Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Kibondo katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Kibondo Mkoani Kigoma, leo tarehe 16 Oktoba, 2022.
Rais Samia akiwa kigoma amesema wanaenda kuzima majenereta huko Kigoma kuwa kuwa Kigoma inaenda kuunganishwa na gridi ya taifa hivyo itapata umeme wa uhakika kwa muda wote. Rais amesema mkoa huo unapakana na nchi kadhaa mabpo ni vizuri kuboresha huduma za nishati kwa kuwa nchi jirani zinaweza kuja kununua umeme kutoka Tanzania.
Katika hatua nyingine Rais amezungumzia miradi ya maji na barabara pamoja na kilimo iliyowekwa katika Mkoa huo. Kuhusu kilimo amesema watu wataanza kufanya kilimo cha umwagiliaji kutokana na uwekezaji utakaowekwa katika sekta hiyo.
Rais Samia yupo Kigoma kwa ziara ya kikazi na amesema ziara hiyo ilicheleweshwa kiasi kutokana na kifo cha malkia wa Uingereza