Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Acha uwongo wa kutumia jina la JPM vibaya.
Wizi ulikuwepo hata kabla. Na waTanzania walijua. Tena yeye aliiba 1.5T ambayo haikuwahi kuibwa na syndicate yoyote.
Zaidi JPM angetaka kuleta mabadiliko angeanzia kwenye kanuni, taratibu na sheria. Alishindwa. Alichoweza ni kujiona Bora na kutaka kujilimbikizia Madaraka. Yaani angeendelea kubaki pale Kila kitu nchi kingeitwa kwa jina lake. Hadi ubini wako ungebadilika.
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote!
Sasa hivi yupo panapomstahiki!
Waliomvimbisha kichwa wanampigia mwingine makofi!
 
Rudi kasome kuanzia uraia, civics, GS, DS, hadi political science.
Wenye nguvu ni wananchi ndani ya nchi Wao ndo wanaamua waongozweje!
 
Hili la kushauri watuhumiwa wahamishwe au kushushwa tu cheo bila kusimamishwa na kuchunguzwa ndio tatizo kubwa tunalolijadili hapa mkuu.
 
Nafikiri wengi tulisema JPM alikuwa mukali sana tukatamani Rais anaendesha nchi kwa sheria za nchi. Sheria hazisemi rais akiona mtu kaiba, basi amutaje hadharani alafu aamulishe afungwe jela. Wa Tz tunapenda kubembelezana ndo ustarabu wetu.
Kwahiyo mkuu sheria hazimruhusu raisi kumsimamisha mtuhumiwa na kuagiza uchunguzi dhidi yake?
 
Na hutoweza kuwa mada kwa akili yako iliyojaa chuki na husda, kisa Samia mzanzibari amekua hana jema kwenu
Ona sasa akili za kushikiwa hizi, umeshaingiza habari za uzanzibari.

Tunajadili mambo ya kitaifa wewe unaleta habari za uzanzibari hapa! Bure kabisa.

Kiongozi akizingua lazima apopolewe haijalishi ni mzanzibari au mtanganyika, wote hao ni watanzania.
Magufuli tumempopoa sana kipindi chake, nae alikua mzanzibari? Ebo!
 
Hapo rais hajatumia cheo chake kuwawajibisha wakosaji! Means amewaachia na kuwalinda waendelee kuliingizia taifa hasara! Hiyo ndio shida ya ukada
 
Inawezekana jamaa ni mmoja wa waliopiga hela serikalini, ndomaana alipoona tunajadili swala hili kakimbilia kujificha kwenye kimvuli cha uzanzibar.
 
Hapo rais hajatumia cheo chake kuwawajibisha wakosaji! Means amewaachia na kuwalinda waendelee kuliingizia taifa hasara! Hiyo ndio shida ya ukada
Ashasema wezi wawe wanahamishwa ofisi au kushushwa vyeo 😄😄
 
Mtasema dikteta mnataka katiba mpya asi abuse power ...... watanzania hatujui tunachokitaka
 
 
Mtasema dikteta mnataka katiba mpya asi abuse power ...... watanzania hatujui tunachokitaka
Kuagiza watuhumiwa wasimamishwe ili kupisha uchunguzi dhidi yao nao huo unaona tutaita udikteta?

Sasa raisi anaeogopa kuchukua hatua kwa masilahi ya umma na taifa eti kwa sababu ataitwa dikteta ni raisi gani huyo?
 
Kuagiza watuhumiwa wasimamishwe ili kupisha uchunguzi dhidi yao nao huo unaona tutaita udikteta?

Sasa raisi anaeogopa kuchukua hatua kwa masilahi ya umma na taifa eti kwa sababu ataitwa dikteta ni raisi gani huyo?
Tushaita mmoja hivyo tukasema ana dhalilisha watu hao watu wana watoto nyumbani..... Huyu mama shida yake anataka kuwapendeza watu wa upande flani anasahau walio mpa kura ni watu wa upande mwingine........ ukiangalia wanaolalamika sana sa hizi ni watu wa upande wake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…