Asalaam Aleykum wapendwa wana jamvi. Ama baada ya salamu hizo napenda kuishukia mada tajwa hapo juu kama ifuatavyo;
Nimefanya utafiti kulingana na kiwango changu cha elimu nilichonacho, nikagundua kwamba, kila mara Mh. Rais, mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hasani akimtaja mtangulizi wake kwa mazuri, basi umati wa watu hulipuka kwa nderemo, vifijo, shangwe na makofi. Sasa nimekuwa najiuliza mwenyewe hapa, hivi ni kwa nini hali hiyo itokee? Halafu mbona baadhi ya watu wakimsema vibaya Hayati JPM, watu wengi ni kana kwamba huwa wanaingiwa na simanzi?!
Anyway naomba msaada kwa yule anayeweza kuniwekea ushahidi hapa wa zile video clips za wakati mradi wa Bwawa la Nyerere (JNHEP) linafunguliwa na ule Mkutano wa Mh. Rais Samia na Viongozi wa wanavyuo uliofanyika majuzi, aziweke hapa ili walau kuongezea nyama nyama kwenye mada yetu.
Ahsanteni na karibuni sana kwa maoni na matusi (maana kuna wengine bila kutukana, hajachangia)..
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Afrika Mashariki, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jamiiforum na members wake wote, Mungu nibariki na mimi mtoa mada pia,
AMINA.