Ninaandika post hii ni saa 9 kasoro usiku machozi yananitiririka nashindwa kulala nipo nimeshika biblia na Quran hapa nashindwa hata la kufanya
Roho inaniuma maana kuna ndugu zetu wapo chini ya vifusi hadi muda huu na wanapigiwa simu zinaita wanalia tu na kutuma voice za huzuni za kuomba msaada[emoji24][emoji24].
Kuna binti yupo chini ya kifusi huko na ni mjamzito hapa nashindwa hata niandike nini
Rais anapata wapi nguvu ya kusafiri?Hiyo nguvu ya kupanda ndege hadi Brazil kaitoa wapi? Its shame and disgusting!! Yaani nyumbani watoto wako wapo chini ya kifusi halafu wewe kama mzazi unaenda kwenye sherehe ya jirani serious??
Sisemi kwa ubaya lakini Rais wetu kwa hili kakosea sana!!kaonesha ni jinsi gani asivyojali hili taifa!! Kaonesha ni jinsi gani asivyo na huruma na raia wake?
Huo mkutano una umuhimu kuliko roho za mamia ya watu walio chini ya kifusi?Rais amepata wapi huu moyo?nawaza nakosa jibu kabisa[emoji24]
Roho inaniuma mnoo!! Kwa hili rais Samia umekosea pakubwa mnoo!! its shame ni aibu mnoo na dharau kubwa kwa taifa hili.
PIA SOMA
-
PICHA: Rais Dkt. Samia aelekea Brazil kushiriki mkutano wa G20