Rais Samia kila akisifia mazuri yaliyofanywa na Hayati Magufuli; Nderemo, shangwe na makofi hutawala. Hii ina maana gani?

Rais Samia kila akisifia mazuri yaliyofanywa na Hayati Magufuli; Nderemo, shangwe na makofi hutawala. Hii ina maana gani?

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
Asalaam Aleykum wapendwa wana jamvi. Ama baada ya salamu hizo napenda kuishukia mada tajwa hapo juu kama ifuatavyo;

Nimefanya utafiti kulingana na kiwango changu cha elimu nilichonacho, nikagundua kwamba, kila mara Mh. Rais, mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hasani akimtaja mtangulizi wake kwa mazuri, basi umati wa watu hulipuka kwa nderemo, vifijo, shangwe na makofi.

Sasa nimekuwa najiuliza mwenyewe hapa, hivi ni kwa nini hali hiyo itokee? Halafu mbona baadhi ya watu wakimsema vibaya Hayati JPM, watu wengi ni kana kwamba huwa wanaingiwa na simanzi?!

Anyway naomba msaada kwa yule anayeweza kuniwekea ushahidi hapa wa zile video clips za wakati mradi wa Bwawa la Nyerere (JNHEP) linafunguliwa na ule Mkutano wa Mh. Rais Samia na Viongozi wa wanavyuo uliofanyika majuzi, aziweke hapa ili walau kuongezea nyama nyama kwenye mada yetu.

Ahsanteni na karibuni sana kwa maoni na matusi (maana kuna wengine bila kutukana, hajachangia)..

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Afrika Mashariki, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jamiiforum na members wake wote, Mungu nibariki na mimi mtoa mada pia

AMINA.
 
We unafikiri kuna mwananchi ambaye hawezi kufikiri kwa kina kuhusu haya maisha, kukatika kwa umeme, mfumuko wa bei, viongozi kupiga pesa kwenye miradi na hata kutokuwajibishwa kwa viongozi wazembe?
Kiukweli inafikirisha sana, hata kama nilikuwa simkubali jamaa lakini alikuwa na mazuri yake
 
Kwa hiyo viongozi waliopo madarakani badala ya kutumia muda mwingi kumnanga Hayati, wangeutumia kutatua kero za jamii!
Shukrani sana kwa maoni yako Mkuu
 
Anauliza kwa kuwa anaona vimelea vya tabia za kuigawa jamii🤔
Basi Hayati aachwe kabisa pasipo kusemwa kwa mema au kwa mabaya kama suala ni kuigawa jamii. Maana kwa hiyo hali ni kana kwamba wengi walimwelewa sana "jiwe"!
 
Bwana yule nikikumbuka tu kwamba alikuwa anatembea na mabegi ya pesa kwenye ziara zake sijui alikuwa analenga nini?Kama ni kutatua matatizo ya watu papo kwa papo je matumizi ya fedha za umma yanatakiwa kufanyika kwa style hiyo ya kugawa kwa watu unaojisikia?
 
Sahau kuhusu sheria za pesa za umma.
Nchi hii ipo ilipo sasa kwasababu ya sheria hizo hizo!

Tukiendeleza huo upumbavu, tutaendelea hivi hivi!

Tukiendelea na habari za demokrasia na utawala bora wa kuambiwa na weupe, tutaendelea kuwa weupe.

Tukiendelea na utaratibu wa haki za binadamu na kusahau kuwa wengine waliendelea kwa kutumia UTUMWA ambao ndio wakina MSOGA na the like wanaendelea kuutumia, tutakuwa kama wanyama wa kwenye Zoo.

Kwasasa, jinsi ilivyo, wenye pesa na madaraka nchini ndio MIUNGU, wasomi ndio kina MWIJAKU.
 
Nilishasema policy ya huyu ni Ile Ile,kusifia marehemu akiwa ndani ,kumponda akiwa nje..ni win win situation kwake..ila kwa jinsi wapiga Kura wa tz walivyokuwa hamnazo,they fall for this act every time.
 
Hivi alifanya kwa kutoa pesa mfukoni mwake,? Uyu alikua tapeli kwa wenyenchi
Hakufanya aliyoyafanya kwa kutoa mfukoni kwake. Hiyo pesa ilikuwa ya waliupa kodi na kazi yake ndiyo hiyo. Lakini alipoondoka hiyo pesa ya kodi sasa inadokolewa mno na viongozi wa zamani wa CCM pampja na wababaishaji wao kama Makamba, Nnauye, Mwigulu, Msoga Gang. pamoja na yule jizi kuu ambaye ana mameli yanayofanya biashara za magendo na madawa kila kukicha (vice chair CCM). Mama angetumia busara na kuachana na wale watu walikuwa wanamtukana JPM hadharani na asingeulizwa na yeyote kana rahisi. Lakini yeye alionyesha chuki yake kwa JPM kwa kuteua wale waliyokuwa wanamtukana mkuu wake wa kazi. Hawa ndiyo walishusha heshima ya mama. Kwani ilikuwa lazima wateua hao. Kosa kubwa na pale alipoanza kumsikiliza mwenyekiti wa Msoga Gang. Pale aliteleza kweli. Alafu sasa ndiyo wake na Makamba senior na junior wakaanza kumdanganya. Msoga Gang ilihakikisha anateua "'weak people" kama Makamba, Nnauye, na Mwigulu" ambao watampa total loyalty. Kwa vile hao waliishajifunza yaliyowapata walipojaribu kufurukuta na kumtukana JPM, walishikishwa adaba na hawataweza kuwa na kiburi cha kudhania nyadhifa za ndugu zao zinaweza kuwalinda.
 
Sasa wewe ulitaka walie au wazomee?

Hata makanisani Pepo likisutwa waumini hushangilia
 
Basi Hayati aachwe kabisa pasipo kusemwa kwa mema au kwa mabaya kama suala ni kuigawa jamii. Maana kwa hiyo hali ni kana kwamba wengi walimwelewa sana "jiwe"!
Kama CCM inataka kushindwa uchaguzi, wamnage JPM. Mgombea yeyote wa CCM atayemnaga JPM hatashinda kura. Pia CHADEMA hawatapata. Vyama vya upinzani ambavyo havimuongelei JPM huenda vikafaidi kwa uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom