Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Hao wanaokufa siyo raia wa nchi yake ya Zanzibar. Huku kaja kuchuma tu
Mbona mnapokea ruzuku za miaka ya nyuma hamsemi mnachuma, acheni Lugha za ubaguzi Mnatia aibu sana
 
Magu asingesafiri ninauhakika 200000% yule baba kwanza hakua na tatiba za misele ya nje kwahio hio ratiba isingekuwepo pia
Hapo kwa lile shetani lenu la Chato lingeshaifanya hiyo ni fursa ya kupiga michango ya wadau.
Refer ya Kagera
 
Mtoa mada una mawazo ya kipumbavu,yani Rais wa nchi ahirishe shughuli za kitaifa kisa watu waliofukiwa na kufa kutokana na jengo
 
Hivi umeziona nondo zilizojengewa kwenye lile jengo? Umeona wingi wa michanga kwenye lile jengo? Waliochimba basement walipewa kibali na nani? Roho za waliokufa kwa uzembe wa wachache zitalipwa na nani?
Kwahyo unataka mm nifanyeje?
 
Hivi umeziona nondo zilizojengewa kwenye lile jengo? Umeona wingi wa michanga kwenye lile jengo? Waliochimba basement walipewa kibali na nani? Roho za waliokufa kwa uzembe wa wachache zitalipwa na nani?
Unatawaliwa Sana na chuki kwahyo wakifukuzwa kazi hzo nondo zitaongezeka size?
 
Afanye nini?
Kweli kabisa!
Wacha tuendelee kula nyama maana mtori wanasema upo chini
kwenye maafa unakuja na njaa na mitori yako ya nyama gentleman?

uko sawa kweli, au hang over?🐒
 
Ninaandika post hii ni saa 9 kasoro usiku machozi yananitiririka nashindwa kulala nipo nimeshika biblia na Quran hapa nashindwa hata la kufanya

Roho inaniuma maana kuna ndugu zetu wapo chini ya vifusi hadi muda huu na wanapigiwa simu zinaita wanalia tu na kutuma voice za huzuni za kuomba msaada[emoji24][emoji24].

Kuna binti yupo chini ya kifusi huko na ni mjamzito hapa nashindwa hata niandike nini

Rais anapata wapi nguvu ya kusafiri?Hiyo nguvu ya kupanda ndege hadi Brazil kaitoa wapi? Its shame and disgusting!! Yaani nyumbani watoto wako wapo chini ya kifusi halafu wewe kama mzazi unaenda kwenye sherehe ya jirani serious??

Sisemi kwa ubaya lakini Rais wetu kwa hili kakosea sana!!kaonesha ni jinsi gani asivyojali hili taifa!! Kaonesha ni jinsi gani asivyo na huruma na raia wake?

Huo mkutano una umuhimu kuliko roho za mamia ya watu walio chini ya kifusi?Rais amepata wapi huu moyo?nawaza nakosa jibu kabisa[emoji24]

Roho inaniuma mnoo!! Kwa hili rais Samia umekosea pakubwa mnoo!! its shame ni aibu mnoo na dharau kubwa kwa taifa hili.

PIA SOMA
- PICHA: Rais Dkt. Samia aelekea Brazil kushiriki mkutano wa G20
Duh...
Aisee...maza anasafiri aisee..
Sio poa
 
kwenye maafa unakuja na njaa na mitori yako ya nyama gentleman?

uko sawa kweli, au hang over?🐒
We jamaa uko na shida kubwa sana. Unajua binafsi Naunga mkono yeye kwenda alikoenda maana hii itaamsha uwajibikaji wa wanaobaki. Sio lazima awepo maana Kama kutokea ishatokea hakuna namna ya kufanya isitokee
 
nadhani marekani limetokea tukio kama hilo,

Rais Joe au Trump akafanye nini eneo la tukio na uokoaji unaendelea? :pulpTRAVOLTA:
Hii sio akili na huo sio uungwana bali ni roho ya kuto kujali , Rais wa nchi ni sawa na baba wa familia, utakuwa baba wa ajabu sana familia ipo kwenye matatizo halafu baba huonekani eti kwa vile nyumban kuna wajomba, mabinamu na mama wadogo.pamoja na upendo wetu kwa Mama lakini tusikose hekima

Hakukuwa na ugumu wowote kwake hata kwenda eneo la tukio hata kutoa pole na kuhamasisha shughuli za uokoaji yeye kama kiongozi mkuu wa nchi, Halafu akaendelea na ratiba zake
 
Mwandishi wa habari badala ya akimbie chap kufikisha taarifa za mahali waliponaswa, ndo kwanza anawauliza wahanga hali zenu zikoje!
Waandishi wengine ni zero brain !
Mimi sikumuelewa alikuwa anauliza swali au alikuwa anatania !
Hali zenu huko chini ya kifusi zikoje ?
Kauliza zaidi ya mara tatu lakini jamaa hakumjibu ! Alitegemea ajibiwe -: poa tu 🙄😳 ! 😱 !
 
chadema msipende kuibuka kwenye matukio mnaonekana watu wa hovyo sana hamjui tuh
 
Hii sio akili na huo sio uungwana bali ni roho ya kuto kujali , Rais wa nchi ni sawa na baba wa familia, utakuwa baba wa ajabu sana familia ipo kwenye matatizo halafu baba huonekani eti kwa vile nyumban kuna wajomba, mabinamu na mama wadogo.pamoja na upendo wetu kwa Mama lakini tusikose hekima

Hakukuwa na ugumu wowote kwake hata kwenda eneo la tukio hata kutoa pole na kuhamasisha shughuli za uokoaji yeye kama kiongozi mkuu wa nchi, Halafu akaendelea na ratiba zake
Rais na kipenz cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan ndie kiongozi wa kwanza kutoa pole,

na ndie ambae maagizo na maelekezo yake yanatekelezwa hivi sasa na kamati ya maafa kitaifa chini ya waziri mkuu.
Gentleman,

Kwa akili zako timamu kuna muujiza gani anaweza kufanya zaidi ya kiwango hicho cha juu sana cha uwajibikaji, kujali na ungwana kwa wahanga wa kuporomoka kwa jengo kariakoo?

umetoka wapi kwanza gentleman leo?
Kuna ajali zinapoteza makumi kwa mamia ya waTanzania, kazi yako huwa ni kuforwad picha na video mbaya mbaya tu, leo hii hiyo huruma umeitoa wapi mnafiki na jeuri mkubwa wewe? Hebu nenda ukatubu?

Mwenyezi Mungu atujaalie subra wakati zoezi la uokoaji likiendelea kwa umakini na weledi mkubwa. Mungu atuonyeshe njia 🐒
 
Back
Top Bottom