Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Mawaziri ndo wanaiba fedha halafu anasema mawaziri na makatibu wa kuu mtu saidie
 
Khaaa umevuka mipaka mkuu! Tuliza hasira kidogo! Tukosowe kwa staha!
Its true staha peleka kwa mumeo watu wanakata makodo , matozo gharama za maisha zipo juu halafu kuna wwtu wanaenda kukwapua mahela hayo kiurahisa .hivi unajua watakuwa wameua watanzania wangapi unafikiri
 
Hayo yote alikua akiyaweza jiwe Magufuli japo maamuzi yake mliyaona ni utopolo saiv ndo mtaelewa mwendo mzuri wa kuwaendesha Watanzania
Alishaenda zake! Sasa Mkuu kifanyike kipi wakati Mwendazake hayupo?
 
Nani kama Mama?
 
Nani kama Mama?
Mama anashindwa kuwaadhibu baadhi ya watoto wanaowanyonya wadogo zao. Ndomaana tumekuja kumkumbusha wajibu wake kama mzazi.
 
Rudi kasome kuanzia uraia, civics, GS, DS, hadi political science.
Wenye nguvu ni wananchi ndani ya nchi Wao ndo wanaamua waongozweje!
Wananchi wa nchi gani???? kwa nyie mliokuwa shule ndio mnavyofundishwa mambo yenu ya kusadikika huku mtaani
 
Kuna shida ya elimu ya utawala wa sheria , hata kama hayo mamlaka Rais anayo haipi jukumu la kutoa amri,Kamata, weka ndani,ndiyo mtu aende mahakamani Rais anatufundisha juu ya Ubutu wa taasisi zetu za haki jinai na uchunguzi,nadhani kuna haja CAG report na PCCB report itungwe sheria kali mtu wa watu wakitajwa kuhusika na wizi wa mali za umma basi siku hiyo watajwe na wawekwe kizuizini kwanza.
 
Wananchi wa nchi gani???? kwa nyie mliokuwa shule ndio mnavyofundishwa mambo yenu ya kusadikika huku mtaani
Kenya baada ya wananchi kuandamana mfululizo bila kujali ukatili wa polisi... Imefikia hatua Ruto kaomba Pause!
Wakumbusheni wananchi umuhimu na ukuu wao kwenye nchi! Msiwakatishe tamaa!
 
Na hao internal auditors ndiyo wanafanya michongo na wakuu wa wa wizara, kurugenzi na taasisi za umma
Sasa hapa Audit inatoa Ukweli? Hakuna anayekubali kufa Njaa. Yaani hakuna Mkate Mgumu mbele ya Chai ya Moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…