba kubwa na kumpeleka kwenye nyumba ndogo ukihisi unamkomoa, wakati zile pesa alizoiba bado anazo ndani, na mwisho wa mwezi anaendelea kupokea mshahara kutoka kwa aliowaibia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…