Rais Samia, kiprotokali ni sahihi kumtaja Rais wa Zanzibar kabla ya Waziri Mkuu wa Tanzania?

Rais Samia, kiprotokali ni sahihi kumtaja Rais wa Zanzibar kabla ya Waziri Mkuu wa Tanzania?

John Okelo alikuwa hawashi wala hazimi, alitumiwa kuwarushia changa la macho, Aliyeongoza mapinduzi alikuwa ni Hanga ambaye alihadaliwa na Nyerere pamoja na Kambona mwisho wakampeleka kwa Karume kuuliwa
Sivyo,
Wakati Field Marshal John OKELLO akipambana visiwani kuikomboa Zenji kutoka mikononi mwa Sultani, Kassim Hanga na Sheikh Karume walikuwa wamekimbilia Dar kujificha
 
Presidential protocol ilibadilishwa mwaka 2015. Kabla ya hapo waziri mkuu alikua anamtangulia Raisi wa Zanzibar. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa yalitokana na mkwara wa Waziri Mkuu bungeni kuhusu je, Zanzibar ni nchi au sio nchi. Pinda aliwapa jibu tamu sana.
Tukumbushe jibu lipi?
 
Sivyo,
Wakati Field Marshal John OKELLO akipambana visiwani kuikomboa Zenji kutoka mikononi mwa Sultani, Kassim Hanga na Sheikh Karume walikuwa wamekimbilia Dar kujificha

Aliyeyapanga ni Nani ? Huyo Karume alikuwa hajuwi chochote mpaka dakika ya mwisho ndiyo akapewa taarifa
 
Sifahamu kuhusu hilo lakini nawashangaa wanaouliza. Hivi wanafikiri Rais anajipangia yeye protocol? Hawaelewi kuwa kuna Ofisi nzima ya Rais ina wataalam wa kila aina?

Unajuwa mtu mweusi alijaaliwa akili nyingi sana lakini tatizo ni kajazwa ujinga mpaka akaamini kuwa yeye ni mjinga, matokeo? Hajuwi kuzitumia akili zake.
.
Order of precedence inaandikwa kila Raisi akiingia madarakani. Anaweza kupanga anavyoweza. Ya nchi kama Marekani na Uingereza zinajulikana.
 
Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Rais kisha Rais wa Zanzibar na baada ya hapo ndio akamataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa na kisha akaendelea kutaja wageni wengine waliokuwa wamehudhuria katika tukio hilo.

Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?

Zanzibar si ni sehemu ya Tanzania, sasa iweje Rais wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?

Rais huwa anaandikiwa tu ratiba...
 
Bongo hatari sana🤣, nimesoma comments za page 1 sijaona source yeyote, wajuzi. Kuna source ya katiba ya huu mtiririko?
 
Presidential protocol ilibadilishwa mwaka 2015. Kabla ya hapo waziri mkuu alikua anamtangulia Raisi wa Zanzibar. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa yalitokana na mkwara wa Waziri Mkuu bungeni kuhusu je, Zanzibar ni nchi au sio nchi. Pinda aliwapa jibu tamu sana.
Link
 
Utoto Ukizidi Sana Ni Upumbavu na Upumbavu ukizidi Sana Unakuwa Ni Ulemavu wa Akili na Ulemavu wa Akili ukizidi sana Unakuwa Mfu wa Maarifa..

Sidhani kama Unafaa hata Kupokea Jibu langu la Aina yoyote ile maana Huna Nafasi hiyo..
Nachokushauri Bado una nafasi ya Kujitoa Kwenye Upumbavu na Kurudi kwenye Ujinga ambapo utaweza Kupona Ili usife kimaarifa..

Ilikuwa Ni vyema sana Kukujibu
ASante
Wewe Dr uchwara acha kulilia watu mitandaoni. Hukutumwa ujiunge na JF
 
Katiba ndo kila kitu, mtu mwenye power protocal na hierarchy seniority order lazima imfuate.


Rais wa Zanzibar alikuwa na nguvu pale alipokuwa Makamu wa Rais kabla ya vyama vingi.

By vatue yeye automatically alikuwa makamu wa Rais.

Baada ya vyama vingi yeye mamlaka ya kuwa namba 2 kwa cheo yalikoma uchaguzi Mkuu wa vyama vingi.

Kinachoendelea sasa ni Kumwinua Rais wa Zanzibar,lakini kiukweli kitatiba na muundo wa Serikali waziri mkuu ni Mtu ni Number Tatu, ndio maana hata BARAZA LA MAWAZIRI Rais asipokuwepo ,na makamu asipokuwepo, Waziri Mkuu anakuwa Mwenyekiti wa Baraza.

Kwahiyo kikatiba PM ni Number 3, akiwa chini ya VP.

