Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Hapana Mkuu.

Mabadiliko popote Duniani yanafanywa na mtu mmoja mwenye roho ya kutaka mabadiliko ya kitu Fulani. Kundi la watu Haliwezi kufanya mabadiliko.

JPM alifanya mabadiliko makubwa sana Kwa muda mfupi.
Mpaka Sasa JPM ndiye aliyewafumbua macho watanzania kujua kuwa Kuna wizi kila mahali mpaka kwenye vyama vya siasa .
JPM alithubutu sana . Ukweli ni kwamba kama angefanikiwa kukaa madarakani Kwa miaka 20 , hii nchi inekua na mabadiliko makubwa sana.

Kagame angekegea Rwanda ingekua kama Burundi lakini mtu mmoja amesinamia kile alichokiamini.

Yesu , Muhamadi ,Musa walita Mageuzi Kwa maelekezo yao bila kubagain na mtu.

Mtu mmoja inaweza kupatikana hata mwezi ujao Kwa Tamko la mtu mmoja TU,Dr. Samia Suluhu Hassan.
Mtu mmoja TU anaweza akavuna Baraza la Mawaziri na kutengua mabalozi wote na maDC na maRC Kwa usiku mmoja.
Mungu anapotoa Kiongozi au Mtawala wa nchi basi ujue anadimama badala ya Mungu katika kutenda haki .
Ni mtu mmoja TU.
Acha uwongo wa kutumia jina la JPM vibaya.
Wizi ulikuwepo hata kabla. Na waTanzania walijua. Tena yeye aliiba 1.5T ambayo haikuwahi kuibwa na syndicate yoyote.
Zaidi JPM angetaka kuleta mabadiliko angeanzia kwenye kanuni, taratibu na sheria. Alishindwa. Alichoweza ni kujiona Bora na kutaka kujilimbikizia Madaraka. Yaani angeendelea kubaki pale Kila kitu nchi kingeitwa kwa jina lake. Hadi ubini wako ungebadilika.
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote!
Sasa hivi yupo panapomstahiki!
Waliomvimbisha kichwa wanampigia mwingine makofi!
 
Hii kazi unayotupa sio yetu kabisa, hao wenye madaraka na mamlaka ndio wanaobadilisha mfumo na mara zote wamejikinga kuzuia waendelee na mambo yao. Raisi atambue mamlaka na madaraka yake kwanza, na achukue hatua kama amiri jeshi yeye ndie katiba imempa kinga hao waliopiga pesa anawajua sasa anaweza hata kuamuru wapigwe risasi hadharani.
Sie huku ni kujaza thread JF, hakuna kitu mifumo wala nini kama chawa na yeye katengeneza wake, kama kusifiwa we shahidi sasa ajipime mwenyewe na ajichukulie hatua.
Rudi kasome kuanzia uraia, civics, GS, DS, hadi political science.
Wenye nguvu ni wananchi ndani ya nchi Wao ndo wanaamua waongozweje!
 
Hajalalamika ametoa maagizo! Tusubiri utekelezaji kwa wasaidizi wake!

Sema rais kuna sehem hata mimi sijamuelewa anasemaje mtu aliyeharibu ahamishwe? Aende wap wanapopendwa kuibiwa? Serikal yote ni ya watz na kodi zote ni zetu iwe pemba au chato!
Kuna alosema warudishe walichoiba au wapelekwe mahakaman!yaan sijaelewa akirudisha anakua siyo mwizi ila alijikopesha au? Manake utakua mchezo acha niibe ntarudisha nikishtukiwa
Hili la kushauri watuhumiwa wahamishwe au kushushwa tu cheo bila kusimamishwa na kuchunguzwa ndio tatizo kubwa tunalolijadili hapa mkuu.
 
Nafikiri wengi tulisema JPM alikuwa mukali sana tukatamani Rais anaendesha nchi kwa sheria za nchi. Sheria hazisemi rais akiona mtu kaiba, basi amutaje hadharani alafu aamulishe afungwe jela. Wa Tz tunapenda kubembelezana ndo ustarabu wetu.
Kwahiyo mkuu sheria hazimruhusu raisi kumsimamisha mtuhumiwa na kuagiza uchunguzi dhidi yake?
 
Na hutoweza kuwa mada kwa akili yako iliyojaa chuki na husda, kisa Samia mzanzibari amekua hana jema kwenu
Ona sasa akili za kushikiwa hizi, umeshaingiza habari za uzanzibari.

Tunajadili mambo ya kitaifa wewe unaleta habari za uzanzibari hapa! Bure kabisa.

Kiongozi akizingua lazima apopolewe haijalishi ni mzanzibari au mtanganyika, wote hao ni watanzania.
Magufuli tumempopoa sana kipindi chake, nae alikua mzanzibari? Ebo!
 
Hapo rais hajatumia cheo chake kuwawajibisha wakosaji! Means amewaachia na kuwalinda waendelee kuliingizia taifa hasara! Hiyo ndio shida ya ukada
 
Inawezekana jamaa ni mmoja wa waliopiga hela serikalini, ndomaana alipoona tunajadili swala hili kakimbilia kujificha kwenye kimvuli cha uzanzibar.
 
Hapo rais hajatumia cheo chake kuwawajibisha wakosaji! Means amewaachia na kuwalinda waendelee kuliingizia taifa hasara! Hiyo ndio shida ya ukada
Ashasema wezi wawe wanahamishwa ofisi au kushushwa vyeo 😄😄
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa Rais kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake Rais eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anayeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali. Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Rais na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Mtasema dikteta mnataka katiba mpya asi abuse power ...... watanzania hatujui tunachokitaka
 
Screenshot_20230330_094039_Twitter~2.jpg
 
Mtasema dikteta mnataka katiba mpya asi abuse power ...... watanzania hatujui tunachokitaka
Kuagiza watuhumiwa wasimamishwe ili kupisha uchunguzi dhidi yao nao huo unaona tutaita udikteta?

Sasa raisi anaeogopa kuchukua hatua kwa masilahi ya umma na taifa eti kwa sababu ataitwa dikteta ni raisi gani huyo?
 
Tushaita mmoja hivyo tukasema ana dhalilisha watu hao watu wana watoto nyumbani..... Huyu mama shida yake anataka kuwapendeza watu wa upande flani anasahau walio mpa kura ni watu wa upande mwingine........ ukiangalia wanaolalamika sana sa hizi ni watu wa upande wake mwenyewe
 
Back
Top Bottom