Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Kwanza, rais kasemaje?

Tuhakiki maneno aliyosema kwanza.
 
”Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. ” Sio maneno yangu.
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
 
I thought so.

Maneno halisi aliyosema rais yako wapi?
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
Hayuko sahihi kabisaaa!!!

Kwasababu sheria inasema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana wajibu wa kusikiliza Rufaa zoote na kuzitolea maamuzi yenye haki.
 
Hayuko sahihi kabisaaa!!!

Kwasababu sheria inasema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana wajibu wa kusikiliza Rufaa zoote na kuzitolea maamuzi yenye haki.
Maneno verbatim aliyosema yako wapi?
 
Kwa kiasi gani unaijua Tume ya Utumishi wa Umma??
Unaijua Tume ya Utumishi wa Umma??
Ushawahi kupeleka rufaa yako pale??
Kama ulionewa (Kabla ya tamko hili la Rais) ulikata rufaa kwa Mh. Rais kupinga uamuzi wa Tume? Je, kama Tume ilikuonea Ulishinda rufaa yako Kwa Mh. Rais??

Tuanzie hapa kwanza
 
Nakubaliana na ww mkuu kuwa Rais anafauata taratibu... Lakini kama kuna mwanya wa kukata rufaa ina maana tume ya utumishi imeonekana kuna muda inaweza kufanya maamuzi ambayo sio sahihi sasa unaposema kuwa kesi ikishaamuliwa kule isifike kwake tena inatoa nafasi kwa waajiri na watuimishi wa tume kufanya maamuzi kwa manufaa yao maana wanajua maamuzi yao hata ukiyakatia rufaa hayatabadilishwa! Kikubwa kama ni hivyo ajitahidi kuweka watu wenye weledi basi kuliko hawa ambao kutwa wanalalamikiwa kuwabeba waajiri na hakutakiwa kuyaongea yale mbele za watu... Nipo kusahihishwa
 
waOhoooo kwani nchi haina Labour Court?au commission ya usuluhishi?kama hatuna ni muhimu tuwe na taasisi hizi mbili na kwa president sio jukumu lake kabisa

Labour court kwa mashauri ya watumishi wa Umma hufuata baada ua uamuzi wa Rais dhidi ya Maamuzi ya Tume. Halafu baada ya mabadiliko ya Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 watumishi wa umma, hawahudumiwi na CMA tena.
 
magufuli tunakubaliana kuna mazuri amefanya ila tu mabaya ni mengi mno na mazito. elewa hilo kwanza.
Pili , hebu eleza mwisho wa kesi za utumishi katika mhusika kutafuta haki ni wapi? tuanzie hapo
 
Kama hawamuumizi kichwa anakuja mwz kufanya nn.anajua umuhimu wa mwz sana
Jinga wewe, kwani Mwanza ipo Uganda???! Ivi unadhani kwa Tanzania Rais anategemea kura za kwenye sanduku ili ashinde, Tena mkizingua na mkong'oto tutawapa na kura Mwanza mtatupa kwa 100%
 
Rais anayo mamlaka ya kusikiliza rufaa yoyote ile hata kama imetoka court of appeal... Ndio maana anawasaidizi. Na katiba imempa mamlaka ya kusamehe mtu kama ametiwa hatiani na mahakama. Rufaa au malalamiko yanaruhusiwa kupelekwa kwa Rais. Labda itokee rufaa ni ya kitoto.. ndio maana ilitolewa mfano mtu hajaonekana kazini wiki mbili bila taarifa kisha unakata rufaa kwa Rais inakuwa unapoteza muda.
 
Aifanyie amendment public service act maana Hilo ni takwa la kisheria maana kwa watumishi wa Uma maamuzi ya Rais ndio Final, baada ya hapo mtumishi anatakiwa kwenda mahakama kuu akitaka. Kwa judicial writs.

Ama la afanye amendment ili watumushi wa uma wote waende CMA.
 
Kisheria, rufaa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma inapelekwa kwa Mhe. Rais. Kwa kuwa watumishi wataendelea kufuata sheria, rufaa zitaendelea kupelekwa kwa Mhe. Rais. Labda kama rufaa husika 'hazitafika' au kufanikiwa ziendako.
Fanyeni kwamujib washeria yoote hayo yarufaa na nk hayatatokea
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
Rais ni Taasisi wala siyo mtu. Sheria za kazi ni fani inayosomewa chuoni au katika LLB, au HR au Industrial Relations.

Kwenye kifungu 25 (1) (d) ya Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya 2002, wanaposema Mfanyakazi ambaye hakuridhika naaamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma atakata Rufaa kwa Rais, maana yake Rais ndiye mamlaka. Lakini Rais ana Ofisi yake ya Katibu Mkuu Kiongozi ambayo ina wataalamu wote wa nyanja ambazo Rais anahitahi ushauri.

Baada ya barua kupokelewa, wataalamu wa Ofisi ya KMK wataipitia rufaa, watatafuta kumbukumbu kwa Mwajiri na Tume ya Utumishi na kuchanganua.

Kisha watatoa hitimisho/ pendekezo ambalo ndilo Rais atalisoma na kuandika "Nakubali" au "Sikubali".

Rais kimsingi kama binafsi hafanyi kazi ya kuchambua bali ni timu iliyo ofsini kwa KMK
 
Kama Samia anaona Uraisi ni Mgumu basi kwa heshima na taadhima aachie kijiti mwaka 2025, Lakini kiukweli kabsia na kwa mujibu wa katiba yeye ni mkuu wa utumishi wa Umma nchini na anapaswa kuwasikiliza watumishi. AACHE UVIVU!
 
Bila katiba mpya tutapata shida haswa kwa hawa watawala wa CCM, dawa yao ni kuwaendea kwa waganga wa kienyeji mnamalizana bila lawama.

Sasa Naanza Kuelewa Umuhimu wa katiba Mpya....
Mwanzo sikuona Umuhimu kwasababu Niliona Hata Katiba Mpya Ikiwepo Na Aliekuwepo asipoitekeleza nani atamfanya nini?
Haya yalikuwa Mawazo yangu!
Kwamba Unaweza kuwa na Katiba Mpya na Kama Haifuatwi?
Yaani unaweza kuwa na Katiba ya sasa na Haifuatwi sasa utadai Mpya ili iweje?
Huu ni Mfano tuu!
PIA Nadhani Tume haiko independent,Inaogopa Gharama kama Mtumishi Ana Haki...Yaani Kurejeshewa stahiki zake...
Wanaona hiyo hasara italipa Serikali,Na Serikali inawakilishwa na Tume!
Soma Paragraph hii ya Mwisho Utaelewa ndio kwenye ujumbe Mzito kwanini Tume inaogopa/
Sababu ni Part and Parcel ya Serikali Yaani Kuna Link kati ya Utumishi na Tume!
Mfano Kenye Judge yuko Independent uneona Juzi Jaji Mkuu Mwanamke kamuonya Kenyatta Kuchagua Majaji waliobaki kwa Mujibu wa Katiba!
Hapa Kwetu Vyombo hivyo Haviko Independent 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…