Nakutakia mkutano Mwema wa TLS huko DODOMA.
Yes kikatiba Waziri Mkuu is No.3, Rais wa Zanzibar is nobody kwenye set up ya Muungano, ni Waziri asiye na Wizara maalum ili aingie cabinet, PM ni boss wa Rais wa Zanzibar, lakini ki protocol Rais wa Zanzibar ni number 3. Hata wale makamo wawili wa Zanzibar, katiba ya JMT, haiwatambui, they are nobody huku, ila protocol inawatambua na vingora wanapewa!.
P
 
Kikatiba Rais wa Zanzibar ni kama Makamu wa Rais wa pili wa JMT ndio maana hata vikao vya baraza la mawazili anaitwa kushiriki akiwepo Rais wa JMT.Katiba ya Tanzania ibara ya 54 kifungu cha kwanza
Haipo hivyo, leta facts za Kikatiba siyo maoni Yako.
 
Waziri Mkuu kikatiba ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar.
Hizo zinafanyikan zinafanyikan makusudi kabisa ku mo overate Rais wa Visiwabvya Zanzibar ambavyo sawa na wilaya Moja huku Bara.

Mamlaka ya Waziri Mkuu, kwenye Baraza la MAWAZIRI ,
Ibara ya 50, kifungu kidogo Cha (I) na Cha (ii) kinaonesha vizuri sana, kwamba KUTAKUWA NA BARAZA LA MAWAZIRI,

Linaundwa na Rais wa URT nayae atakuwa Mwenyekiti, asipokuwepo Makamu wa Rais.

Ikitokea Rais na makamu kwa pamoja hawapo,waziri Mkuu ataongoza kikao Cha Baraza la MAWAZIRI.

Wajumbe wanaounda Baraza la MAWAZIRI.

Mosi Rais, Mbili Makamu, tatu Waziri Mkuu.
Nne MAWAZIRI wote kamili sio manaibu,ni wajumbe, na Rais wa Zanzibar ni mjumbe tu,akiwa anaingia baraza la mawaziri hadhi yake ni sawa na Innocent Bashungwa au Masauni.

Nyongeza ikitokea Rais hayupo nchini Rungu anashiklia Makamu wa Rais, asipokuwepo yeye pia, Rungu atashika waziri Mkuu, naye asipokuwepo atashika speaker wa Bunge, na ikitokea wote hao hawapo kwa pamoja nchi itakuwa chini ya jaji mkuu!

Hapo Rais wa Zanzibar hatajwi.

Kumruka waziri mkuu au waziri mkuu kutangulia kuingia kwenye sherehe za kitaifa katika accending order na descending order yaani order of seniority ni JANJAJANJA tu ya makusudi inayofanyika.

Lakini ni ukiukwaji wa katiba mchana kweupe.

Hayo yanatosha kuelewa hata kwa mwanafunzi wa elimu ya Uraia Civics kuelewa kuwa waziri mkuu ni Mtu Mkubwa sana katika nchi kimamlaka na protocal akiwa chini ya Makamu wa Rais.

Kwahiyo kumdogosha waziri mkuu ni mbwembwe na janjajanja flani ya makusudi.

😅🤔🙏
Waziri mkuu hana mandate ya kushikilia Nchi ikitokea Rais kusafiri basi nchi anapewa Makamu na makamu kama hayupo nchi anapewa Spika wa bunge JMT
Kama hayupo anapewa Jaji mkuu. Waziri mkuu hana sifa ya kuachiwa nchi kwa mujibu wa katiba.
 
Raisi wa Zanzibar ni Mkubwa kuliko Waziri Mkuu kiitifaki. Sehemu yeyote akiwepo Raisi wa Zanzibar, PM anakuwa namba 4.
Kwenye dhifa ya Kitaifa, Waziri Mkuu JMT, hawezi kuongea au kwenda kwenye chakula mbele ya Raisi wa Zanzibar (Kama akiwepo). 😁
 
Yes kikatiba Waziri Mkuu is No.3, Rais wa Zanzibar is nobody kwenye set up ya Muungano, ni Waziri asiye na Wizara maalum ili aingie cabinet, PM ni boss wa Rais wa Zanzibar, lakini ki protocol Rais wa Zanzibar ni number 3. Hata wale makamo wawili wa Zanzibar, katiba ya JMT, haiwatambui, they are nobody huku, ila protocol inawatambua na vingora wanapewa!.
P

Mkuu hautaeleweka humu. Watu wanachanganya Itifaki (Protocol suite) na Daraja (Hierarchical). Mama yupo Sahihi kiitifaki. Mifano ipo mingi tuu, waangalie nani anatangulia Kuzungumza kwenye matukio ya Kitaifa. Ni PM au Raisi wa Zanzibar. Watapata jibu.
 
Mkuu hautaeleweka humu. Watu wanachanganya Itifaki (Protocol suite) na Daraja (Hierarchical). Mama yupo Sahihi kiitifaki. Mifano ipo mingi tuu, waangalie nani anatangulia Kuzungumza kwenye matukio ya Kitaifa. Ni PM au Raisi wa Zanzibar. Watapata jibu.
Kwenye uvamizi /Muungano huu hiyo katiba ni changa la uso tu kudanganya Toto , Tz Hakuna cha katiba wala mavi ya protokoll, kuna vile watawala wanavyojisikia wanavyoamka au kutetea maslahi yao . Hii nchi Haina sheria.
 
Back
Top Bottom